Naomba nisijisifu kuwa na akili, wakati nasoma nilipania sana kuwa lawyer, hivyo nikiwa form III Tambaza nilichagua arts, home waligomea, hivyo nikasoma science na kusoma arts as an option, jamaa wanaopuliza ile 'kitu' wote walitoka na DIV 1 kali za pts 7, Mimi nilapatan I ya pts 17!. Hivyo nilipoenda Ilboru na mimi nikaamua kuanza kupuliza ili nitoke na pts 3!. Very unfortunately mimi ikanituma vibaya!. Ile baridi ya Ilboru, vile vibinti vyeupe vya Kiarusha ambavyo havijui kusema hapana, nikajikuta nimechanganyikiwa kwa mengine na sio masomo, matokeo ya form 6, nikakosa I and forget kuhusu sheria!. Amini usiamini nili opt kusoma Journalism by choice. Baada ya kuhudumu media for 10 years, nilitinga UDSM kufanya LL.B, nika graduate with honors, hivyo hiyo ni proof kichwani niko vizuri ila tuu ni dhaifu kwa yale mambo yetu yale!.
Kwanza ni kweli mwanzo wa uhusiano ni academic related ya kijakazi kumsaidia academically. Ka binti kalisoma girls school only hivyo kamakuja chuo kakiwa bado!. Hivyo mimi kwake ndio nilikuwa kila kitu!. Kalipenda kakafa kakaoza, na ndio maana kalifanya kila kitu hadi kugharimia harusi ya kifahari, honeymoon London etc, it was true love!.
Kwanza nikurekebishe, hakuniacha!, baada ya London, familia yake ikamlipia shule 4 years in US, hivyo mimi kutakiwa kuwa babysitter na house husband, wife ndio bread winner. Kuna makabila wanaweza hiyo hali, sisi Wasukuma, kiukweli hatuwezi, hivyo ni mimi ndio niliamua kuondoka kurudi bongo!. Na kufika huku, mimi bado kijana, damu inachemka, ni Mtangazaji maarufu wa kipindi Kiti Moto, pesa ipo, usafiri upo, nyumba ipo, mke yuko masomoni kwa miaka 4!, hata ungekuwa wewe!. Tatizo jingine baya sana kwa Wasukuma ni hatuna siri na hatufanyi mambo yetu kwa siri!.
Hivyo nilipokwenda kumtembelea after 2 years nikakuta taarifa zangu zote anazo, wabongo kwa kufuatilia maisha binafsi ya watu hawajambo!. Hivyo nikanyimwa chakula mpaka nipime!. Tulisolve issue ikaisha, nikarudi Bongo.
Alipomaliza shule nikamfuata wife turudi Bongo, akanigomea kuwa ameisha amua our life is in US, mimi nikubali kuwa house husband!. Niligoma na mimi ndio nikarudi zangu Bongo, hivyo sikuachwa mimi ndio niliacha!, ila ukiwa masikini jeuri umeoa mke tajiri, anaishi top life US, hata ukisema ni wewe ndio ameacha, utaonekana umeachwa!. We are still very good friends.
Na mimi huku kwa upande wangu kiukweli kabisa am just a human being, I'm neither a saint nor an angel!.
P