Bila kuzuia kivitendo matumizi ya mkaa kwa taasisi mazingira yataendelea kuharibika

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,869
9,692
Ipo haja kutekeleza kivitendo makatazo ya taasisi mbalimbali nchini Tanzania kutumia nishati ya mkaa na kuni kulisha watu wao
Taasisi kama vile
Vyuo Vikuu
Magereza
Mashule
Viwanda vya chai na tumbaku
Nakadhalika

Hawa wote wapigwe marufuku kutumia mkaa na usimamizi wa NEMC uwe wa kivitendo.

Tukileta utani tutageuka jangwa. Idadi yetu inaongezeka na matumizi ya mkaa yanapanda kila siku.

Viwanda vya chai na tumbaku vitumie nishati mbadala na sio kuni.
 
Unawaza kinyume. Waambie pamoja na utajiri wa gesi na umeme wa ziada ambao hautumiki mpaka sasa viwe nishati mbadla wa mkaa.

Unit za umeme zipungue bei
Gesi isambazwe majumbani kwa bei nafuu uone kama kuna mtu atapambana ma mkaa.

Chekecha akili yako tena
 
Bei ya gesi si rafiki kwa ujumla

Kingine ni dhana hasi kua chakula cha kupikwa kwa kuni na makaa ni kitamu

Kwa mashule na magereza ni vyema wakapatiwa miradi ya ng'ombe na waweze kuzalisha biogas itawasaidia zaidi kuliko kutumia magogo ya kuni
 
Back
Top Bottom