Karibu nikukutanishe na mkulima kutoka Jijini Mbeya Rafael Saimon Ndelwa, Mmiliki wa Kampuni ya Rapha Group iliyo Uyole Mkoani hapo.
Rapha ni miongoni mwa Mabilionea wa Mkoa wa Mbeya na utajiri wake unatokana na Kilimo cha mpunga, kilimo ambacho kilimfanya Bilionea Bill Gate amuite ili waweze kujadili amewezaje kufanikiwa katika kilimo hicho.
Uwezo wake wa kukopesheka na Benki ni zaidi ya BILIONI 3
Raphael Saimon ameelezea kuwa alianza kwa kulima kwa kutumia jembe na kuanza kufanya biashara ya kuuza mpunga katika Mikoa mbalimbali Tanzania na kupelekea kuwa mzalishaji bora wa zao la mpunga kutoka jijini Mbeya.
"Nilikuwa nauza zao la mpunga katika Mikoa ya Tanga, DSM, Morogoro na kuanza kupeleke zao hilo hadi nje ya Tanzania na sababu kubwa iliyopelekea kufanikiwa mpaka hapa ilikuwa nikununua mashine kubwa za kukoboa mchele kutoka nchini India na kuongezeka kwa uzalishaji". Rapha
Rapha anasema Balozi kutoka nchini Marekani ndiye aliyefanya mpango wa kumkutanisha na Bill Gate baada ya kuona mafanikio aliyofikia na kupewa tunzo ya kuwa Mfanyabiashara mdogo na alishindanishwa na wafanyabiashara kutoka Afrika Kusini, Nigeria lakin kupitia kampuni yake RAPHA GROUP akafanikiwa kutwaa tunzo ya mfanyabiashara bora barani Afrika.
Katika maisha nimuhimu kujituma ilikufanikisha ndoto za maisha yetu Pia na serikari iwena msaada kwa wafanyabiashara ilikufanikisha malengo ya wananchi wake wanafanikiwa.