Vitoe vitabu vya dini halafu rudi kwenye tamaduni zako za asili utajikuta unarudi palepale,kwamba bikra ni kitu cha thamani kwa mwanaume wa jamii yoyote. Duniani kuna watu wa tamaduni na asili tofauti,hawajawahi kukutana kusema waliweka kikao cha kukubaliana kuhusu thamani ya mwanake mwenye bikra, ila still jamii zote duniani bikra wanaipa thamani.
Bikra ni kielelezo cha uwajibikaji wa mwanamke katika kujitunza na kwa mwanaume kwake ni kitu cha thamani mno haijalishi kama anaamini kwenye dini au laah. Halafu kama hujui hamna dhambi mbaya kama kutokuwajibika, ukishindwa kuwajibika kuna vitu vibaya utaviona vya kawaida sana, mfano kubadilisha mabwana, kutoa mimba nk hivi vishakuwa vya kawaida. Bikra ni mali yako na ipo chini ya maamuzi yako, husiipoteze kwa tamaa zako, itunze kwa ajili ya mme wako wa ndoa.
Ila tukubali kiujumla jamii nzima tumefeli kwenye swala uwajibikaji na malezi,ndio maana siku hizi umalaya kawaida, kubadilisha mabwana kawaida, kutoa mimba kawaida, single parenting kawaida, kubambikizana watoto kawaida, watoto wa mitaani kawaida na tunapo elekea hata upunga utakuwa kawaida nk ukitizama kwa jicho la hekima utajua tu hayo yote ni matunda ya zinaa,yatokanayo na kutokuwajibika.Kutokuwajibika kwenye kitu fulani, kusifanye hiko kitu kuwa halali.
Ila yote kwa yote kila mtu ana preferences zake,wanawake kwenu mbele ya macho yenu mwanaume mwenye fedha ni wathamani, nyie tabia kwenu sio kipaumbele. Ila kwa wanaume bikra/purity ni ya thamani ipo hivyo na itabaki kuwa hivyo,so kila mtu ashike lake.