Bilal Waikela ni nani?

Peter maicko

Member
Jul 21, 2012
12
2
Katika ile kesi inayomkabili sheikh ponda ambayo kwa sasa inaendelea kwa kutoa utetezi kwa upande wa washitakiwa,juzi alisimama mzee mmoja aitwae bilal waikela ktk kutoa ushahidi kwa upande wa mshitakiwa.

Mzee huyo mwenye mvi zenyekuonesha kiasi ya chumvi aliyokula alielezea historia fupi juu ya kiwanja cha chang"ombe na bakwata.

Pia alimuelezea mwalimu nyerere juu harakati zake za kuivunja EAST AFRICA MUSLIM SOCIAL WELFARE na kuunda BAKWATAA kama chombo cha Waislamu tz.kwa ufupi ameelezea mengi kuhusu bakwata,serikali na Nyerere.

Nahisi ni bora tukamjua ni nani,anamchango ganiktk kutafuta uhuru na undani ndani wa uwepo wa bakwata na wanachodai waislam juu ya mchango wao ktk uhuru wa nchi wa shutuma zao juu ya serikali zote zilizopita tangu ukolon mpaka uhuru.

Swali la msingi NI NANI BILaL WAIKELA
 
Wanabodi kwa wale mnaojua historia huyu mwanaharakati mkongwe na mpigania uhuru na mwasisi wa TANU ndugu Bilal Waikela naomba mtujuze, nimehamasika kujua hili baada ya kuona post ya ndugu Zitto huko fb akiwa amemtembelea mzee huyo.
 
Mmoja wa Waasisi wa TANU Mikoa ya Magharibi

Don wa Zamani Mpigania uhuru aliekuwa anamiliki Rizki ya kutosha ikiwemo 'Motokari' Miaka ya 1960 enzi hizo kwa Sheria ya Nyerere kumiliki gari lazima Muwe Watu Sita kuombea Kibali cha Umiliki

Mpinga Bakwata wa awali kabisa Tangu inaanzishwa1967 akipinga kwa hoja kuwa inafanywa tawi la TANU/CCM ni Mzaliwa wa Tabora
 
Katika ile kesi inayomkabili sheikh ponda ambayo kwa sasa inaendelea kwa kutoa utetezi kwa upande wa washitakiwa,juzi alisimama mzee mmoja aitwae bilal waikela ktk kutoa ushahidi kwa upande wa mshitakiwa.

Mzee huyo mwenye mvi zenyekuonesha kiasi ya chumvi aliyokula alielezea historia fupi juu ya kiwanja cha chang"ombe na bakwata.

Pia alimuelezea mwalimu nyerere juu harakati zake za kuivunja EAST AFRICA MUSLIM SOCIAL WELFARE na kuunda BAKWATAA kama chombo cha Waislamu tz.kwa ufupi ameelezea mengi kuhusu bakwata,serikali na Nyerere.

Nahisi ni bora tukamjua ni nani,anamchango ganiktk kutafuta uhuru na undani ndani wa uwepo wa bakwata na wanachodai waislam juu ya mchango wao ktk uhuru wa nchi wa shutuma zao juu ya serikali zote zilizopita tangu ukolon mpaka uhuru.

Swali la msingi NI NANI BILaL WAIKELA

Ndugu zangu,
Mimi ninaweza kusema kuwa namjua Mzee Waikela.

Mzee Waikela kabla sijakutananae uso kwa macho 1987 nyumbani kwake
Gongoni Tabora, nilisoma nyaraza zake zilizohusu kile lichokuja kujulikana
kama, ''Mgogoro wa East African Muslim Welfare Society, (EAMWS),'' wa
mwaka wa 1968.

Nyaraka hizi Mzee Waikela alizikabidhi kwa Muslim Student Association of
University of Dar es Salaam (MSAUD) nami nilizikuta katika hapo maktaba ndipo
nikapata nafasi ya kuzisoma.

Hizi nyaraka zilikuwa ni barua za EAMWS na ''cutting,'' za magazeti ya kipindi
kile kile kilichoitwa cha ''mgogoro.''

Hizi nyaraka nilielezwa kuwa Mzee Waikela alizileta pale MSAUD kwa lengo la
kwanza zihifadhike na pia zitumike katika kuandika historia ya kweli ya Waislam
wa Tanzania na matatizo waliyokumbananayo baada ya uhuru mwaka wa 1961.

Mwaka wa 1987 nilisafiri hadi Tabora kwenda kumuona na kufanyanae majadiliano
kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika yeye akiwa mmoja wa waasisi wa TANU.
 
Ndugu zangu,
Mimi ninaweza kusema kuwa namjua Mzee Waikela.

Mzee Waikela kabla sijakutananae uso kwa macho 1987 nyumbani kwake
Gongoni Tabora, nilisoma nyaraza zake zilizohusu kile lichokuja kujulikana
kama, ''Mgogoro wa East African Muslim Welfare Society, (EAMWS),'' wa
mwaka wa 1968.

Nyaraka hizi Mzee Waikela alizikabidhi kwa Muslim Student Association of
Dar es University (MSAUD) nami nilizikuta katika hapo maktaba ndipo
nikapata nafasi ya kuzisoma.

Hizi nyaraka zilikuwa ni barua za EAMWS na ''cutting,'' za magazeti ya kipindi
kile cha kile kilichoitwa mgogoro.

Hizi nyaraka nilielezwa kuwa Mzee Waikela alizileta pale MSAUD kwa lengo la
kwanza zihifadhike na pia zitumike katika kuandika historia ya kweli ya Waislam
wa Tanzania na matatizo waliyokumbananayo baada ya uhuru mwaka wa 1961.

Mwaka wa 1987 nilisafiri hadi Tabora kwenda kumuona na kufanyane majadiliano

Nikushukuru sana mzee SAID kwa historia hiyo mujarabu kabisa na sisi vijna tupate jifunza ingawa umeweka kifupi sana
 
Ndugu zangu,
Mimi ninaweza kusema kuwa namjua Mzee Waikela.

Mzee Waikela kabla sijakutananae uso kwa macho 1987 nyumbani kwake
Gongoni Tabora, nilisoma nyaraza zake zilizohusu kile lichokuja kujulikana
kama, ''Mgogoro wa East African Muslim Welfare Society, (EAMWS),'' wa
mwaka wa 1968.

Nyaraka hizi Mzee Waikela alizikabidhi kwa Muslim Student Association of
Dar es University (MSAUD) nami nilizikuta katika hapo maktaba ndipo
nikapata nafasi ya kuzisoma.

Hizi nyaraka zilikuwa ni barua za EAMWS na ''cutting,'' za magazeti ya kipindi
kile cha kile kilichoitwa mgogoro.

Hizi nyaraka nilielezwa kuwa Mzee Waikela alizileta pale MSAUD kwa lengo la
kwanza zihifadhike na pia zitumike katika kuandika historia ya kweli ya Waislam
wa Tanzania na matatizo waliyokumbananayo baada ya uhuru mwaka wa 1961.

Mwaka wa 1987 nilisafiri hadi Tabora kwenda kumuona na kufanyane majadiliano
kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika yeye akiwa mmoja wa waasisi wa TANU.
Tunakusubiria kwa hamu.
P.
 
Tunakusubiria kwa hamu.
P.
Pascal,
Ni vigumu kueleza historia ya Mzee Waikela katika mahali kama hapa JF
kwa ajili ya nafasi.

Kwani historia yake inaanza 1955 wakati wa kuunda TANU Tabora hadi
kufika kupatikana kwa uhuru mwaka wa 1961 yeye akiwa mshiriki mkuu
katika historia yenyewe ya kwanza kuundaTANU na kushiriki katika matukio
makubwa ya wakati ule kama Kura Tatu ya 1958 yeye akiwa kijana.

Mzee Waikela wakati ule alikuwa pia ni kiongozi wa EAMWS akiwa katibu
wa Western Province na mfuasi wa Mufti wa Tanganyika, Sheikh Hassan
bin Amir.

Nilipokwenda kuonana na Mzee Waikela, hakuwa peke yake aliwaita wazalendo
wenzake, Abdallah Kassongo, Mohamed Mangiringiri na Ramadhani
Singo.

Sijapatapo kukutana wana TANU waliokuwa wanaijua historia ya chama chao na
wakaieleza kwa utulivu na ufasaha kama watu hawa.

Baada ya hahojiano haya Mzee Waikela akanita pembeni mimi na walionisindikiza
kwake, marehemu Sheikh Ilunga Hassan Kapungu na shemeji yake Salum
Mkangwa
.

Mzee Waikela alituambia turejee kesho atueleze yale yaliyotokea baada ya uhuru
kupatikana mwaka wa 1961.

Nilirejea na wenyeji wangu siku ya pili na Mzee Waikela alifunguka.
Alizungumza kwa takriban saa tatu sote tukiwa kimya tukimsikiliza.

''Mohamed mimi niliwekwa kizuizini jela ya Uyui mwaka wa 1964 na babu yako, Mkuu
wa Jela akiwa Bwana Munthali na Regional Commissioner akiwa Rashid Kheri
Bagdelleh,
ilikuwa mwezi wa Ramadhani na walinifuata usiku kunikamata na ndiyo
kwanza nilikuwa naanza kula daku....''

Mazungumzo yale na Mzee Waikela ndiyo yaliyotengeneza sehemu ya tatu katika
kitabu cha Abdul Sykes na sehemu hiyo nikaipa jina, ''Njama Dhidi ya Uislam (1961 -
1970).

Tulipomaliza mahojiano nilimwambia Mzee Waikela, ''Mzee Waikela umenieleza habari
nzito sana na za kutisha mimi nataka unifahamishe ikiwa unanipa ruhusa ya kukutaja
wewe kwa jina kuwa hizi taarifa chanzo chake ni wewe.''

''Nitaje bila hofu waeleze kuwa hizi habari nimekupa mimi Bilal Rehani Waikela.''

Tulipokuwa tunaagana, Mzee Waikela alinyanyua mikono juu akaniombea dua ndefu
sana na akaniambia, ''Mohamed kitabu kitoke Waislam waujue ukweli wa historia yao
kisiishie katika makaratasi.''
 
Pascal,
Ni vigumu kueleza historia ya Mzee Waikela katika mahali kama hapa JF
kwa ajili ya nafasi.

Kwani historia yake inaanza 1955 wakati wa kuunda TANU Tabora hadi
kufika kupatikana kwa uhuru mwaka wa 1961 yeye akiwa mshiriki mkuu
katika historia yenyewe ya kwanza kuundaTANU na kushiriki katika matukio
makubwa ya wakati ule kama Kura Tatu ya 1958 yeye akiwa kijana.

Mzee Waikela wakati ule alikuwa pia ni kiongozi wa EAMWS akiwa katibu
wa Western Province na mfuasi wa Mufti wa Tanganyika, Sheikh Hassan
bin Amir.

Nilipokwenda kuonana na Mzee Waikela, hakuwa peke yake aliwaita wazalendo
wenzake, Abdallah Kassongo, Mohamed Mangiringiri na Ramadhani
Singo.

Sijapatapo kukutana wana TANU waliokuwa wanijua historia ya chama chao na
wakaieleza kwa utulivu na ufasaha kama watu hawa.

Baada ya hahojiano haya Mzee Waikela akanita pembeni mimi na walionisindikiza
kwake, marehemu Sheikh Ilunga Hassan Kapungu na shemeji yake Salum
Mkangwa
.

Mzee Waikela alituambia turejee kesho atueleze yale yaliyotokea baada ya uhuru
kuatikana mwaka wa 1961.

Nilirejea na wenyeji wangu siku ya pili na Mzee Waikela alifunguka.
Alizungumza kwa takriban saa tatu sote tukiwa kimya tukimsikiliza.

''Mohamed mimi niliwekwa kizuizini jela ya Uyui mwaka wa 1964 na babu yako, Mkuu
wa Jela akiwa Bwana Munthali na Regional Commissioner akiwa Rashid Kheri
Bagdelleh,
ilikuwa mwezi wa Ramadhani na walinifuata usiku kunikamata na ndiyo
kwanza nilikuwa naanza kula daku....''

Mazungumzo yale na Mzee Waikela ndiyo yaliyotengeneza sehemu ya tatu katika
kitabu cha Abdul Sykes na sehemu hiyo nikaipa jina, ''Njama Dhidi ya Uislam (1961 -
1970).

Tulipomaliza mahojiano nilimwambia Mzee Waikela, ''Mzee Waikela umenieleza habari
nzito sana na za kutisha mimi nataka unifahamishe ikiwa unanipa ruhusa ya kukutaja
wewe kwa jina kuwa hizi taarifa chanzo chake ni wewe.''

''Nitaje bila hofu waeleze kuwa hizi habari nimekupa mimi Bilal Rehani Waikela.''

Tulipokuwa tunaagana, Mzee Waikela alinyanyua mikono juu akaniombea dua ndefu
sana na akaniambia, ''Mohamed kitabu kitoke Waislam waujue ukweli wa historia yao
kisiishie katika makaratasi.''

Jamani hii mambo ya Waislamu wakati hata Watanzania tu bado haijakaa sawa hivyo kweli tunajitakia heri au shari hapa...? Watu wenyewe sisi mpaka sasa hata maji ya safi hatujaweza kujikimu leo mnataka kuchimba sana haya mambo ya Waislamu au Wakristo kwenye hivi vinchi vyetu uchwara hivyo msidhani hakuna Tai huko juu wanasubiri mianya kama hii kuturudisha kwenye adha ya kutawaliwa au hatuamini kwamba historia hujirudia..? Wacheni mchezo nyie watu weusi mnatatizo gani..? Hamkomi tu..?!! Mmetumikishwa, mmenyanyaswa kupindukia na bado mnanyanyaswa na kudhalaurika lakini eti bado tunataka kuchimba chimba nyufa ili hata kidogo tulichojenga kiwe dhaifu Zaidi. Mwalimu marehemu Ali Mazrui aliwahi andika kuwa Waafrika weusi sio race iliyoteswa kuliko zote duniani maana kuna wengine kama Ma Aborigines na Wahindi wekundu wa bara la Marekani wao waliteswa Zaidi yetu, lakini Mwafrika mweusi ndie pekee Duniani aliedharirishwa kupita mfano!!!! Hebu tuchukue hii iwe dira katika kila tulifanyalo au kulifikiria tujiulize linatusaidiaje kujenga umoja wetu ili utusaidie kutokana na adha hii kama sio leo basi hata vizazi vijavyo. Tufike mahali tuseme imetosha. Hii oh mchango wa Waislamu oh mchango wa Wakristo upuuzi mtupu maana hizo dini zote hazikusaidia ilipofika sisi kuvishwa minyororo na mijeredi nyuma kuelekea utumwani. Wacheni upuuzi hapa.
 
Kokola,
Hapana haja ya kutukana.

Hapana "upuuzi," hii ni historia ya uhuru wa Tanganyika ipo kwenye
kitabu cha Abdul Sykes na toka kichwapwe sasa ni miaka 20 kipo
madukani kinasomwa na sasa kinakwenda toleo la nne.

Hapajakuwa na tatizo lolote.

Mtu kamuuliza Rehani Waikela ni nani hata Zitto Kabwe afike
nyumbani kwake kumsalimia?

Mimi nimemweleza Waikela kadri ninavyomjua.

Huu si ''upuuzi,'' bali ni historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa
nchi yetu bega kwa bega pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere
.

Ni bahati mbaya tu historia hii haikuthaminiwa ndiyo maana leo Waikela
hajulikani na anapata umaarufu baada ya kutembelewa na mwanasiasi
kijana aliye mashuhuri - Zitto Kabwe.
 
hajulikani na anapta ummarufu baada ya kutembelewa na mwanasiasi
kijana aliye mashuhuri.
Najua ni taabu sana kueleza uhuru wa Tanganyika na waliopigania uhuru huu bila kuwataja waasisi wa harakati na maisha yao kwaa ujumla, nakushukuru sana mzee wangu lkn naona kila wakati unapleta ufafanuz kuhusu historia ya nchi hii suala la dini hasa uislam lazima uingie, embu siku ukipta nafasi labda kama na historia pia inauunganisha ukristo na uhuru utueleze kidogo mchango wake ktka uhuru wa TANGANYIKA
 
Kokola,
Hapana haja ya kutukana.

Hapana "upuuzi," hii ni historia ya uhuru wa Tanganyika ipo kwenye
kitabu cha Abdul Sykes na toka kichwapwe sasa ni miaka 20 kipo
madukani kinasomwa na sasa kinakwenda toleo la nne.

Hapajakuwa na tatizo lolote.

Mtu kamuuliza Rehani Waikela ni nani hata Zitto Kabwe afike
nyumbani kwake kumsalimia?

Mimi nimemweleza Waikela kadri ninavyomjua.

Huu si ''upuuzi,'' bali ni historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa
nchi yetu bega kwa bega pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere
.

Ni bahati mbaya tu historia hii haikuthaminiwa ndiyo maana leo Waikela
hajulikani na anapata umaarufu baada ya kutembelewa na mwanasiasi
kijana aliye mashuhuri - Zitto Kabwe.
LKN PIA NATAMANI SANA SIKU NIKIJA DAR NIPATE HATA WASAA NIKUSALIM, NAJUA UNA MENGI SANA YA KUTUFUNZA VIJANA KAMA MIMI HASA LINAPOKUJA SUALA LA HISTORIA YA NCHI YETU
 
Najua ni taabu sana kueleza uhuru wa Tanganyika na waliopigania uhuru huu bila kuwataja waasisi wa harakati na maisha yao kwaa ujumla, nakushukuru sana mzee wangu lkn naona kila wakati unapleta ufafanuz kuhusu historia ya nchi hii suala la dini hasa uislam lazima uingie, embu siku ukipta nafasi labda kama na historia pia inauunganisha ukristo na uhuru utueleze kidogo mchango wake ktka uhuru wa TANGANYIKA
Experience Kleist Sykes katika mswada alioandika kabla ya kufariki mwaka wa 1949 anaeleza kuwa wengi waliokuwa viongozi waasisi wa African Association ni Waislamu kwa kuwa Kanisa likiwakataza waumini wao kujihusisha na siasa. Unaweza kusoma habari hizi katika kitabu kilichohaririwa na John Iliffe (1973).

TANU ilipoasisiwa 1954 Kanisa Jimbo la Kusini likiwakataza waumini wake wasijiunge na TANU wakisema kuwa Waislam wanataka kuleta Vita ya Maji Maji kama walivyofanya 1907 dhidi ya Wajerumani.

Mwaka 1955 ukatumwa ujumbe uje TANU HQ ionane na uongozi wa juu wa TANU ili Nyerere aende Lindi akaeleze ukweli.

Waliokuja Dar es Salaam alikuwa Ali Mnjale na Salum Mpunga.

Nyerere alikwenda Lindi akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani.

Sina uwezo mimi wa kubadili historia hii.
 
shukrani jazzzakalahu kheir maali, niliuliza swali hili kusaidia wengine pia wapate elewa mchango wa uislam ktk uhuru. Mie nshashibisshwa muda sana nawe na ;ia na makongamano ya al marhum Sheikh HASSAN ILUNGA KAPUNGU
 
Hakuna Mungu huyu tuliyeletewa kwenye vitabu. Hayupo. Katungwa na watu tu.

Habari za Uislamu na Ukristo ni tamaduni za watu wa nje tumepandikiziwa tu sisi Waafrika na sasa zinataka kutumaliza.

Tamaduni za uongo wa kijinga sana unaokuambia Wayahudi ni taifa teule la Mungu. Hivyo wewe Mzaramo huna maana kwa Mungu kulinganisha na Myahudi.

Ujinga sana.

Tamaduni zinazokuambia ukisali angalia Maka. Kama vile Mungu anakaa Maka. Kama vile kwenu Africa si muhimu Maka ndiko muhimu.

Ni njia ya kuku control kisaikolojia ufikiri Muafrika hana maana. Mwenye maana Muarabu na Myahudi.

Ujinga mkubwa sana.

Ukitaka kujua hilo angalia Quran na Biblia vitabu vyote hivi vimejaa logical contradictions kiasi kwamba haiyumkiniki kwamba ni vitabu vya Mungu.

Ukielewa hili, haya mengine ni mambo ya siasa za watu tu zinazotaka kujipaza juu kwa kutumia madhabahu ya dini za uongo na Mungu ambaye hayupo.

Waafrika weusi wanajifanya wanaujua Uislamu na Ukristo kupita Waarabu na Wayahudi.

Lakini historia za Waafrika na tamaduni zao wengi hata kuzijua hawazijui.

Aibu kubwa.
 
Pascal,
Ni vigumu kueleza historia ya Mzee Waikela katika mahali kama hapa JF
kwa ajili ya nafasi.

''Mohamed mimi niliwekwa kizuizini jela ya Uyui mwaka wa 1964 na babu yako, Mkuu
wa Jela akiwa Bwana Munthali na Regional Commissioner akiwa Rashid Kheri
Bagdelleh,
ilikuwa mwezi wa Ramadhani na walinifuata usiku kunikamata na ndiyo
kwanza nilikuwa naanza kula daku.....''
Mkuu Maalim, Mohamed Said, kuna vitu unaeleza vinaumiza moyo na fikra na kuacha maswali bila majibu!.

Nimetokea kusoma darasa moja na mtoto wa Rashid Kheri Baghdelleh, naye akiitwa Rashidi, pia tulikuwa darasa moja na mtoto wa Robert Makange akiitwa Moses, tukiwa shule ndipo niliposoma kitabu sikumbuki jina la mwandishi, ila kilizungumzia harakati za uhuru na kueleza jinsi Makange na Baghdelleh walivyofungwa jela moja wakati wa kupigania uhuru, haiwezekani Baghdelleh huyu huyu aliyeonja mateso ya jela enzi ya mkoloni, halafu aje kumtia jela mpigania uhuru mwenzake, Mzee Waikela!. Hapa unapata maswali mengi kuliko majibu.

Pale Magomeni Mikumi kwa kina Rashidi ni jirani kidogo na nyumbani kwa Saadani Abdul Kandoro ambako nako nilifikikwa urafiki na mwanae Bilal, kiukweli ni bahati mbaya mimi uandishi wangu ni kupitia utangazaji wa TV, lakini ningeshika kalamu na kuandika kwa kuhoji, labda nami kuna ambayo ningechangia!, maadam saa hizi, nami jioni inaanza kuniotea, ngoja nijitathmini, naweza kufanya mahojiano na kina nani waliopo, niweze kuhifadhi kwenye audio visual, watoto wetu na watoto wa watoto wetu, waje kusikiliza. Nikifikia aumuzi wa kuhifadhi, nitakutafuta kwa msaada wa kunielekeza hawa waasisi wa TANU, ni wangapi wangalipo hai, ili angalau hiki kidogo kilichobaki kihifadhiwe kabla hakijapotea chote!.

Asante.

Paskali
 
Paskali rudia kunisoma ili uelewe nilichoandika. Hakuna mahali niliposema Rashid Kheri Bagdelleh alimtia kizuizini Bilal Waikela. Waikela pamoja na babu yangu na Sheikh Jumanne Bias waliwekwa kizuizini chini ya Dentation Act ya 1962. Nikuongeze kitu. Bagdelleh alikuwa rafiki ya baba yangu na akija nyumbani kwetu.
 
Asalaam aleikum maalim.
Nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa makala na maandiko yako mengine.Hongera sana kwa kuutangaza na kuutetea umma was kiislamu ingawa historia "ya pili" imekuwa ni kikwazo katika hili.
Naamini Allah (s.w) ataendelea kukuongoza udumu katika kheri.Inshaallah.
Pamoja na hayo, natamani kupata nakala(hata soft copy) za maandiko yako.
 
Kokola,
Hapana haja ya kutukana.

Hapana "upuuzi," hii ni historia ya uhuru wa Tanganyika ipo kwenye
kitabu cha Abdul Sykes na toka kichwapwe sasa ni miaka 20 kipo
madukani kinasomwa na sasa kinakwenda toleo la nne.

Hapajakuwa na tatizo lolote.

Mtu kamuuliza Rehani Waikela ni nani hata Zitto Kabwe afike
nyumbani kwake kumsalimia?

Mimi nimemweleza Waikela kadri ninavyomjua.

Huu si ''upuuzi,'' bali ni historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa
nchi yetu bega kwa bega pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere
.

Ni bahati mbaya tu historia hii haikuthaminiwa ndiyo maana leo Waikela
hajulikani na anapata umaarufu baada ya kutembelewa na mwanasiasi
kijana aliye mashuhuri - Zitto Kabwe.

Bwana Mohamed Said "upuuzi" hapa halikuwa tusi ni kinyume cha hoja yenye mantiki ile isiyo na maana ndio upuuzi sio tusi kamwe!! We ndugu yangu nilichosema mimi sio kuwa hatupendi au hatuwaenzi wapigania uhuru wetu la hasha!! Tena ifike mahali wapewe hadhi ya manabii wetu lakini katika context ya Utaifa na sio udini au ukabila Kaka!! Waikela kama yeye ni shujaa wa kumtoa mkoloni kwangu na naamini kwa Watanzania wengi ni mtu muhimu sana bila kujali dini yake au kabila lake. Hapo pia, haitegemei kutembelewa kwake na "mwanasiasa kijana aliye mashuhuri - Zitto Kabwe". Historia yetu imeandikwa na wageni sisi ndio sasa tunaamka kama anavyotaka kuamka rafiki yangu Paskali. Kama hao mashujaa hawakuthaminiwa au hawakutanjwa kwenye historia basi isiwe kuwa tuone ni kwa ajili ya dini zao bali tu kwa ajili ya kile walichokuwa wanakipigania ambacho mgeni alieandika historia hakukipenda. Wewe kama kijana wa sasa rekebisha ukisisitiza Utaifa na sio udini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom