Big up Lowassa kazana uchukue nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Big up Lowassa kazana uchukue nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kada Deya, Nov 24, 2011.

 1. K

  Kada Deya Senior Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nampongeza sana lowasa kwa kunyamazisha vuvuzela zote zilizopanga kufuka moshi kwenye kikao cha cc dodoma akiwemo nape nnauye ambaye kimsingi amefyata mkia!!!!!!!!!!!!!
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  La kuchukua nchi usijidanganye kaka labda aichukue hiyo hiyo ccm yenu inayomdekeza!
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Akazane na nani? Hili neno Samuel Sitta alishawahi likataa..............
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Tutamwomba Nape afunge rasmi domo lake.
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape ni sawa na kelele za mlango hazimnyimi Lowassa usingizi.
   
 6. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  achukue inchi au achukue nchi? au nawe ni vuvuzela?
   
 7. M

  Mbonafingi Senior Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajidanganya hamuwezi kumtakasa fisadi Lowasa mbele ya macho ya Watanganyika wala mhambi zake haziwezi kufutika mioyoni mwetu. Jidanganyeni wenyewe ccm sio watanganyika
   
 8. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  2015 tunahitaji rais mtendaji na shupavu(Jasiri).Lowassa daima
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kuna mijitu imepinda humu ndani!
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kweli wewe humjui lowassa. pia wewe ndio vuvuzela mkubwa wa lowassa:photo::lol::spy:
   
 11. A

  Anold JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Labda wewe usimpe kura watu kibao wakiwemo wasomi wanaopima mambo kwa kina wameshasema kura zao kwa Lowasa kama ataamua kugombea, fitna hazina nafasi. Nikurudishe nyuma kidogo kwa Rais zuma wa Africa Kusini, aliwekewa zengwe la tuhuma za kupangwa akazipangua zote mahakamani maana hawakuwa na ushahidi wa kutosha na sasa ni rais wa Afrika ya Kusini. Wewe unahaki ya kumpigia kura mtu anayemtaka ila huna haki ya kuzuia watanzania kuchangua mtu wanayemtaka. Tanzania tunahitaji watu wanaoweza kufanya mambo yatokee sio watu wenye nadharia za kusadikika!:eyebrows:
   
 12. M

  Mbonafingi Senior Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usituchafue. vibaraka wakubwa nyie mnaoshabikia dhambi. Unalipwa kiasi gani hautofautiani na wale waliozimia igunga
   
 13. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huko mnako mpeleka Lowasa ni upotevuni,Mwalimu alisema,huyu ni fisadi na hafai kuhudumu nafasi yoyote ya umma.Ninyi mkampa kua PM,nini kilitokea???????

  Msimdanganye enyi wanafiki kwa Manufaa yenu binafsi,akapumzike,alipofika panatosha si haba.......
   
 14. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I am slowly starting to be convinced that Lowassa is more of a presidential material than JK and the fact that he's decided to lean on the youth for helping him campaign for 2015 poll tells something on how strategic he is. Unofficial opinion polls suggest that Lowassa's approval ratings have recently surged to 55 percent with more of his supporters being university students and the clerics. I, myself, do not side with Lowassa given his bad history but I'm increasingly interested with the way he shrewdly carry out with his tactical campaigns towards 2015 electons.
   
 15. K

  Kada Deya Senior Member

  #15
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Who is samwel sitta mnafiki kama wanafiki wengine ana uchu wa madaraka tu
   
 16. K

  Kada Deya Senior Member

  #16
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mwalimu alisema kipindi cha Analogy this is DIGITAL age.
   
 17. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Anakulipa shilingi ngapi.
  OTIS.
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  we mnyisanzu ni nani amekuloga kiasi cha kudevelop sighn za ward za mirembe! mimi nijuavyo lowasa ni jasiri wa kukiuka taratibu na sheria, ni jasiri kupanga mipango ya kujinufaisha kwa hasara ya masikini, pia ni shupavu kutetea uovu wake, ni shupavu kutoa rushwa, ni shupavu kugombea madaraka, haya taja ujasi na ushupavu wa lowasa wako.
   
 19. k

  kizungwangoma New Member

  #19
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kiukweli mi nimemkubali jamaaa lowassa anaweza he is the specail one.kimfano cheki nape alivyokua moto afu msikie sas kama punga vile.
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Gamba gumu CCM
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 23 November 2011 20:45 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  [​IMG]Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) akiwasalimia wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Edward Lowassa (wapili kushoto) na Kingunge Ngombale-Mwilu kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC, Makao Makuu ya Chama hicho mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

  WATUHUMIWA WAGOMA KUJIUZULU,JK AHOJI UVCCM WALIKOPATA FEDHA
  Neville Meena, Dodoma
  UTEKELEZAJI wa mpango wa CCM uliolenga kuwashinikiza watuhumiwa wa ufisadi kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho, umechukua sura mpya na sasa Kamati Kuu (CC) inaomba ipewe kibali cha kuwachukulia hatua zaidi wale ambao wamegoma kujiuzulu.Juzi, katika kikao chake mjini hapa, CC iliazimia kuomba idhini ya Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM ili ifanye kazi hiyo baada ya kuwepo ukimya ambao unaashiria kutokuwepo viongozi na makada ambao wako tayari kujiuzulu nyadhifa zao kwa hiari.

  Tangu kupitishwa kwa mpango huo maarufu kwa jina la kujivua gamba katika kikao cha NEC kilichopita cha Aprili mwaka huu, ni kada mmoja tu, Rostam Aziz aliyechukua hatua za kujiuzulu ubunge wa Jimbo la Igunga na ujumbe wa NEC, lakini wengine wamekuwa kimya hadi sasa.

  Katika kikao cha Aprili NEC hiyo ya CCM ilipitisha maazimio 26 lakini kubwa ni lile lililokuwa likihimiza vita dhidi ya ufisadi kuendelea na kutoa mwito kwa watu wanaotajwa na jamii kuhusika na ufisadi ambao wako ndani ya chama kujitathmini kisha kuchukua hatua za kuachia madaraka waliyo nayo.

  Sehemu ya mwisho ya azimio hilo inasomeka: “Wasipoachia madaraka chama kiwachukulie hatua mara moja.”

  Mmoja wa wajumbe wa CC ambaye ameomba jina lake kuhifadhiwa alisema: “Tunawaomba NEC waturuhusu jambo hili tulifanyie kazi sisi (CC) na litafanyiwa kazi kupitia taratibu za kawaida za chama kwa kuzingatia kanuni na taratibu za maadili za chama hicho.”

  Kubadilika kwa utaratibu wa kuwashughulikia watuhumiwa wa ufisadi, kulipokewa kwa shangwe na wafuasi wa watuhumiwa hao ambao wanasema kulikuwa na ajenda ya siri, kubwa likiwa ni vita ya urais wa 2015.

  Hata hivyo, kada mwingine ambaye yuko karibu wa vigogo wa chama hicho alisema: “Hivi sasa hali itakuwa mbaya zaidi kwa watuhumiwa, tunakokwenda si hiari tena itakuwa ni lazima ikiwa chama kitawapata na hatia.”

  “Ujue azimio la kwanza lilikuwa na pande mbili, kwanza ni watuhumiwa hao kujipima wenyewe kisha kuchukua hatua, lakini pili ni upande wa chama, sasa ukomo wa upande wa kwanza ambao ni kuchukua hatua wenyewe umekwisha, sasa ni zamu ya upande wa pili ambao ni wa chama,” alisema kada huyo ambaye pia ni mshiriki wa vikao vya uamuzi ndani ya CCM.

  Makatibu wapya
  Halmashauri ya CCM iliyoanza mkutano wake jana, ilifanya mabadiliko ya makatibu wa chama hicho katika mikoa sita.Walioteuliwa ni Joyce Masunga, Mohamed Nyawenga, Pazi Mamulima, Zainab Shomari, Abdallah Mihewa na Rahel Ndegeleki ambao watapangiwa vituo vya kazi hivi karibuni.

  Habari kutoka katika kikao cha Kamati Kuu zinasema kwamba imebariki pendekezo la kumvua madaraka kiongozi mmoja wa ngazi za juu baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubadili orodha ya matokeo ya kura za madiwani wa Viti Maalumu bila kushirikisha vikao husika.

  Kigogo huyo alitiwa hatiani kuchakachua orodha ya madiwani iliyowasilishwa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuondoa jina namba mbili katika mtiririko wa orodha hiyo na kuliweka chini, hivyo kumkosesha mmoja wa makada wa chama chake nafasi ya kuwa diwani.

  Kikwete anena
  Kikao cha NEC kilianza jana saa 5:00 asubuhi kwa Rais Kikwete kuwatoa hofu wajumbe akisema hakuna kitakachoharibika. Mara baada ya kuingia, Rais Kikwete aliwasalimu wajumbe akisema: “Jamani hamjambo …. mmelala salama?” Baada ya wajumbe kujibu ndiyo aliongeza:

  “Mbona nimeambiwa kwamba wajumbe wengine hamjalala vizuri, mmelala na hofu tu, CCM ni chama kikubwa, kwa hiyo jamani tulieni hapa hakuna jambo litakaloharibika, watu msiwe na hofu,” alisema kisha kutamka kwamba kikao hicho kimefunguliwa rasmi na kuwataka waandishi wa habari kutoka ndani ya ukumbi wa mikutano.

  Kauli ya Kikwete ilikuwa ni kama mwangwi wa yaliyotokea juzi usiku baada ya kumalizika kwa kikao cha CC, kwani wapambe wa makundi mawili hasimu ndani ya chama hicho yalikuwa yakihaha kushawishi kuungwa mkono na wajumbe wakati wa vikao vya NEC.

  Kati ya saa saba na nane usiku wa kuamkia jana, wapambe wa makundi hayo na mmoja kati ya makada hao alisikika akisema kuwa: “Ujue sikulala kabisa na sasa naingia kwenye NEC, fitina ilikuwa kubwa sana jana (juzi) usiku, lakini tutashinda tu.”

  Kundi la makada wanaojipambanua kuwa wapambanaji wa ufisadi walikuwa wakihaha kushawishi wajumbe wa NEC kukataa uamuzi wa suala la kujivua gamba kurejeshwa CC, wakati kundi la pili lilikuwa likishawishi wajumbe kusimama kidete na kuunga mkono pendekezo hilo.

  Habari zilizopatikana jana jioni zinadai kuwa, jana NEC haikuwa imejadili suala lolote kuhusu kujivua gamba na kwamba hata mmoja wa wajumbe ambaye amekuwa akitajwa katika suala hilo, Edward Lowassa alipotaka kulizungumzia aliambiwa asubiri wakati mwafaka wa ajenda husika.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu pendekezo hilo alisema: “Jamani, kikao hiki bado kinaendelea, kama kuna jambo lolote mimi niliwaahidi kwamba niko tayari kuwaambia.”

  “Kwa sasa siwezi kuzungumza lolote zaidi ya yale niliyowafahamisha leo (jana) mchana na ujue kwamba yapo mambo mengi ambayo ili kwenda kwa umma lazima yapate kibali cha NEC, vinginevyo nitakuwa navunja taratibu,” alisema Nape.

  Kombora UVCCM
  Katika hatua nyingine, kundi la viongozi na marafiki wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) lililopo Dodoma, jana lilitaharuki baada ya kupokea taarifa za kurushiwa makombora, huku Rais Kikwete akiwazodoa kwa kuwaambia: ‘Msitutishe,’ ishara ya kukerwa na taarifa kwamba vijana hao walitishia kuhamia Chadema ikiwa Umoja wao utavunjwa.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao cha CC kilichomalizika juzi usiku zinasema, ajenda kuhusu UVCCM ni kama haikuwa rasmi lakini baada ya kuibuliwa na Nape ilisababisha Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Benno Malisa kusakamwa ipasavyo na kutishwa kwamba hatima yake kisiasa inaweza kuwa mbaya.

  “Yule bwana mdogo (Benno) alipata wakati mgumu sana, maana wale wazee walimshughulikia ipasavyo, alijaribu kujitetea lakini haikusaidia, kweli nilimwonea huruma sana maana hakuwa na mtetezi mle ndani,” kilisema chanzo kingine kutoka ndani ya CC.

  Taarifa hizo ziliendelea kudai kuwa Nape aliomba kikao hicho kimpe majibu ya kutoa kwa waandishi wa habari ambao wamekuwa wakimwuliza kuhusu suala hilo ambalo alisema hakuwa na majibu.

  “Nimeambiwa UVCCM viongozi wa mikoa na baadhi ya wilaya wako hapa, mwenyekiti naomba nipate majibu nisaidiwe katika hili, kama ni Baraza Kuu linakutana nifahamu na kama kuna mkutano mwingine nijue pia, lakini hali hii inaniweka katika wakati mgumu mimi kama mwenezi,” alinukuliwa Nape na chanzo chetu ndani ya CC.

  Maelezo hayo yalisababisha Benno kusimama kutoa utetezi ambao hata hivyo, haukusikilizwa na hapo wajumbe wawili, Mawaziri, William Lukuvi na Steven Wassira kila mmoja kwa wakati wake, aliushambulia umoja huo.

  Inadaiwa kuwa Rais Kikwete ndiye aliyegongelea msumari wa mwisho pale aliponukuliwa na mtoa taarifa wetu akisema: “Mnataka kututisha, msitutishe hata kidogo maana nasikia kwamba mnataka kwenda Chadema, nendeni hata kesho, au mnasubiri tuuvunje ndiyo muondoke!”Kadhalika Rais alinukuliwa akihoji vijana hao walikopata fedha zinazowawezesha kukaa hapa kwa muda wote huku akiwakumbusha kwamba CCM hakiwezi kuyumba ikiwa kitawatimua kwani kimewahi kufanya hivyo kwa viongozi wa ngazi za juu.

  Pamoja na hali hiyo, viongozi wengi wa UVCCM wa mikoa na wilaya mbalimbali nchini bado wapo Dodoma na baadhi yao walisema huenda wakatoa tamko baada ya kikao cha NEC kumalizika.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 20. K

  Kada Deya Senior Member

  #20
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Lowasa hakuwepo igunga
   
Loading...