'Bilionea' Chenge akimbia waandishi

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
'Bilionea' Chenge akimbia waandishi

*Alitoka mkutanoni Hoteli ya Kempinski Dar

* Waandishi wakamfuata hakusimama

* Alipopigwa swali alisema, "Siongei chochote'

* Akapanda gari na kuondoka zake


Na Muhibu Said


UAMUZI wa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kukataa kujibu tuhuma zinazomkabili za kumiliki mabilioni ya fedha nje ya nchi, umeingia katika sura mpya, baada ya kuwakimbia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.


Chenge ambaye anatuhumiwa kumiliki dola za Marekani 1 milioni (Sh1.2 bilioni) katika mazingira tata, alifikia hatua hiyo baada ya kukataa kujibu maswali ya waandishi wa habari kwa muda mfupi baada ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa nchi 19 duniani kuhusu Udhibiti wa Vitendo vya Uharamia na Uvamizi dhidi ya Meli zinazopita katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, uliofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, jijini Dar es Salaam, Aprili 14-18, mwaka huu.


Mara baada ya kufunga mkutano huo, alitoka nje ya ukumbi wa mkutano na mwandishi wa gazeti hili alimfuata na kumwomba kufanya naye mahojiano kidogo lakini alimkatalia.


Chenge, ambaye jana alionekana kuzidisha umakini na kuchukua tahadhari kubwa kwa waandishi wa habari, awali, alitaka kumfahamu mwandishi aliyemkabili na chombo cha habari anachotoka.


"Kwanza, wewe ni nani?" aliuliza Chenge na kujibiwa na mwandishi: "Mimi ni mwandishi wa habari."


"Wa chombo gani?" aliuliza tena.


"Wa gazeti la Mwananchi," alijibu mwandishi.


"Enhee, unasemaje?" alimuuliza tena.


Mwandishi alimweleza kuwa anataka aeleze kama ameshatekeleza azma yake aliyoitangaza alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, kwamba atawasiliana na mwanasheria wake ili avichukulie hatua za kisheria vyombo vya habari alivyodai kuwa vimevuka mipaka katika kuandika na kutangaza tuhuma dhidi yake pamoja na ufafanuzi wa kauli yake ya kuziita Sh1.2 bilioni kuwa ni "vijisenti" anazotuhumiwa kujipatia kwa njia zisizohalali na kuzihifadhi katika kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza.


Akajibu kwa ufupi akisema: "Siongelei chochote," huku akitembea na kushuka kwenye ngazi za hoteli hiyo kwenda mahali lilipoegeshwa gari lake.


Jibu kama hilo, Chenge alilitoa pia kwa waandishi wengine waliomfuata hotelini hapo kumuuliza maswali mbalimbali.


Hali kama hiyo pia iliwakuta waandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) waliotaka kuhojiana naye huku wakimwelekezea vinasa sauti lakini alipunga mkono kuashiria kukataa kuzungumza na kuingia kwenye gari lake.


Baada ya kuingia kwenye gari lake, aliwaambia waandishi wa habari: "Mvua zinatusumbua," kisha akafunga mlango wa gari na kumuaru dereva wake kuondoka.


Tuhuma dhidi ya Chenge za kujilimbikizia fedha hizo, ziliibuliwa na gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza katika toleo lake la Jumamosi wiki iliyopita ambalo lilieleza kuanza kwa uchunguzi dhidi yake, kutokana na akaunti yake kukutwa na zaidi ya dola za Marekani 1 milioni.


Kwa mujibu wa gazeti hilo, Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai nchini humo ya Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa pauni za Uingereza milioni 28, ambazo ni sawa na Sh70 bilioni, mwaka 2002.


Gazeti hilo lilieleza kuwa uchunguzi huo wa SFO unatarajiwa kuanza katika kipindi cha wiki sita zijazo.


Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, moja ya mambo yanayofuatiliwa ni kujua iwapo fedha hizo zinazoaminika kuwa za Chenge, zilizowekwa katika akaunti moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutoka katika Kampuni ya BAE System, inayotuhumiwa kuinyonya Tanzania kwa kuiuzia rada kwa bei kubwa kuliko ilivyotakiwa.


The Guardian katika habari yake hiyo iliyowekwa katika mtandao wa intaneti, liliripoti kuwa taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.


Gazeti hilo lilimkariri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni mali yake, lakini alikanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu.


Siku moja baada ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa taarifa rasmi zikifika serikalini kuhusiana na tuhuma hizo, sheria itachukua mkondo wake na kuonyesha kushangazwa kwake iwapo Chenge alizipata fedha hizo kihalali au la.


Siku moja baadaye, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kumtaka Rais Jakaya Kikwete amsimamishe kazi Waziri Chenge na awekwe chini ya ulinzi, wakati uchunguzi wa kina wa mali zake ndani na nje ya nchi unafanyika.


Alisema anamfahamu vema Waziri Chenge na kwa hiyo, mshahara na marupurupu ya serikali anayolipwa, havimwezeshi kulimbikiza kiasi hicho cha fedha katika akaunti.


Kabla ya gazeti la The Guardian kuibua tuhuma hizo, Septemba 15, mwaka jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, walimtaja Chenge katika orodha ya vigogo kumi na moja, wakiwamo viongozi kadhaa wa serikali nchini wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi wa mabilioni ya shilingi za walipakodi.


Baadaye Septemba 19, Waziri Chenge aliliambia gazeti hili kuwa walioibua hoja ya ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali kama wakipata au kama wana ushahidi, yeye binafsi anatoa ruksa waupeleka katika vyombo husika vya dola ili ufanyiwe kazi.


Hata hivyo, Chenge alithibitisha kwamba yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Tangold, ambayo inamilikiwa na serikali na kwamba hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia kuwa mkurugenzi.


"Nasubiri nipate hizo tuhuma kwa maandishi maana siwezi kuzungumza tu bila kuziona, lakini kama ni ukurugenzi Tangold, mimi siyo kwamba niliwahi kuwa mkurugenzi, ni mmoja wao mpaka sasa. Hii ni kampuni ya serikali, tatizo nini?" alihoji Chenge.


Waziri huyo alisema hapendi malumbano, isipokuwa yote yaliyozungumzwa atahitaji kuyaona kwa maandishi na uonyeshwe ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja na ufisadi uliotajwa.


Februari 12, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitangaza Baraza jipya la Mawaziri baada ya Februari 7, kulivunja baraza la awali ambapo baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliachwa na kumteua Chenge kuendelea na wadhifa wake katika Wizara ya Miundombinu.


Hata hivyo, uteuzi wa Chenge kuendelea na wadhifa aliokuwa nao katika wizara hiyo, ulizua mjadala mkali kutoka kwa wananchi, ambao walidai kuwa hafai kutokana na kuhusika kwake na mikataba mibovu akiwa Mwanansheria Mkuu.


Pia baadhi ya wananchi walisema tangu ashike wadhifa huo mwaka 2005 hakuna mabadiliko katika ujenzi wa barabara zaidi ya mafanikio na ufanisi vilivyoachwa na serikali ya awamu ya tatu, ambayo John Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi.


Pamoja na malalamiko hayo ya wananchi, Chenge aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kujiuzulu kutokana na maneno ya watu na kwamba suala la yeye kuendelea kukaa katika baraza hilo aulizwe Rais Kikwete ambaye ndiye alimteua.

Source: Mwananchi
 
Hao waandishi nao waoga, si wangemkata mtama halafu wapige kelele za mwizi mwizi mwizi,
 
Hao waandishi nao waoga, si wangemkata mtama halafu wapige kelele za mwizi mwizi mwizi,

U make my day mama umenifurahisha sana ila huyu jamaa anakufuru anadai eti "mvua zinatusumbua" Mungu atamwangaza huyu!
 
Mama, you are so so soo funny mama!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ha ha ha
didn't expect to laugh this much this morning.... lol:)
:)
 
Hatimaye sasa ameanza kuwakimbia Waandishi maana Chenge alikuwa aogopi waandishi wa habari hata kidogo zaidi ya yeye kuwatishia. time will tell the truth.
 
Wakati waandishi wanakabiliana na "fisadi" Chenge, nasi wananchi tuonyeshe kutoridhika na ufisadi huo kwa kumzomea popote atakapokuwa - hakika yeye na wenzie wamelitia Taifa doa kubwa ni vyema tuwan'goe mafisadi kama hawa kwa njia yeyote ile.
 
Hao waandishi nao waoga, si wangemkata mtama halafu wapige kelele za mwizi mwizi mwizi.

Bora useme wewe Mama, ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaa.........


chengetqf5.jpg


Huyu ndiye Chenge - Mwizi mkuu hakuiba kuku wala nini bali amesafisha hazina ya Tanzania.

Picture: Credit - Mjengwa Bloghttp://mjengwa.blogspot.com/http://mjengwa.blogspot.com/
 
Wakati waandishi wanakabiliana na "fisadi" Chenge, nasi wananchi tuonyeshe kutoridhika na ufisadi huo kwa kumzomea popote atakapokuwa - hakika yeye na wenzie wamelitia Taifa doa kubwa ni vyema tuwan'goe mafisadi kama hawa kwa njia yeyote ile.

Sidhani kama ataenda jimboni kwake maana naamini jimboni kwake kwenyewe wamemshangaa kuita bilioni moja nukta mbili vijisenti. Lazma watamzomea na mawe watampiga!
 
Sidhani kama ataenda jimboni kwake maana naamini jimboni kwake kwenyewe wamemshangaa kuita bilioni moja nukta mbili vijisenti. Lazma watamzomea na mawe watampiga!

Hiki ndo ninachokipenda maana hawa mafisasi lazima tuanza kuwaalibia kwao, wanapogombea ubunge, raisi akiwateua tutamuuliza kwanini amewateua mafisadi kama tunavyomuuliza sasa kwanini alimteua Chenge kuwa waziri wakati anajua kabisa anachunguzwa kwa ufisadi.
Lazima wananchi wa kawaida waeleze na waelewe jinsi gani amewadharau watanzania kwa kuita pesa ambayo watanzania wengi hawawezi kuipata maishani mwao vijisenti.
 
Yaani pale pale anetokea mtu na petroli, gurudumu na kiberiti watu wakamaliza kazi ninauchungu nao hawa!!! nchi hii ingekuwa na tunguaji nadhani huyu jamaa wala asingechuua round maana tunapigika wengine wanatukejeli.

..uchungu ulionao ni sawa!...nadhani ni vizuri kuwa na uchungu wa kudhibiti kabla uhalifu haujatokea: huo utasaidia zaidi ya kusubiri litokee!
 
Is there any connection between New Habari Corp and Hon. Andrea Chenge?

Mbona hili gazeti lina news tofauti? Ama ndio kazi ya kuhandishi habari? Mwandishi wa Habari kaficha jina as if news anayoiripoti ni nyeti sana. Kama Chenge aliyasema hayo maneno wakati akifunga semina iweje mwandishi afiche jina lake? Maana ni maneno aliyonukuliwa akiyasema mwenyewe kwa kinywa chake! Kwa mwendo huu ndiyo maana baadhi ya magazeti ama waandishi wa habari wanatuhumiwa kupewa mshiko.

Nimejaribu kusoma magazeti mengine yote hayana hii habari isipokuwa hili gazeti la CCM Mafisadi. Kuna haja ya wahariri kuogopa dhambi ya kudanganya ama kutumika kuweka habari mbaya. Basi angalau ingekaa pages za ndani, lakini iko front page na ndiyo inayouza gazeti kwa siku ya leo.

Au kuna Balile mwingine kajotokeza kumsaidia mzee mzima ili ajisafishe mbele ya watanzania????


Chenge aomba radhi


  • [*]Ni kwa kauli yake ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jumatano
    [*]Asema hakuwa na maana mbaya, usukuma wake umemwathiri
    [*]Asisitiza hana nia ya kuvishitaki vyombo vya habari vilivyomwandika

na mwandishi wetu (hili ndiyo linatia mashaka maana sioni umuhimu wa mtu kuficha jina iwapo maneno yalisemwa mbele ya vyombo vingine vya habari)

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge, amewaomba radhi Watanzania kwa kuziita fedha zaidi ya Sh bilioni moja zilizokutwa kwenye akaunti yake nchini Uingereza 'visenti'.

“Sikuwa na maana mbaya, pengine nimeathirika na utamaduni wa Kisukuma, kwetu sisi tumezoea kusema vijisenti, visichana na vitu kama hivyo, nawaomba radhi Watanzania kama wamenielewa vibaya,” alisema Chenge.

Chenge aliomba msamaha huo jana jioni jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga semina ya mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.

Chenge alisema kutokana na kuathiriwa na kabila lake la usukuma, alijikuta akitoa kauli hiyo, akiamini kuwa alikuwa hajakosea na akasema kama kuna Watanzania wameudhika na kauli hiyo, anawaomba radhi.

Chenge pia alisema hana kinyongo na wala hana nia ya kuvishitaki vyombo vya habari vilivyoandika habari hizo kama inayoandikwa na baadhi ya watu.

“Sina ugomvi na vyombo vya habari na wala sina nia ya kuwashitaki watu walioandika habari hizo kwa kuwa naamini walikuwa wakitekeleza majukumu yake,” alisema.

Alikuwa akizungumza hayo kutokana na kauli aliyoitoa Jumatano wiki mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akitokea China alikokuwa ameongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara yake ya siku sita.

Chenge alikaririwa na vyombo vya habari akikiri kuchunguzwa na taasisi moja ya upelelezi ya Uingereza ya Serious Fraud Office (SFO) kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kampuni ya BAE Systems ya Uingereza ili kufanikisha ununuzi wa rada ya serikali mwaka 2002.

Mbali na kugoma kujiuzulu kutoka katika nafasi yake, Chenge pia aligoma kutoa maelezo juu ya namna alivyopata fedha hizo, akisema kwanza anasubiri uchunguzi dhidi yake ukamilike ndipo atatoa maelezo ya namna alivyopata fedha hizo.

Gazeti la The Guardian la Uingereza liliandika Aprili 12, mwaka huu kwamba jumla ya pauni za Kiingereza 507,500, ambazo ni sawa na zaidi ya Sh bilioni moja zilikutwa kwenye akaunti ya benki moja iliyopo katika kisiwa cha Jersey nchini Uingereza.

Gazeti hilo lilisema akaunti hiyo ilikuwa ikichunguzwa ili kupata uhakika wa wapi fedha hizo zilitoka na kwamba iwapo ingegundulika kuwa zilitoka BAE Systems, angechukuliwa kuwa mmoja wa mashahidi dhidi ya maafisa wa kampuni hiyo wanaotuhumiwa kutumia rushwa kushawishi ununuzi wa rada hiyo.

Baada ya habari hizo, viongozi kadhaa wamejitokeza kumtaka ajiuzulu uwaziri ili kupisha uchunguzi huo unaoendeshwa na SFO.

Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliyemtaka Rais Kikwete amwajibishe kwa kumwondoa katika Baraza la Mawaziri.

Source: Mtanzania

NB: Soma kwa makini maana hili gazeti linaeleweka kwa vibweka, nimeiweka hapo ili kujaribu kupata ukweli na kulinganisha na kile kilichoandikwa na gazeti jingine.
 
Hatimaye sasa ameanza kuwakimbia Waandishi maana Chenge alikuwa aogopi waandishi wa habari hata kidogo zaidi ya yeye kuwatishia. time will tell the truth.


Nakwambia mwaka huu hakuna rangi wataacha ona!
 
Hii Link kati ya RA na AC itakuja kujulikana muda si mrefu, tuombe mungu tuwe hai, haiwezekani hata siku moja RA apitishe mkataba wa Richmond ofisi ya zamani ya AC bila yeye kumsaidi.
 
Is there any connection between New Habari Corp and Hon. Andrea Chenge?
Mbona hili gazeti lina news tofauti? Ama ndio kazi ya kuhandishi habari? Mwandishi wa Habari kaficha jina as if news anayoiripoti ni nyeti sana. Kama Chenge aliyasema hayo maneno wakati akifunga semina iweje mwandishi afiche jina lake? Maana ni maneno aliyonukuliwa akiyasema mwenyewe kwa kinywa chake! Kwa mwendo huu ndiyo maana baadhi ya magazeti ama waandishi wa habari wanatuhumiwa kupewa mshiko.

Nimejaribu kusoma magazeti mengine yote hayana hii habari isipokuwa hili gazeti la CCM Mafisadi. Kuna haja ya wahariri kuogopa dhambi ya kudanganya ama kutumika kuweka habari mbaya. Basi angalau ingekaa pages za ndani, lakini iko front page na ndiyo inayouza gazeti kwa siku ya leo.

Au kuna Balile mwingine kajotokeza kumsaidia mzee mzima ili ajisafishe mbele ya watanzania????

Jana nilisema katika yale majina ya watu waliolipwa kutoka account ya Chenge mmoja wapo alikuwa ni mwandishi kutoka Habari Corp anaeitwa Livingston Luhere. Sasa sitaona ajabu kuandikwa habari hiyo wao wapo duania tofauti na sisi. Na kumbuka Habari Corp ni mali ya RA kwahiyo fisadi hawezi kukubali fisadi mwenzie aumbuliwe!
 
Sasa anawaingiza wasukuma kwenye ishu yake? Kwani wachagga wamezoea kusema kula vinyasi?
 
Kwa mara ya kwanza ndiyo nimesikia kwamba Chenge aliwakimbia waandishi wa habari na nina uhakika anaweza kukwepa kwenda Dodoma kwenye vikao vinavyoendelea vya Bunge.

Hii kashfa ni nzito na sidhani kama ana muda mwingi wa kuendelea kuwa Waziri. Kinachoniuma ni kwamba CCM bado watamwacha aendelee kuwa kwenye CC, NEC na kwenye kamati ya maadili ya CCM. Sasa ni maadili gani ambayo Chenge atayasimamia? Akipelekewa tuhuma za ufisadi/rushwa kwenye chama atakuwa na ubavu wa kukemea wakati yeye mwenyewe ni fisadi na inawezekana ni mla rushwa mkubwa?

Watanzania tunachezea ncha ya mkuki na tusipoangalia itatumaliza huku tukidhani ni maskhara.

Watanzania tutanusurika iwapo upinzani utaongezewa nguvu bungeni ama CCM yenyewe ikiamua kujifumua na kujisuka upya kitu ambacho ninakiona ni kigumu maana asilimia kubwa ya walio kwenye ngazi za kufikiriwa kupewa ukubwa wengi wao ni mafisadi na Kamanda wao nae amebaki ni mtu wa kuangalia tu, aidha kwa kuwa walimsaidia kuingia madarakani ama na yeye anahofia kwamba ufisadi wake utaanikwa iwapo akiamua kuwashughulikia kikamilifu mafisadi wote.

Bado tuna safari ndefu na sijui kama tutafika salama .... Mungu Ibariki Tanzania!
 
Jana nilisema katika yale majina ya watu waliolipwa kutoka account ya Chenge mmoja wapo alikuwa ni mwandishi kutoka Habari Corp anaeitwa Livingston Luhere. Sasa sitaona ajabu kuandikwa habari hiyo wao wapo duania tofauti na sisi. Na kumbuka Habari Corp ni mali ya RA kwahiyo fisadi hawezi kukubali fisadi mwenzie aumbuliwe!

Kuna sehemu wakati tunaongelea uhuru wa vyombo vya habari nilisema huu uhuru hautakuwa na maana kama maadili ya uandishi wa habari hayakufuatwa, maana mtu antumia professional yake kutetea maovu kisa apate kitu kidogo.
Wanataaluma wengi wa habari wako concerned na personal interest zaidi ya national interest, na wanaangalia zaidi short term benefit zaidi ya long term benefit, hii inatupeleka pabaya mtu anaandika kitu chauongo ili mradi amfuhishe mtu anayempa pesa alizopata kutoka kwenye ufisadi.
 
Kuna sehemu wakati tunaongelea uhuru wa vyombo vya habari nilisema huu uhuru hautakuwa na maana kama maadili ya uandishi wa habari hayakufuatwa, maana mtu antumia professional yake kutetea maovu kisa apate kitu kidogo.
Wanataaluma wengi wa habari wako concerned na personal interest zaidi ya national interest, na wanaangalia zaidi short term benefit zaidi ya long term benefit, hii inatupeleka pabaya mtu anaandika kitu chauongo ili mradi amfuhishe mtu anayempa pesa alizopata kutoka kwenye ufisadi.


Haitoshi uhuru zaidi ya miaka 40, Kati ya nchi 10 Masikini sana Tanzania ipo. Sasa hata Msumbiji iliokuwa masikini kuliko siye baada ya kuchapana wameanza safari hawapo tena. Waandishi pia wanachangia Tanzania kuwa masikini kuweni kama ulaya maana waandishi wanachangia kufanya utawala uwe bora na wenye viongozi wanaowajibika.

Nafasi Nchi
--------------
1 Malawi
2 Somalia
3 Comoros
4 Solomon Islands
5 DRC
6 Burundi
7 East Timor
8 Tanzania
9 Afghanistan
10 Yemen

Watanzania tunafanya nini na tunakwenda wapi???? Hakuna mzungu wa kutusaidia kujibu hili!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom