Bila maamuzi magumu kutoboa kupitia kuajiriwa nitakusikia tu kwenye bomba Ajira za afya michosho tu sifa mtaani tu ila hela hamna

Bila maamuzi magumu kutoboa kupitia kuajiriwa nitakusikia tu kwenye bomba Ajira za afya michosho tu sifa mtaani tu ila hela hamna

Ni umasikini mkuu tu kweli wewe ulipwe 450k kwa maisha ya Dar es salaam una familia unapanga unaishi je, kama sio umasikini wengine tungekua na wazazi wenye uwezo bora urudishe majeshi kwa wazazi yuishi kama hao waarabu koko wa kariakoo baba mama shangazi watoto mke wote sehemu moja
450k kwa dar ni ndogo apo ni hela ya Kodi na msosi.
 
Njaa kali sana hao ndiyo maana wamegueka majambazi waliovaa sare za polisi.....Usijichanganye uingie kwenye 18 zao ni bora ukutane na majambazi wenyewe kuliko hao.
Wanakumaliza na hela wanachukua wanasema ulikuwa jambazi
 
Ukitaka ufurahie ajira ya serikali, uwe na hela ya ziada, mfano hela ya Chai, nyumba, nauli, extra duty, per dierm, nk taasisi hizi huwezi kusikia watu wanalia njaa, Tanesco,Gepsa , TRC, EWURA, TPDC, na zipo taasisi nyingi ambazo watumishi wake wanaishi maisha mazuri Balaa! Hata Askari siku hizi Wana maslahi mazuri sana! Mshahara Peke yake kwa kweli maisha ni magumu!
Tatizo sasa hawa dhulma ni nyingi sana kwa jamii wanayoihudumia.

Nalo ni tatizo jengine.
 
Anzisha Biashara ukiwa humo humo kwenye ajira hadi hiyo biashara ianze kukupa return mara 5 au zaidi ya unachopata kwenye ajira usithubutu kuacha kazi akakimbilia kujiajiri.
Kujiajiri hakutaki watu legelege utaishia kuongea mwenyewe barabarani.
Hata ukiona mtu anachoma mahindi barabarani ujue yupo smart masna siikila mtu anaweza kufanya hivyo
 
Pesa ipo kwenye kujiajiri Tu asikudanganye mtu , kama umeajiriwa ni Bora uweke interval ya kukusanya mtaji let say miaka miwili au mitatu then Acha kazi nenda kajiajiri, angalizo ni kwamba usije ukakimbilia kujiajiri Tu kisa umeona mtu au Kwa tamaa Tu ya kutaka pesa haraka haraka bila kujipanga.

Kumbuka kwenye kujiajiri itachukua muda zaidi kujipata pengine zaidi ya ulivyotarajia lakini ukikomaa unatoboa ukiwa kijana mdogo kabisa Hadi unajilaumu kuwa siku zote ulikuwa wapi, pia kumbuka zaidi ya asilimia tisini ya waliojiajiri biashara zao hufa Kati ya mwaka mmoja Hadi mitatu, unapochukua maamuzi ya kujiajiri Ingia jumla jumla Kwa miguu yote kinyume na hapo hutoboi may be Kwa kazi zisizohitaji uwepo wako sana tena may be.

Asilimia kubwa au tuseme 97% ya waajiriwa TZ watakufa maskini, mishahara inayolipwa ni kama ya vibarua, ni watu wachache Sana wanaokula maisha...

Cha msingi usikimbilie kuacha kazi ghafla, lazima ujipange Kwanza, ujipange kimtaji (X2), ujipange kiroho na kimwili, ujipange kimaarifa....ukishajipanga sasa unachomoka bila kuangalia nyuma....

No risk no rewards, No discipline no results...kama ikikufaa zaidi tumia filosofi ya kijapani inaitwa IKIGAI (nenda Google au youtube ukaitafute).

NB: Usiombe ushauri wa kujiajiri Kwa mtu ambaye hajawahi kujiajiri...zingatia Sana Hili.
 
Anzisha Biashara ukiwa humo humo kwenye ajira hadi hiyo biashara ianze kukupa return mara 5 au zaidi ya unachopata kwenye ajira usithubutu kuacha kazi akakimbilia kujiajiri.
Kujiajiri hakutaki watu legelege utaishia kuongea mwenyewe barabarani.
Hata ukiona mtu anachoma mahindi barabarani ujue yupo smart masna siikila mtu anaweza kufanya hivyo
Siyo rahisi kihivyo kwa muajiriwa kuanzisha biashara ikasimama kwa viwango hivyo,wakati muda mwingi unaitumikia serikali kuanzia sa 1 asbh mpaka sa 9 na nusu jion
 
Mtafute ANKO T utoboe fasta.

Watu wanatajirika kwa kuendeleza walipoacha wazazi wao, wewe umezaliwa Juzi tu unataka utoboe ndani ya miaka 3.

Baba na Babu yako hawajaacha kitu. Huna kipaji chochote wala bahati.

Jichunge utaanza kufirwa muda si mrefu.
Mhhhh ko unataka kusema kinyeo kina leta utajiri???? ungekuta watu wote ni matajiri maana Kila mtu ana kinyeo, hakuna mtu anaupenda umaskini, kila mtu anapenda utajiri
 
Fanya yote mkuu, ila usiache KAZI ukaenda, kujiajiri utakufa kwa presha kaka mtaani kugumu sana, jitahidi tu kuwa mbunifu sahivi tech imerahisisha sana unaweza endesha duka ukiwa ofisini ulipo ajiriwa. Tena bila shida kabisa na washikaji zangu Wana maduka na Wana ajira serikalin, na maisha yanaenda, Tena Kuna muda duka Lina buma anasubiri mshahara umuboost.
 
Vp
Ili umiliki ukwasi wa maana ni lazima ujiajiri mwenyewe ,ukitegemea kuajiriwa hautoboi unless otherwise uwe mwizi ambapo lazima utastukiwa na kufukuzwa kazi.

Mwajiri hata akiiingiza Bilioni wewe atakupa Mshahra wako manara tu(Laki 7).

Kama ukiajiriwa jitahidi uwe na kipato kingine nje ya mshahara hapo kazi utaona nzuri lakini ukitegemea salary 100% utaumia.
VP kuajiriwa TRA nako hutoboi???
 
Fungua kiduka chako pembeni kidogo kidogo uwe unatibia watoto homa homa mdogo mdogo atatokea mfadhili mbele ya safari huko akakuamini mkafungua hospital kubwa
Mhhhh mfadhili Tena!!!!?????, Hapo kwenye mfadhili awe makini asiombwe rinda, Dunia skuizi imevaa sketi

Akijaa kwenye mfumo anafadhiliwa Kwa masharti na rinda linaliwa

Na akiliachia rinda siku moja tuu Kwa tamaa ya mabilioni ndo basi Tena mpaka anakufa ataendelea kutafunwa rinda, Yani ndo imeisha hiyo hawezi pona tena hio tabia.
 
Siku baada ya siku sioni dalili ya kutoboa kupitia haya maisha ya kuajiriwa mambo yanazidi kuwa tough familia inaanza kukua kwa mshahara huu wa single digit sina hakika kama kuna kutoboa bila kuchukua action sasa

Kinachouma zaidi kuna watu huo mshahara wako ni per diem ya siku mbili tu aisee haki iko wapi? Kusema ukweli huku kuajiriwa ni hatari sana sijasema kuajiriwa ni kubaya ila shida je unalipwa kiasi gani? Yaani kuna sehemu ukiajiriwa au kuna halmashauri ukiajiriwa unajichimbia kaburi tu kutoboa hapo sahau kabisa aisee bila maamuzi magumu kutoboa nitakusikia tu kwenye bomba yaani huku Afya mnafanya kazi kubwa ila Mshahara wenyewe kuduchuu yaani unakuta hamna semina, hamna extra duty wala pesa nje ya mshahara wewe ni kutegemea mshahara tu full stop hii haikubaliki kabisa

Acha kazi ujiajiri.
 
Back
Top Bottom