Bila Nyerere Mkapa asingekuwa Rais, na bila Mkapa Magufuli asingekuwa Rais, hivyo bila Nyerere, Magufuli asingekuwa Rais

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Wana JF, ningependa kuwapa historia kidogo. juu ya tulikotoka

Baada ya awamu ya Raisi Mwinyi kuelekea uchaguzi Mkuu kulikuwa joto kubwa na upendezi kuelekea NCCR Mageuzi ambayo mgombea wao wa urais alikuwa ni Lyatonga Mrema. Mrema alifikia umaarufu wa kulinganishwa na Sokoine kwa kupendwa na wananchi, na alionekana kiongozi namba moja wa kutatua matatizo ya wananchi mara moja, kama Sokoine. Umaarufu wa Mrema akiwa ndani ya CCM ulifanya apewe cheo cha Naibu Waziri Mkuu ambacho hakikuwapo kikatiba.

Msimamo mkubwa wa Mrema katika kupambana na ufisadi ulisababisha agongane na uongozi wa Rais Mwinyi wakati huo, ambaye alionekana kuegemea sana na kuwapendelea wafanyabiashara wenye asili ya kiasia na wengi wao wakionekana kuwa na uhusiano wa kibiashara na mke wa rais. Ikulu ikaonekana ni sehemu ya kufanyia biashara. Kuna wakati hata wahujumu uchumi wenye connection na waasia hawa walipofungwa walipewa msamaha wa raisi "kwa sababu za kifamilia", jambo lilolomuudhi sana Mrema. Wahujumu hawa walimwona Mrema kuwa kikwazo na ikabidi mamlaka yake yapunguzwe katika kumdhibiti, na hatimaye kumfanya ajitoe CCM na kujiunga na NCCR Magaeuzi.

Ilionekana njia ya Mrema kuwa rais ilikuwa wazi. Mrema alipendwa hadi watu walikuwa tayari kusukuma gari lake ili lisitumie mafuta. Kuna wakati fulani hadi wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliamua kusukuma gari la Mrema! Polisi walipojaribu kuwapiga watu mabomu ili wasisiukume gari la Mrema Nyerere aliingilia akawazuia Polisi kufanya hivyo!

Njia ya Mrema kuwa rais wa Kwanza Tanzania kutoka chama cha upinzani iliwekwa wazi zaidi pale ambapo Nyerere alizuia uteuzi wa Kikwete kuwa mgombea wa CCM na kumchagua Mkapa. Hii iliwaudhi watu wengi ambao walimpenda sana Kikwete hasa kutokana na mwonekano wake wa kuvutia. Nyerere alisema wazi wanaompenda Kikwete kutokana na kuvutia kwake wapeleke posa, kwa kuwa Tanzania ilihitaji raisi makini sio mzuri!

Nyerere akijua kuwa Mkapa asingefua dafu katika uchaguzi dhidi ya Mrema, aliamua kujitwika jukumu la kumpigia kampeni Mkapa. Alifanya kazi kubwa ambayo ilizaa matunda, na Mkapa akawa raisi, japo kulikuwa na madai kwamba kuna mchezo ilibidi ufanyike ili kufanya Mkapa awe raisi!

Kitu cha kushangaza ni kwamba Mkapa alipotwaa urais alibadilika sana dhidi ya Nyerere. Akawa hamsikilizi tena. Mkapa alianzisha kampeni ya kubinafsisha mashirika ya umma, jambo ambalo Nyerere alilipinga kabisa. Kwa mfano, kitendo cha kubinafsisha iliyokuwa National Bank of Commerce (NBC) kilimuuma sana , kama sio kumuudhi sana Nyerere, kwa kuwa NBC ilijiendesha kwa ufanisi na faida kubwa . Kulikuwa na tetesi za mkono kulambwa katika ubinafsishaji wa NBC, na hata ikafikia Nyerere kumwambia Mkapa inawezekana ikafikia ukabinafshisha hata magereza!

Mkapa kutomsikiliza tena Nyerere iliharibu sana uhusiano wao kiasi kwamba inasemekana Nyerere alipoanza kuumwa Mkapa hakujihusisha nae wala kumjulia hali! Ilifika mahali watu binafsi ndio waliojitolea kumsaidia Nyerere, msaada ambao Nyerere aliukataa akidai kwamba serikali ndio ilipaswa kumtibu. Hatimae Mkapa akajitokeza, labda akiwa ameambiwa Nyerere asingepona! Suala hili hata lilizaa minong'ono kwamba ugonjwa na kifo cha Nyerere vilikuwa na utata!

Baada ya Mkapa kuwa raisi aliamua kumuingiza Magufuli katika Baraza lake la mawaziri. Hadi leo kuna maswali mengi sana juu ya sababu ya upendezi wa juu wa Mkapa kwa Magufuli. Kuna maneno mengi yanasemwa juu ya sababu iliyomfanya Mkapa ambebe sana Magufuli, kutia ndani kwenda yeye binafsi kumfanyia kampeni ya ubunge. Na ni wazi bila Mkapa kumfanyia kampeni ya Ubunge Magufuli basi Magufuli asingepita ubunge kwa kuwa alishajaribu huko nyuma akashindwa!

Baada ya Magufuli kushinda ubunge, mara moja Mkapa alimteua kama Naibu Waziri kumwandaa kuwa waziri kamili. Baada ya muda si mrefu akamteua kuwa waziri kamili. Watu wanauliza je, Mkapa aihusika moja kwa moja Magufuli kuwa rais? Hatuna jibu la moja kwa moja. Lakini jambo moja lililo wazi sana ni kwamba, bila Nyerere Mkapa asingekuwa raisi, na bila Mkapa Magaufuli asingekuwa raisi na hivyo bila Nyerere Magufuli asingekuwa raisi!
 
Anataka kusema kwamba eti Magufuri ni Nyerere anayeishi.
Aaah, usinilishe maneno! Ila la msingi ni kwamba kuna jambo nawaambia, ila sio lazima nikutafunie kila kitu. Fumbo hufumbiwa mjinga!
 
Back
Top Bottom