Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Shukran akhuy kwa maelezo yaliyonyooka.
 
Mkuu huu mjadala ndio umemaliza hapa, asiyetaka kuelewa na asielewe tena.
 
kabla ya biblia na quran hakukuwa na yehova wala allah
nafikiri umenielewa
Nyabhingi! Najua unayo Hoja; lakini presentation yako inawaacha watu njia panda-Unashambulia badala ya kudadavua shari ilianzia wapi;Mchango wako waweza kuwa mzuri sana! jaribu kubadilisha uwasilishaji wako wa mada ili wengi wafaidike na wajue wapi pakuanzia kujibu hoja zako mkuu.(Unashambulia kama vile unaharaka ya kumaliza mjadala kimabavu)
kabla ya Biblia na quran hakukuwa na Yehova wala Allah!
Yesu kuwa na birthday mbili!
Biblia ni Plagiarism from the Egyptian book of the dead!
Hoja zako zote hizo zinamajibu,najua pia unalifahamu hilo.
Lakini pia mtindo wako wa kunukuu maandiko kwa mstari husika pekee;bila kuanzia Mwanzo wa sura husika kunafanya hoja zako zipwaye! Naamini ukirefresh katika hayo tutafaidika sana Kiongozi.
Asante.
 
nani kakwambia mimi nashindana wewe mdingi?
natoa elimu kwa watumwa wa akili kama nyinyi
kamuulize padri wako inakuwaje yesu anakuwa na bithday mbili
Nikikwambia unakurupuka unabisha...
Mimi sina padri kwani mi si mkristo.
Na hakuna elimu inayotolewa kwa kejeli
 
allah alishindwa nini kuwaambia ukweli kuwa jua halizami kwenye bwawa isipokuwa dunia ndio huzunguka?
na mohamed amesapoti hili la kuzama kwenye bwawa katika hadith;sunan abu 3991
kwa vile umejitolea kutupa dahwa naomba tuelezee kuhusu hizi aya;
quran 88:20 (earth is flat)
quran 65:12 (there are 7 earths)
quran 36:38-40 (the sun and moon chase one another)
quran 22:65 (the sky would fall if allah didn't hold it up)
quran 31:31 (ships sailing through the sea is a miracle by allah)
quran 9:29 (violently subjugate christians and jews)
 
nakuelewa ila kuhusu kudadavua hayo yote nilishaanzishaga nyuzi kuhusu yote uliyoeleza,zitafute humu na debate utaziona
njia yangu ya uwasilishaji ni sahihi ukizingatia sumu walizonazo watu weusi tokea wamezaliwa
my harsh approach inalenga kumtia mtu hasira ili akafanye research na hapo dipo atakapokutana na ukweli
sorry to say kuwa approach hii ndio sahihi kwa wakati huu,time is running out na watu wanatoa zaka kila siku huku taifa likiendelea kuwa masikini
 
Nikikwambia unakurupuka unabisha...
Mimi sina padri kwani mi si mkristo.
Na hakuna elimu inayotolewa kwa kejeli
kejeli itakufanya ukafanye utafiti
hii ndio approach sahihi
stop being sensitive,debate zinahitaji kuwa na ngozi ngumu
 
kejeli itakufanya ukafanye utafiti
hii ndio approach sahihi
stop being sensitive,debate zinahitaji kuwa na ngozi ngumu
Wewe unafanya debate gani humu zaidi ya kushambulia na kukimbia?
 
Wewe unafanya debate gani humu zaidi ya kushambulia na kukimbia?
kwa vile umesema wewe sio mkristo na hujui chochote kuhusu biblia basi lile swali kuhusu birth day ya yesu hatuwezi kudebate
 
kwa vile umesema wewe sio mkristo na hujui chochote kuhusu biblia basi lile swali kuhusu birth day ya yesu hatuwezi kudebate
Kuna sehemu nimezungumzia kuwa mimi ni imani fulani au sio imani fulani? Wewe utakuwa umejichanganya,na kama ni hivyo inakuwaje wewe ambaye wewe sio mkristo wala muislamu ila ujadili Qur'an na Biblia?
 
Kuna sehemu nimezungumzia kuwa mimi ni imani fulani au sio imani fulani? Wewe utakuwa umejichanganya,na kama ni hivyo inakuwaje wewe ambaye wewe sio mkristo wala muislamu ila ujadili Qur'an na Biblia?
sababu quran na biblia nazijua na nina uwezo wa kuchallenge maandiko yake
 
Wow, walau sasa umetanua mjadara; hiki kitabu nani mwandishi? Hope hiki ndio kitabu cha kipagani and hence, kikitofautiana na Biblia haliwezi kua jambo la ajabu and again, kukifanyia reference kwa mambo ya Mungu, linabaki kua suala la HIYARI la mtu but Mkristo wa kweli sidhani kama anaweza kukifanya kua kitabu chake cha reference when it comes kutaka kujua mambo ya Mungu!
Kuhusu issue ya Midian na Ethiopia kwenye hicho kitabu chako, je kuna mtu anaweza kunambia Midian ndio wapi leo!? Maanake ni kweli kwamba Biblia imesema Musa alikimbilia Midian, but who can tell me where is Median kwasasa!? Nchi ya Ethiopia na Misri ndizo nchi zinazo tajwa katika Africa, I suppose hizi ni nchi za siku nyingi sana, Misri walau haijabadiri jina la nchi vizazi na vizazi since Enzi za Nabii Ibrahim (Musa akiwa hata hafikiriwi) lakini Ethiopia mara iitwe Kushi, mara sijui jina gani, so kwenye hilo la kutofautiana kwa Biblia na hicho kitabu kuhusu alikokimbilia Musa, I'm still speechless cause I don't know Median ndio wapi sasa hvi!?
 
Lakini huoni hii ina maanisha mmoja kafoji?? Sasa swali linakuja (offcourse inahitaji uzi wake) je nani mkweli na nani muongo??
Kuhusu nani Muongo na nani mkweli, please naomba kwa heshima yako nisitoe jibu, tutagombana na wachangiaji wengine and hence maana ya UZI wako itaharibika, tuendelee na mjadara brother!
 
sababu quran na biblia nazijua na nina uwezo wa kuchallenge maandiko yake
Unazijua kwa maana ipi? maana kwa uelewa wangu mtu kusema anavijua hivyo vitabu maana yake ana elimu ya hivyo vitabu.
 
Bismillah Raham rahim

Nimepeda hoja zako maana ntawafungua wengi narudia kusema mnapotosha au mnasumbuliwa tafsiri na uzuri wa Quran bado ipo kwenye lugha halisi so kabla kuja huku ni vema ukawa unajiridhisha kwanza vyuo vikuu vikubwa ulimwengu wana vitengo vya utafiti qa kisayansi kupitia Quran.

Qur 88:20: surat Ghashisyia Allah anauliza " Na jins gani tulivyoitandaza Ardhi?"
Ukisoma tafsiri ya kingereza inasema "And at the Earth, how it is spread out?"
Kiarabu inasomeka "Wa-ila li-Ardhi- kaifa sutihat?"
Neno Ardhi kiarabu linamaana mbili ya earth na ardhi kama sisi tunapotumia lakin huwez kutumia neno land wakati unazungumzia earth unamaamisha had eneo la bahari bahari imekaa juu ya ardh...sasa unakiwa unatafsir unangaalia neno hilo linatumika wakati gani na minajili gani mfano aya hiyo ilikuwa ipo kwenye mtiririko wa Allah kuhoji kuhusu mbingu zilivyo,akaja milima na ndio akaja ardh so ulipaswa uchukue maana inayoendana na zipo aya nyingi sana za hivyo ndan ya Quran

Neno zuri lilalofaa hapo ni earth kwa luhha ya kijografia earth pia hutumika kama ardhi.
Lakin kumbuka kuwa Quran ndio ilikuja kutoa tafsir bora kabisa ya umbo la dunia pale Allah alipisema katika surat naziiat 79:30 inasema " "We have made the earth Egg- shape" kiarabu inasoma "Walbada dhalika ardh daha-ha" kama nilivyojueleza kule juu hapa ardh imetumika kama Earth ya dunia Allah akosema tumeumba dunia kwa umbo la Yai...neno Dahaha limetoka kwemye mzizi neno la kiarabu "Duria" likiwa linamaana Ya ndege mbuni so Allha alimaanisha umbo la dunia yetu ni kama yai la mbuni...na leo wansayansi wanakunbalina kiwa dunia yetu yaipo complete round ila ipo spherical shape kama imebonyea juu na chin na kati kati ipo round nadhan unajua nilichosema na ndivyo yai la mbuni lilivyo.!

Hoja yako ya pili ni kule quran 65:12

It is Allah who has created seven heavens and of the earth, the like of them. [His] command descends among them so you may know that Allah is over all things competent and that Allah has encompassed all things in knowledge.

Kama unapoona hapo Allah anazungumzia kuumba mbigu saba sawa sawa na ardhi akiwa na maana ya matabaka saba ya ardh na matabaka saba ya mbingu kitu amacho leo sayans inakikubali kuwa ardh yet ina matabaka saba na pia mbingu zetu zina matabaka saba.


Hoja yako nyingine hii ya Quran 36:38-40 katika sirut yaasin hapa kuna miujiza mikubwa ambayo kupitia aya hii huenda ukaona Allah alivyokuu na ukaamin uwepo wake inasema


36:38
And the sun runs [on course] toward its stopping point. That is the determination of the Exalted in Might, the Knowing.

36:39
And the moon - We have determined for it phases, until it returns [appearing] like the old date stalk.

36:40
It is not allowable for the sun to reach the moon, nor does the night overtake the day, but each, in an orbit, is swimming

Hapa Allah kasema jambo kubwa amabli wengi wetu tulipokuwa shule tulipotoshwa kuwa jua lipo tu limetulia lakin dunua ndui inakizuguka lakin Quran imesema Jua nalo linazunguka kwemye obirt yake leo sayans baada ya kua adadvance inasema jua huchukua siku 26 kukamilisha mzuguke wake wanauita black dot.
Na hakuna sehem kumeandikwa mwez na jua vinakimbizana ila imeandikwa kila kimoja kinaelea kwenye njia yake usije kusema kinaogelea n hapo inakuambia haruhisiwa jua kukutana kila kimoja kipo kwenye njia yake...

Jiulize Muhhamad angeyajua vip haya kama sio kwa yule aliyeviumba hivyo vitu

Hoja yako ya Quran 22:65 surati hajj hapa allha anazungumzia power yake sio kwamba ameshikilia kwa mikono kuwa kila kitu kinachoendelea ulimwenguni au kilichopo kipo kwa vile yeye anataka na vipo wanasayans wameits Law of principle... Aya yenyewe inasema hivyi

Do you not see that Allah has subjected to you whatever is on the earth and the ships which run through the sea by His command? And He restrains the sky from falling upon the earth, unless by His permission. Indeed Allah, to the people, is Kind and Merciful.

Nadhan unaona mwenyewe bapo Allah anafafanua kuwa mbigu zipo zinaelea hazijashikwa na kitu na wala hazina nguzo ni kwa amri yake zipo hivyo zilivyo

Hoja yako ya Quran 31:31 surat Luqman Allha kwenye Quran amekuwa akikumbusha watu mara kwa mara juu Neema alizowandalia wanadamu ili wawezw kuish na kufanya mambo yao ili waweze kumtambua Mola wao neno llilitumuka pale sio miujiza ila ni ishara na ndio maana kasema hizo ni katika favor zake kwa wanadamu ambao walioaswa kushukuru kuoitia bahari wanasafiri na kupata chakula na mali so anakumbusha kama kawaida juu ya watu kutizama vitu na kumshukuruku yeye aya yenyewe inasema hivi


Do you not see that ships sail through the sea by the favor of Allah that He may show you of His signs? Indeed in that are signs for everyone patient and grateful.

Hoja yako ya mwisho Quran 9:29 surat Tawbah hii ni aya namba moja kwa kupotoshwa kwenye Quran na wanaitumia sana wanaoupinga islam sababu wanachikifanya wananyofoa aya moja halafu wanaisambaza

Surah hii ileteremka wakati wa vita na katika surah hii Allah anampa maelekezo Muhamahad juu ya vita hiyo kabla kufika kwenye aya hiyo inayopotosha Allah anamumbia Muhham piganeni katika njia ya Allah msiwauwe wanawake na watoto, walemavu na wagonjwa, msiharibu vyanzo vya maji na wala msikate miti, kisha akasema piganeni na wale tu wanaotaka kupigana na nyie na mstari unapotoshwa ndio unafatia
Fight those who do not believe in Allah or in the Last Day and who do not consider unlawful what Allah and His Messenger have made unlawful and who do not adopt the religion of truth from those who were given the Scripture - [fight] until they give the jizyah willingly while they are humbled

Lakin baada ya Aya hii inasema kama watahitaji suluhu fanyan hivyo haraka na pia muwasindikize kwenye sehem salama..

Nakushauri ukasome mwenyewe kuanzja aya ya kwanza acha kuchomoa chomoa aya moja mija ba kuzipotosha au kushindwa kuzitafsiri sawa uzuri wa kitabu chetu lugha yake ya asiki bado ipo kama tafsiri haijajitoshelza tunarud kwenye lugha yenyewe.!

Allah amesema Hichi ni kitabu kisicho na shaka ndani yake na pia kasema kama mnasema muhamad katunga hii Quran basi leten mfano wake.!

Wabilah Tawfiq
 
nani kakwambia mimi nashindana wewe mdingi?
natoa elimu kwa watumwa wa akili kama nyinyi
kamuulize padri wako inakuwaje yesu anakuwa na bithday mbili
Nadandia UGOMVI wenu though sijasoma huko juu mmeanzia wapi na huyo "mgomvi" mwenzio. The truth is, Chrismas pamoja na kusherehekewa na Wakristo wengi but still sio siku aliozaliwa Yesu, hiyo tarehe 25 December ni tarehe ya kutungwa, huyo unae bishana nae wala hana sababu hata ya kwenda kumuuliza Padri wake, hiyo tarehe kwenye Biblia haipo, ilitungwa tu, sasa kama ni vyema kutunga tarehe ni sawa au sio sawa, huo unabaki kua mjadara mwingine. Sijui kama nimedandia train kwa mbele na kufanikiwa kuendelea na safari!?
 
Mkuu, kuna uhusiano wowote wa hiki tunacho changia na huo ushauri wako!? Sijasema kama ushauri ni mbaya au mzuri, ila nahisi kama hauna uhusiano na hiki tunacho jadiri. Nadhani ungefungua UZI special kwa hilo then tutachangia huko!
 
Kuna sehemu nimezungumzia kuwa mimi ni imani fulani au sio imani fulani? Wewe utakuwa umejichanganya,na kama ni hivyo inakuwaje wewe ambaye wewe sio mkristo wala muislamu ila ujadili Qur'an na Biblia?
Nimemwambia anakurupuka kabisha. Mimi kanibandika ukristo nikamjibu kuwa hiyo si dini yangu. Sasa hivi kahamia kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…