Nilitaka kujiunga na CRDB siku za nyumba lakini niliamua ku-cancel forever wazo hilo baada ya fedha nyingi za UFISADI hasa wa EPA kuonekana zilipitia CRDB. Hadi benki ya Wakenya KCB walistukia dili la EPA na kukataa baadhi ya fedha kupitishwa kwenye benki yao lakini benki 'yetu' CRDB ilikubali uchafu huo.
Nadhani badala ya kusifia kila kitu kuna haja sasa ya sisi wananchi kuzisusia taasisi za kibiashara zitakazoonekana ku-support ufisadi kwa njia moja ama nyingine IWE KWA KUJUA, KUTOKUJUA, AU KWA BAHATI MBAYA hata kama watatoa huduma nzuri namna gani! In the long run ni sisi wananchi ndio tutakaoumia kwa vitendo vyao. Ni wajibu wao kuhakikisha hilo halitokei.