Bikira mnadani

Bikira mnadani

Glucky

Senior Member
Joined
Dec 16, 2009
Posts
123
Reaction score
41
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 aliinadi bikira yake kwenye mtandao wa www.ineed.co.nz baada ya kukabiliwa na ukata wa pesa.

Mwanafunzi huyo anayejiita "Unigirl" alijitambulisha kuwa yeye ni mrembo mwenye kuvutia, yuko fiti na mwenye afya njema.

Zaidi ya watu 1,000 walijaribu kuinunua bikira yake lakini mwanaume mmoja ambaye hakutajwa jina lake aliibuka mshindi baada ya kuweka dau kubwa la dola 31,900. (Takribani Tsh. Milioni 42).

"Nawashukuru watu wote zaidi ya 30,000 waliolitembelea tangazo langu, na zaidi ya watu 1,200 walioweka madau yao kuinunua bikira yangu", alisema mwanafunzi huyo.

"Dau lililoshinda ni kubwa sana kuliko hata nilivyotarajia".

Mwanafunzi huyo alisema kuwa hajawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na pesa atakazopata atazitumia kulipia masomo yake.

Mwanafunzi huyo aliendelea kusema kuwa ili mradi masuala ya afya yake yatapewa kipaumbele hana hiana kumtunuku bikira yake mwanaume yoyote yule bila kubagua kabila wala umri ilimradi apate pesa za kulipia masomo yake.

Mmiliki wa tovuti iliyotumika kuinadi bikira hiyo, Ross MacKenzie, alisema kuwa tangazo la mwanafunzi huyo lilikuwa ni halali kisheria na hakuna sheria yoyote iliyovunjwa.

Mwanafunzi huyo aligoma kufanya mahojiano na waandishi wa habari lakini MacKenzie, aliliambia gazeti la Waikato Times kuwa ameruhusiwa kutaja kiasi cha dau lililoshinda bila kutoa maelezo ya ziada.

Matukio ya wanawake kuzinadi bikira zao kwenye internet yaliibuka kwa kasi baada ya mwanafunzi wa Marekani Natalie Dylan ,22, kuinadi bikira yake na kupata mteja aliyeweka dau la dola milioni 3.7.

Natalie naye wakati anainadi bikira yake alitoa sababu kama hizi kuwa anatafuta pesa za kulipia masomo yake.

Mwezi mei mwaka jana nchini Ujerumani, mwanamke mmoja toka Romania, Alina Percea, 18, aliinadi bikira yake kwa matumaini ya kuingiza mamilioni kama Natalie lakini aliambulia euro 10,000 tu toka kwa mfanyabiashara wa Italia mwenye umri wa miaka 45 aliyeshinda katika mnada huo.

Mbali ya kupata dau dogo, Alina alipata hasara zaidi baada ya maafisa kodi wa Ujerumani kuzikata kodi pesa alizopata kwa kuinadi bikira yake akiambiwa kuwa alichofanya ni sawa na wanachofanya makahaba ambao nao wanalipa kodi kwa shughuli zao.

Alina alibakia na karibia nusu ya pesa alizopata baada ya makato ya kodi kufanyika.
 
Mmmmh kama hawajaambulia patupu

kuna bibi yuko hapa,wengi wanakuja kutoka mjini, wanasukwa ile mbaya, akienda mjini kuwaonjesha baada ya muda mfupi jamaa anatangaza ndoa.
Jeni, ntakupeleka ukajionee mwenyewe, utatengenezwa halafu utakuja kutupa ushuhuda.
 
Huyo bibi si angekuwa bilionea??????
Jeni usiende ukja oza machine ukabaki kutumiwa t...gooooooo!!! lol.
 
eeeeeeeeeeeeeh ww uncle kwani jenny kakwambia sio bikiraaaaaaaaaaa?
kuna bibi yuko hapa,wengi wanakuja kutoka mjini, wanasukwa ile mbaya, akienda mjini kuwaonjesha baada ya muda mfupi jamaa anatangaza ndoa.
Jeni, ntakupeleka ukajionee mwenyewe, utatengenezwa halafu utakuja kutupa ushuhuda.
 
kuna bibi yuko hapa,wengi wanakuja kutoka mjini, wanasukwa ile mbaya, akienda mjini kuwaonjesha baada ya muda mfupi jamaa anatangaza ndoa.
Jeni, ntakupeleka ukajionee mwenyewe, utatengenezwa halafu utakuja kutupa ushuhuda.

Duh kwa staili hii ngoma haitaisha ..mtu unajitumbukiza mzima mzima ukijua hapa kuna mwali lol
 
eeeeeeeeeeeeeh ww uncle kwani jenny kakwambia sio bikiraaaaaaaaaaa?

Nadhani ni shahidi kuwa Jenny hana tena ubikira, lakini anaweza kutengenezwa kichina. Labda aliondoa mwenyewe.
 
mungu wangu jamani kweli shida ni mbaya sana ..

Hoja hapa sio shida FirstLady,hoja ni zuri na umuhimu wa bikira..Mimi naona wamefanya jambo la maana kuliko nyie wabongo mnaodai ooh bikira heshima bora yeye amejipatia na pesa za kumsaidia kwenye masomo yake..Je sisi wanaume are we paying money pale tunapowakuta wapenzi wetu ni virgin?Vipi FirstLady wewe ulishia kuambiwa hongera sana basi.
 
Mbona humu leo thread za bikira zimekuwa nyingi sana?
 
Hoja hapa sio shida FirstLady,hoja ni zuri na umuhimu wa bikira..Mimi naona wamefanya jambo la maana kuliko nyie wabongo mnaodai ooh bikira heshima bora yeye amejipatia na pesa za kumsaidia kwenye masomo yake..Je sisi wanaume are we paying money pale tunapowakuta wapenzi wetu ni virgin?Vipi FirstLady wewe ulishia kuambiwa hongera sana basi.
Dah, this is so funny!
 
Mimi nilipewa senksi, na hela ya taxi, hela ya pain killers,,,, na usimwambie mama...
 
Back
Top Bottom