Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 129
'Bilionea' Chenge akimbia waandishi
*Alitoka mkutanoni Hoteli ya Kempinski Dar
* Waandishi wakamfuata hakusimama
* Alipopigwa swali alisema, "Siongei chochote'
* Akapanda gari na kuondoka zake
Na Muhibu Said
UAMUZI wa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kukataa kujibu tuhuma zinazomkabili za kumiliki mabilioni ya fedha nje ya nchi, umeingia katika sura mpya, baada ya kuwakimbia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Chenge ambaye anatuhumiwa kumiliki dola za Marekani 1 milioni (Sh1.2 bilioni) katika mazingira tata, alifikia hatua hiyo baada ya kukataa kujibu maswali ya waandishi wa habari kwa muda mfupi baada ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa nchi 19 duniani kuhusu Udhibiti wa Vitendo vya Uharamia na Uvamizi dhidi ya Meli zinazopita katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, uliofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, jijini Dar es Salaam, Aprili 14-18, mwaka huu.
Mara baada ya kufunga mkutano huo, alitoka nje ya ukumbi wa mkutano na mwandishi wa gazeti hili alimfuata na kumwomba kufanya naye mahojiano kidogo lakini alimkatalia.
Chenge, ambaye jana alionekana kuzidisha umakini na kuchukua tahadhari kubwa kwa waandishi wa habari, awali, alitaka kumfahamu mwandishi aliyemkabili na chombo cha habari anachotoka.
"Kwanza, wewe ni nani?" aliuliza Chenge na kujibiwa na mwandishi: "Mimi ni mwandishi wa habari."
"Wa chombo gani?" aliuliza tena.
"Wa gazeti la Mwananchi," alijibu mwandishi.
"Enhee, unasemaje?" alimuuliza tena.
Mwandishi alimweleza kuwa anataka aeleze kama ameshatekeleza azma yake aliyoitangaza alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, kwamba atawasiliana na mwanasheria wake ili avichukulie hatua za kisheria vyombo vya habari alivyodai kuwa vimevuka mipaka katika kuandika na kutangaza tuhuma dhidi yake pamoja na ufafanuzi wa kauli yake ya kuziita Sh1.2 bilioni kuwa ni "vijisenti" anazotuhumiwa kujipatia kwa njia zisizohalali na kuzihifadhi katika kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza.
Akajibu kwa ufupi akisema: "Siongelei chochote," huku akitembea na kushuka kwenye ngazi za hoteli hiyo kwenda mahali lilipoegeshwa gari lake.
Jibu kama hilo, Chenge alilitoa pia kwa waandishi wengine waliomfuata hotelini hapo kumuuliza maswali mbalimbali.
Hali kama hiyo pia iliwakuta waandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) waliotaka kuhojiana naye huku wakimwelekezea vinasa sauti lakini alipunga mkono kuashiria kukataa kuzungumza na kuingia kwenye gari lake.
Baada ya kuingia kwenye gari lake, aliwaambia waandishi wa habari: "Mvua zinatusumbua," kisha akafunga mlango wa gari na kumuaru dereva wake kuondoka.
Tuhuma dhidi ya Chenge za kujilimbikizia fedha hizo, ziliibuliwa na gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza katika toleo lake la Jumamosi wiki iliyopita ambalo lilieleza kuanza kwa uchunguzi dhidi yake, kutokana na akaunti yake kukutwa na zaidi ya dola za Marekani 1 milioni.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai nchini humo ya Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa pauni za Uingereza milioni 28, ambazo ni sawa na Sh70 bilioni, mwaka 2002.
Gazeti hilo lilieleza kuwa uchunguzi huo wa SFO unatarajiwa kuanza katika kipindi cha wiki sita zijazo.
Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, moja ya mambo yanayofuatiliwa ni kujua iwapo fedha hizo zinazoaminika kuwa za Chenge, zilizowekwa katika akaunti moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutoka katika Kampuni ya BAE System, inayotuhumiwa kuinyonya Tanzania kwa kuiuzia rada kwa bei kubwa kuliko ilivyotakiwa.
The Guardian katika habari yake hiyo iliyowekwa katika mtandao wa intaneti, liliripoti kuwa taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.
Gazeti hilo lilimkariri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni mali yake, lakini alikanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu.
Siku moja baada ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa taarifa rasmi zikifika serikalini kuhusiana na tuhuma hizo, sheria itachukua mkondo wake na kuonyesha kushangazwa kwake iwapo Chenge alizipata fedha hizo kihalali au la.
Siku moja baadaye, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kumtaka Rais Jakaya Kikwete amsimamishe kazi Waziri Chenge na awekwe chini ya ulinzi, wakati uchunguzi wa kina wa mali zake ndani na nje ya nchi unafanyika.
Alisema anamfahamu vema Waziri Chenge na kwa hiyo, mshahara na marupurupu ya serikali anayolipwa, havimwezeshi kulimbikiza kiasi hicho cha fedha katika akaunti.
Kabla ya gazeti la The Guardian kuibua tuhuma hizo, Septemba 15, mwaka jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, walimtaja Chenge katika orodha ya vigogo kumi na moja, wakiwamo viongozi kadhaa wa serikali nchini wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi wa mabilioni ya shilingi za walipakodi.
Baadaye Septemba 19, Waziri Chenge aliliambia gazeti hili kuwa walioibua hoja ya ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali kama wakipata au kama wana ushahidi, yeye binafsi anatoa ruksa waupeleka katika vyombo husika vya dola ili ufanyiwe kazi.
Hata hivyo, Chenge alithibitisha kwamba yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Tangold, ambayo inamilikiwa na serikali na kwamba hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia kuwa mkurugenzi.
"Nasubiri nipate hizo tuhuma kwa maandishi maana siwezi kuzungumza tu bila kuziona, lakini kama ni ukurugenzi Tangold, mimi siyo kwamba niliwahi kuwa mkurugenzi, ni mmoja wao mpaka sasa. Hii ni kampuni ya serikali, tatizo nini?" alihoji Chenge.
Waziri huyo alisema hapendi malumbano, isipokuwa yote yaliyozungumzwa atahitaji kuyaona kwa maandishi na uonyeshwe ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja na ufisadi uliotajwa.
Februari 12, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitangaza Baraza jipya la Mawaziri baada ya Februari 7, kulivunja baraza la awali ambapo baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliachwa na kumteua Chenge kuendelea na wadhifa wake katika Wizara ya Miundombinu.
Hata hivyo, uteuzi wa Chenge kuendelea na wadhifa aliokuwa nao katika wizara hiyo, ulizua mjadala mkali kutoka kwa wananchi, ambao walidai kuwa hafai kutokana na kuhusika kwake na mikataba mibovu akiwa Mwanansheria Mkuu.
Pia baadhi ya wananchi walisema tangu ashike wadhifa huo mwaka 2005 hakuna mabadiliko katika ujenzi wa barabara zaidi ya mafanikio na ufanisi vilivyoachwa na serikali ya awamu ya tatu, ambayo John Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi.
Pamoja na malalamiko hayo ya wananchi, Chenge aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kujiuzulu kutokana na maneno ya watu na kwamba suala la yeye kuendelea kukaa katika baraza hilo aulizwe Rais Kikwete ambaye ndiye alimteua.
Source: Mwananchi