Biharamulo: Picha ya mtoto akisomea kwenye taa za barabarani

Aisee ?!!!!!

Hivi vidude vinauzwa kiasi gani, je ni gharama kuliko hio camera jamaa aliyotumia

images
Mwanga wake ni afifu sana labda kama unatafuta upofu kwa lazima, sasa kama familia sometime inakosa mafuta ya taa ya 500 au buku, hicho kidude kinauzwa 3000 mpaka 5000 na kinaweza kuharibika ndani ya mwezi mmoja au mvua ikinyesha mfululizo siku 2,3 kinakuwa hakifanyi kazi, je dogo atakaa asubiri hicho kitaa kwanini asiende barbarani akafanya kazi zake.
 
Aisee babu zako na bibi zako waliosomea koroboi na karabai walipofuka mara ngapi unajua LED Lights za sasa huenda ni efficient na zina mwanga kuliko taa ya 100 watts walitumia watu miaka kadhaa iliyopita unaongelea kuweza kuharibika kwa mwezi (kwamba havipo vinavyokaa miaka) kwahio mvua ikinyensha mfululizo siku mbili au tatu unaenda kusoma kwenye taa barabarani ?

Kwahio na wewe town Makamba akikata umeme huwa unakwenda Barabarani kufanya kazi zako ? Na dogo akijua mvua leo imenyesha huenda afanye kazi zake mapema zaidi (Time management ni moja ya Elimu inayofaa katika Maisha)..., Ulizia Babu mzaa babu yako kama yupo na kama alikuwa kama watanzania majority atakwambia alisoma saa ngapi na ng'ombe alichunga saa ngapi na kuti kutafuta na kukata saa ngapi... By the way kama hapo kuna mbu aongee na gharama ya kuumwa mbu hence kujitibu Malaria...

Narudia tena kwa kusaidia huyo aliyempiga picha amsaidie kwa kumnunulia taa ya Solar.....

Au kama vipi Necessity being the mover of all invention ajaribu hata kutengeneza mechanical light ambayo ni powered ni gravity kama anaogopa siku tatu mvua ikinyesha mfululizo
 
KATORO NA BIHARAMULO KUNA WAHAYA WA KUTOSHA KAMA KAWAIDA JAPO PALIKUWA MPAKANI MWA KAGERA NA MWANZA KABLA YA KUPATIKANA MKOA MPYA WA GEITA.
 
Kuna ujumbe huu niliusoma kwenye lori "KUSOMA KUFAULU, KUKESHA MBWEMBWE" awe makini ujumbe huu usije ukamhusu.
 
Picha inasambaa kama moto wa kifuu Africa na duniani ikimuonesha mtoto mmoja mpenda shule akipigia msuli kwenye taa za barabarani hivi majuzi huku akiwa amevalia tisheti ya timu ya taifa ya Tanzania (taifa stars).

Barabara hiyo ambayo haiko busy sana imewekewa taa za barabarani hivi karibuni.

USSR View attachment 2580948

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo kawaida ya Watoto wa siku hizi,wakipata kaupenyo kakufungua daftari basi wanafungua hapohapo, kwa mfano naonaga vitoto vya shule vikiandika notes kwenye Pantoni za kule Kigamboni, na raia wala hawastuki!!
 
Waziri wa Nishati naye atakuja na takwimu zake za kunjunga kuwa keshapeleka umeme kaya bilioni 5.
 
Picha inasambaa kama moto wa kifuu Africa na duniani ikimuonesha mtoto mmoja mpenda shule akipigia msuli kwenye taa za barabarani hivi majuzi huku akiwa amevalia tisheti ya timu ya taifa ya Tanzania (taifa stars).

Barabara hiyo ambayo haiko busy sana imewekewa taa za barabarani hivi karibuni.

USSR View attachment 2580948

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu dogo atakuja kuwa engineer 🙏
 
Tanzania hii....!

Yani mtoto kaamua aende kwenye Taa za Barabarani kufanya kazi zake za Shule...

Huku kuna watu wanateseka na kuumizwa.
 
Natumaini pasaka inaendelea vyema;

Katika picha ya kijana inayosambaa mitandaoni ikimuonesha akitumianmwanga wa taa za barabarani kujisomea umenipa maswali mengi sana hasa kwa jamii zetu nyingi hapa nchini kwa sisi watu wa chini ni ukweli usiopingika kwamba hatupendi kujihangaisha.
Maswali niliyojiuliza ni kama haya;
1. Kama mtu anashindwa kuutumia mwanga huo kuchoma mahindi,kuuza karanga au kufanya biashara yoyote,inawezekana vipi mtanzania huyuhuyu akautumia mwanga huo kujisomea?
2.mazingira kama hayo anawezaje kuelewa anachoandika? Kwasababu ya upepo unaosababishwa na magari na makelele pia?
3. Huwa anasoma kila siku? Kwasababu suala la kusoma usiku ni la kila mara kama kupumzika labda kwa wiki mara mbili au tatu.
FB_IMG_1681057869238.jpg
 
Huyo ni mtoto atafanyaje biashara usiku huo? Hapo anaandika homework fasta fasta na kurudi kwao
 
Inawezekana dogo alikuwa akimsubiri mwenzie akaona isiwe tabu, ngoja akumbushie baadhi ya 'definitions'
 
Back
Top Bottom