Paskali,
Mimi babu yangu Salum Abdallah aliwekwa kizuizini na hakuwa mtu mjinga.
Alikuwa mtu barabara sana.
1947 aliongoza ''general strike,'' dhidi ya wakoloni na akafanya hivyo 1949.
1953 alikuwa akihudhuria mikutano ya siri wakipanga kuundwa kwa TANU na
katika kundi lao wakamleta Germano Pacha Dar es Salaam kuhudhuria mkutano
wa TAA 1954 ulioasisi TANU.
1955 babu yangu akaasisi Tanganyika Railway African Union (TRAU) akiwa rais
muasisi.
1960 akiwa rais wa TRAU aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82.
Hii ilikkuwa haijapatapo kutokea.
Mgomo mrefu Afrika Mashariki ulikuwa ule wa Kenya ulioongozwa na Makhan
Singh.
Babu aliingoza TRAU ikishirikiana na TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hakuwa mtu, ''mjinga mjinga,'' au wa ''mchezo mchezo.''
Alikuwa na dereva wake Msukuma tulimpa jina, ''Msloopagas.''
Hadi leo sijajua jina lake halisi lilikuwa lipi.
Babu yangu aliwekwa kizuizini kwa sababu alitofautiana na Nyerere alipotaka
viongozi wa vyama vya wafanyakazi wavunje vyama vyao pawepo na chama
kimoja nchi nzima chini ya TANU.
Katika watu waliompinga katika mkutano wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi
uliofanyika Moshi alikuwa babu yangu Salum Abdallah.
Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kizuizini mwaka wa 1964 akisingiziwa kuwa
alikuwa mmoja wa watu waliokula njama ya kupindua serikali wakati jeshi lilipoasi
Januari 20, 1964.
Babu yangu hakuwa mjinga wala mtu wa mchezo.