KAMATI ndogo ya Ulinzi na Usalama wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar kuwapa waandishi wa habari elimu ya haki zao

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
473
699
Na Waandishi wetu Tunu Bashemela na Abrahamu Ntambara

KAMATI ndogo ya Ulinzi na Usalama wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam imeazimia kuendelea kuwapa waandishi wa habari elimu ya namna gani wanatakiwa kujua haki zao za msingi wanapokuwa wakitekeleza majuku yao, Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Faraji Mangula akizungumza baada ya kikao hicho kilichofanyika Kigambon jijini Dar es Salaam.
IMG-20240715-WA0042.jpg

"Tumejadiliana ni namna gani waandishi wa habari wanatakiwa wawe wanajua haki zao na majukumu yao katika kufanya kazi, na pia haki zao za msingi wakati wa kazi hizo. Tumejadili mambo mbalimbali, lakini pamoja na mambo mengine tunakubaliana kuendelea kuwapa waandishi wa habari elimu ya namna ya kufanya kazi zao, namna ya kuhusiana na vyombo vingine vya kiserikali pamoja na mahusiano kwa ujumla yawe mazuri wanapotekeleza majukumu yao," alisema Wakili Mangula na kusisitiza,
"Kwahiyo tulijadiliana kwamba waandishi wa habari sio maadui ila ni watu wanaofanya kazi zao ya kuihabarisha jamii, kwahiyo ni vyema wakawa na mahusiano mazuri na hiyo jamii wakiwemo viongozi wa kiserikali na vyombo vyote vya kidola,".
IMG-20240715-WA0039.jpg

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Askofu Emmaus Mwamakula alisema wamekubaliana kutekeleza majukumu yao na kamba watawasaidia waandishi wa habari kwa kuhakikisha wanakuwa salama kwa kuzingatia Sheria za nchi ambapo wapo huru kwenye nchi yao na wana haki ya kulindwa na haki ya kuwa hai wakati wakitekeleza majukumu yao.

Alieleza kuwa kikao hicho kilikuwa ni cha kwanza ambapo Kamati hiyo inajumuisha Waandishi wa Habari, Vongozi wa Dini, Mawakili na Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Dar es Salaam."Kwahiyo kikao kilikuwa na mambo kadhaa kwanza, tulikuwa tuchague uongozi ambao tumefanikiwa, lakini pia kuweka mikakati ya kwenda mbele na mipango mbalimbali jinsi ya kuenenda katika kipindi ambacho kina fuata, hilo tumejadili tumekamilisha, lakini na mambo mengine ambayo yametokea, hasa kikubwa pia ya kutoa elimu kwa waandishi wa habari na kuwatia moyo katika kazi zao ili wanapopata madhira wafanye nini na hatua gani zichukuliwe na sisi tunaweza tukawasaidia kwa namna gani," alisema Askofu Mwamakula.
IMG-20240715-WA0037.jpg

Kwamba Kamati hiyo itaweza kupunguza misuguano kunapotokea tatizo lolote kwa mwandishi wa habari ambapo wataweza kuwasilisana na Serikali ama Jeshi la polisi au kwa wanamna yoyote ile kwa kutumia wanasheria na kutoa msaada.
Kadhalika Kamati itajenga undugu na ushirikiano ili jamii isiwaone waandishi wa habari kama maadui na waone waandishi wa habari kama watenda kazi na muhimili mwingine wa dola katika utendaji kazi duniani.

"Tumetoka na azimio moja muhimu juu ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari hususani kwa mkoa wa Dar es Salaam, na kubwa tunajua ya kwamba moja ya azimio ambalo tumeliazimia ni kuhakikisha usalama wa waandishi ni kipaumbele namba moja wanapokuwa wakitimiza majukumu yao," aliongeza Askofu Mwamakula.

Hivyo Kamati imeona ya kwamba ni vyema mamlaka zinazohusika ikiwemo Jeshi la Polisi na viongozi mbalimbali wa ngazi zote kushirikiana na waandishi wa habari na kuto wabughudhi wakati wakitekeleza majukumu yao.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) ambaye pia ni Katibu wa Kamati hiyo Fatma Jalala alisema kiako hicho kimefana kwani kimefanyika kwa kuzingatia malengo yale yale ambayo yalikuwa yamepangwa.

Kwamba pamoja na mambo mengine Kamati ilijadili juu ya madhira aliyopata hivi karibuni mwandishi wa habari Dickson ambapo Kamati itakuja na mapendekezo ya nini kifanyike na kwamba kabla ya mapandekezo hayo kutafanyika uchunguzi ili kubaini ukweli juu ya jambo hilo.

Kamati hiyo inaundwa na watu sita (6) ambao ni Mwenyekiti wake Wakili wa kujitegemea Faraji Mangula, Makamu Mwenyekiti Askofu Emmaus Mwamakula pamoja na wajumbe Ntimi Charles Mkurugenzi wa Taasisi ya ‘The Right Way’ na Twende Pamoja, Sheikh wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu kwa niaba ya Sheikh wa Mkoa Sheikh Walid Alhad, Bakari Kimwanga mwanachama wa DCPC, SACP John Malulu RPC wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, ambapo katibu wa kamati hiyo ni Fatma Jalala.

Kamati hiyo iliundwa Machi 22, 2024 kwa lengo la kushughulikia masuala ya ulinzi na usalama kwa Waandishi wa Habari kuhusu madhira mbalimbali yanayowakumba wanapokuwa katika majukumu yao ya kila siku, kukuza ushirikiano na mahusiano kati ya jamii, waandishi wa habari na Jeshi la Polisi ili kuchangia ukuaji wa ulinzi na usalama kwa waandishi hao.
Lakini pia kuhakikisha kamati inatoa msaada wa haraka na wenye ufanisi kwa matukio yanayohatarisha usalama wa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom