Bidhaa za Ukweli ni Kutoka Uturuki!. Karibu Uje Ushuhudie!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,291
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,291 2,000
Wanabodi, kuna ule msemo wa Kiswahili usemao, "Kizuri Kula Na Mwenzio"!.

Wengi wa sisi Watanzania ni "wachoyo", vitu vizuri tunapenda kula wenyewe tuu!, hatupendi kuwashirikisha wenzetu!, ndio maana utakuta Watanzania wenye mafanikio ya ukweli ni wachache na hawapendi kuweka wazi siri za mafanikio yao ili na wengine wasifanikiwe kama wao!.

Sasa mimi nimeamua kujitolea kuwamegea nanyi wenzangu kizuri hiki ili usiendelee kudanganywa kwa kutojua, labda tuu muendelee kudanganywa kwa kupenda wenyewe!.

Kizuri hiki ni kuhusu uibora wa bidhaa za ukweli kutoka nchini Uturuki. Watanzania tumekuwa tukiuziwa bidhaa za ubora wa hali ya chini sana kutoka China, na nyingi ya bidhaa hizo zikiwa ni fake!.

Sasa ili kuzitambua bidhaa fake, kwanza ni lazima utambue bidhaa za ukweli ndipo utangamanishe na hizo fake, ukiendelea kuzikumbatia fake, angalau uzukumbatie huku ukijua kuliko hali ilivyo sasa, wengi wananunua bidhaa za fake kwa kutokujua!.

Watanzania sasa tumepatiwa fursa za kutambua bidhaa za ukweli kutoka nchini Uturuki katika maonyesho ya siku 3 ya bidhaa kutoka nchini Uturuki yatakayofanyika kuanzia kesho mpaka Jumamosi, ndani ya Uwanja wa Saba Saba kuanzia saa 4:00 asubuhi -1:00 usiku.

Wana jf wenzangu mnaopenda bidhaa za ukweli, karibuni sana, tukutane pale, kwa mfano mimi ni mdau mkubwa sana wa vazi la suti, kuanzia za mtumba, za Mchina, za Mzungu na sasa za Mturuki!.

Jijini Dar, maduka wanaoleta suti za ukweli, ukiondoa AK's na Famozo pale JM Mall, hawa wengine wengi including majina makubwa akiwemo Mwasu, Marriedo, yule dada pale pembeni ya Best Bite, na maduka fulani fulani ya imported suits ndio wanaoleta genuine piece by piece na famba ndani yake!. Hizi suti za Uturuki zote ni suti kweli na kitu kizuri zaidi, hazina bei!.

Kuanzia kesho mpaka Ijumaa, nitajitolea ku run TV series za program 4 dedicated kwenye maonyesho haya ili angalau nyinyi mlioko majumbani mpate japo picha kwa kutokufika Saba Saba, what will you be missing!.

Please be there!

Karibu Sana

Pascal.
 

Attachments:

saitama_kein

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Messages
982
Points
170

saitama_kein

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2009
982 170
Wanabodi, kuna ule msemo wa Kiswahili usemao, "Kizuri Kula Na Mwenzio"!
Pia kuna msemo wa Kiswahili usemao, "Kizuri chajiuza Na Kibaya chajitembeza"......Misemo yote yawezekana kuwa na ukweli katika maonyesho hayo.....Ushauri wangu kwa ndugu wana JF "Akili za Kuambiwa Changanya na za Kwako- JK"
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,291
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,291 2,000
Ni suti tu? Nini vingine ili tuje, joto na suti na gari hauna ni uzezeta kama sera ya kuvuana magamba
Mkuu Nyakageni, nakubaliana na wewe, ila usichojua ni baadhi ya wavaa suti wetu huku Afrika, tunakabiliwa na kasumba ya ushamba wa suti za ulaya. Kufuatia majira ya baridi kwa nchi za wenzetu, wanatengeneza suti nzito za wool tena sometimes, 3 pieces ili kujitia joto!. Sisi kwa kutokujua kuwa zile suti were ment for winter, unamkuta mtu amepiga 3 pieces yake kituo cha dala dala!.

Njoo uone light suits kwa mazingira ya joto, mfano ukivaa linen suit, hutoki jasho ni kama umevaa shati tuu.

Ila kabla hujaja, pitia lists ya products ujiridhishe kwanza, it will be a wastage of your precious time, kama utafunga safari kuja maonyeshoi kwa ajili ya suti tuu!.

Pascal.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,291
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,291 2,000
tunashukuru kwa taarifa, nadhan ni fursa njema kwa wajasiriamali wakubwa/wadogo kuhudhuria maonyesho, ili kuona bidhaa za kituruk lakini pia kuweza kupata uwakala wa bidhaa tofauti.
Mkuu Tisa Desemba, hili ndilo lengo lao, mwanzo mimi nilidhani ni maonyesho ya gulio kama yale yetu ya sabasaba kwa watu kujitokeza kwa wingi, kuja kujisombea bidhaa za mahitaji madogo madogo. kumbe no!. Waturuki means bussiness, wamekuja kufanya marketing ya products zao na kutafuta wabia.

Kiukweli umasikini wetu mwingine ni umasikini wa kujitakia kwa kutojua tuu, wengi wanadhani ili mtu ufanye biashara kubwa ni lazima uwe na mtaji mkubwa!, no way!. Mtaji mkubwa kuliko wote ni "The Will" to do business!, hizi producta wao watakuletea on hire purchase on credit, ukishauza, unakata commission yako, unawapelekea pesa yao!.
Pascal.
 

Kidzude

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2011
Messages
4,435
Points
2,000

Kidzude

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2011
4,435 2,000
Hujasema kipindi chako kitaonyeshwa katika TV station gani na muda gani pia hiyo list ya bidhaa iko wapi.
Nadhani angeandika hivi. Bidhaa nzuri zilizotengenezwa Tanzania kwa teknolojia ya Turkey. Mnalia maskini kumbe kazi yenu kununua bidhaa za wenzenu zenu mwazitosa. Next time andika hivi NUNUA BIDHAA ZA KTZ ZILIZOTENGENEZWA KA GERAMNY TEKNOLOGY, TUTAKUWA WATUMWA JAPO WA teknolojia tu.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,291
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,291 2,000
Mkuu Pascal Mayalla mimi wamenitumia ujumbe sms sijui wamepata wapi namba yangu ya simu nawsiliana na wakili wangu aangalie uwezekano wa kuwashitaki ha ha ha ha ha.
Mkuu Ngongo, hiyo sms nimetuma mimi kupitia database ya kampuni ya Push Mobile. Ni kweli imekuja bila ridhaa yako, huwezi kupata legal basis ya kuwashitaki kwa sababu
  1. Haionyeshi ilipotoka, utamshitaki nani?.
  2. The motive behind hiyo sms ni "public information"
  3. Imetumwa in "good faith"
  4. Imetumia "good word" not abusive language!.
  5. Ingawa pia imetumia "enticing words" "kupata zawadi, ni true, waliokuja wamepata zawadi!.
  6. Ili kupata basis ya kushitaki, mlolongo ni mrefu lazima uanzie Polisi upate RB
  7. Then uende TCRA "Consumer Consulatative Comittee, u file complaint
  8. Wakiridhika malalamiko yako ni genuine, then wanakuruhusu kupeleka kesi mahakamani
  9. Huko utatakiwa na kuthibitisha kuwa wewe umeathiriwa na hiyo sms na ku quotify madhara into monetary terms
  10. Hiyo ni kesi ya madai sio ya jinai, hivyo mimi nitakuacha wewe uingie gharama zote, tena nakushauri uwatumie Mkono and Co. Advocates fee yao ni US $ 5000 per hour!, utashinda kesi na mimi nitatakiwa kukulipa fidia! nikishindwa nafilisiwa!, nitakupali kufilisiwa, naishi nyumba ya kupanga zile appartments za nyumba vitatu uswazi, fanicha zote ni za wife, kupitia tin number yangu, I own just an old motabike iliyopaki hapo kibarazani kwangu!, that is all you'll get!.

Nakushauri Mkuu Ngongo, wewe njoo tuu maonyesho ujionee, mwisho ni leo!.
P.
 

Forum statistics

Threads 1,390,094
Members 528,090
Posts 34,042,706
Top