Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,510
- 28,417
- Thread starter
- #21
Ni kweli kabisa mkuu....haya maelezo yameegemea zaidi zile ngano za kwenye biblia ,sidhani kama Quran na vitabu vya iman zingine vina story hizi mkuu
...my point is_una uhakika gani kama hizi story za biblia ndio sahihi kumuelezea Mungu wa kweli na kuona story za tamaduni zingine kama ni za Miungu,Mizimu,Mapepo etc
......sidhani kama wasio wakristo wataelewa hizi mambo unazoeleza hapa mkuu....nafikiri hizi zilifaa zaidi kuelezea kanisani coz uhakika wake pia ni questionable kwa watu wasio amini biblia ambao ni wengi tu
Ndio maana stori hii inasadifu kichwa chake cha habari, kwamba ni masimulizi ya Biblia kwa jicho jingine.
Nakubaliana na wewe kuwa dini nyingine nazo zina versions zao, lakini kujifunza mambo ya wengine ni jambo jema pia ili kupanua ufahamu na kuelewa yale ambayo ulikuwa huyajui.
Mimi Quran naisoma pia mkuu, lakini sijapata wasaa wa kuichambua kwa upana, ila nikipata nitaichambua pia.
Ila kama kuna mtu pia anafahamu historia ya dunia kwa jicho la Quran au dini yoyote au kitabu chochote anaweza kuileta hapa, ila cha msingi tu mjadala usianze kuwa wa kidini na kuaza sarakasi za kidini tulizozoea humu JF....