Biblia kwa Jicho Jingine

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,511
28,412
Nimeamua kuandika makala hii kwa heshima ya Jukwaa hili lakini pia kwa ajili ya kuchochea udadisi lengo likiwa kumpa kila asomaye uthubutu wa kutaka kufukiri nje ya Box.

Makala hii ni mjumuisho wa vitabu vingi vya kiroho kikubwa kikiwa Biblia, Simulizi za Kiyahudi, Vitabu vya Mafunuo ambavyo baadhi ya walioishi duniani walibahatika kuyapata kutoka wa Mungu mwenyewe lakini pia baadhi ya mawazo yangu ili kuweka mtoririko mzuri wa kimakala.

Makala hii huenda ikapingana na unachokiamini, lakini chanzo cha fikra mpya hujengwa katika tofauti ya kimitazamo, na hapo ndipo mwanadamu hukua kimawazo, kwa hiyo ukiona yaliyomo humu yanapingana na uelewa wako ni vema uachukulia tu kama masimulizi ya hadithi za kufikirika, maana lengo la uzi huu si kuchafua au kuvuruga imani ya mtu yeyote.


==========

Hapo mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na nchi nayo nchi ilikuwa giza tena utupu.

SEHEMU YA KWANZA(UTANGULIZI)

Hapo zamani sana kabla ya mwanzo wa kila kitu alikuwepo Mungu pekee bila kiumbe chochote kile kilicho hai wala kilicho mfu, Mungu huyu kwa utashi wake kabisa na kwa mapenzi yake kabisa bila kushurutishwa na yeyote akaamua kujipanua kwa “kuuwekeza utu(uhai) wake” ndani ya vitu vingine ili tu kutimiza yale ambaye yeye aliyaona yanaifurahisha nafsi yake.

Mungu huyu aliamua kujigawa katika vipande vikubwa vitatu ambavyo vyote vilibeba Uungu wake kwa ukamilifu wa 100%, vipande ambavyo vingemuwezesha yeye kwanza kutekeleza tukio zito lililokuwa mbele yake, lakini pili kurahisisha kile ambacho anataka kwenda kukifanya kwa kuwa kwa vyovyote vile kwa hulka yake alitaka kuugawa uhai wake(kuusambaza) kwa viumbe vyake atakavyoviumba lakini pia kuwa navyo karibu kama familia moja.

Viumbe hivi kwa vyovyote vile visingeweza kumuelewa na wala haviwezi kumuelewa milele yeye ni nani, kifupi vinaelewa kile tu ambacho ameruhusu kieleweke kwao kwa wakati huo, pamoja na hilo bado hivyo alivyoviruhusu vieleweke vimekuwa “hekima nzito kweli kweli” , hekima ambayo imeviharibu viumbe hivyo vilivyoamua kuitumia vibaya uelewa mdogo waliopewa kuibeba si wa malaika wala wanadamu wala kwa viumbe vyote vya rohoni alivyoamua kuviumba.

Kwa msingi huu Mungu huyu akaamua kufanya kazi katika nafsi tatu, ya kwanza akaiita Mungu Baba(Mungu Mwenyezi), ya pili akaiita Neno(baadaye alivaa mwili ili aje duniani kama mwanadamu) na ya tatu Roho baadaye alikuja kufahamika kama Roho Mtakatifu huku duniani.

Kimsingi nafsi hizi tatu zina nguvu kubwa sana na imekuwa vigumu sana kwa viumbe vyote vya rohoni na vya mwilini kujua hasa tofauti yao ni ipi na nani ni nani , lakini majukumu yao yamegawanyika kiutendaji zaidi, huku nafsi hizi tatu zikibaki kubeba Uungu wao kwa 100%.

Kifupi unayedhani ni Mungu Baba saa nyingine unakuta siye yeye ila ni Neno, na unayedhani ni Neno sometimes siye yeye ila Roho na unayedhani ni Roho saa nyingine siye ila ni Mungu Mwenyezi mwenyewe kwa kuwa kila mmoja ni tofauti na mwenzake na wakati huo kila mmoja yumo ndani ya mwezake, wote hawa ni nafsi tatu tofauti kabisa zinazojitegemea lakini pia nafsi hizi tatu ni moja.

Mungu Mwenyezi huyu yeye akaamua kuchukua jukumu kama la msimamizi mkuu na Master Planner wa kila kitu kinachoendelea huko kwenye mbingu za juu sana, mbingu tunazozijua sisi na hapa duniani, ni kama Senior Planner na administrator wa kila kitu. Yeye ndiye mpangaji au designer, muandaa maono na senior Founder.

Neno yeye akachukua jukumu la kutekeleza maono yote yanayotoka kwa Mungu Mweyezi, yeye ndiye hasa fundi wa kutafsiri maono na mipango kutoka kwa kwa Mungu Mwenyezi na kuuingiza katika utekelezaji ili vyote vilivyopangwa kugeuka kuwa vitu tangible, lakini pia kunapotokea failure kama iliyotokea kwa Adam na mkewe bustanini Edeni, failure ambayo inatokana na design nzuri kabisa ya kukipa kila kiumbe chake uhuru wa kuishi maisha ya kuwa na utashi akichagua anachotaka na asichotaka bila kushurutishwa na yeyote basi Neno huja na kurekebisha kasoro hio kwa kufuata design kutoka kwa Mungu Mwenyezi.

Kifupi Neno huyu ndiye mwenye jukumu la kurekebisha kasoro hio na ndio maana maandiko yanasema “alichinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya nchi kwa kosa la Adam na mkewe Hawa” Roho yeye akabeba jukumu la uwezeshaji, yeye ndiye supplier wa nguvu na uwezo na materials za kiroho kuhakikisha kuwa plan zote kutoka kwa Mungu Mwenyezi, na utekelezaji wake kutoka kwa Neno unafanya kazi kama ilivyopangwa.

Yeye ndiye mwenye jukumu hasa la kuhakikisha kila kitu kinakuwa maintained katika viwango vyake kama ambavyo Master Plan inavyosema, lakini yeye pia ndiye msimamizi mkuu wa Uungu katika viumbe vyote vilivyoumbwa na vitakavyoumbwa.

Kabla ya Neno kuja kuanza kazi yake, Roho huyu hutangulia kwanza na kuyaaandaa mazingira, na mara baada ya Neno kumaliza kazi zake kama mtekelezaji, Roho hukabidhiwa jukumu pia la kuiendeleza kazi iliyofanywa na Neno lakini pia kuhakikisha kuwa quality na standards zake zinafikia Master Plan kama ilivyopangwa na Mungu Mwenyezi.

Kumbuka hawa watatu ni wamoja na ni tofauti pia, wakati unadhani sasa yuko Neno anafanya kazi, kumbe siye ila ni Roho na wakati unadhani ni Roho anafanya kazi unakuta ni Mwenyezi mwenyewe na wakati unadhani ni Mwenyezi yuko kazini kumbe ni Roho au ni Neno yuko kazini. Biblia inasema Mungu[Jehova] kwa Neno lake[Neno] aliziumba mbingu na nchi na kwa Hekima yake[Roho] akazithibitisha(zikawa maintained).

Kazi ya uumbaji ilipoanza, Mungu Baba akaandaa Master Plan master, Plan hii ikaanza utekelezaji wake awamu kwa awamu kwa kadri alivyoona yeye kuwa inafaa kwa nyakati atakazoziweka yeye na kwa namna atakavyoamua yeye.

Umbaji huu uligawanyika katika vipande viwili (Spheres Mbili)
Uumbaji wa kwanza ulikuwa uumbaji wa viumbe vya Kiroho na uumbaji wa Pili ulikuwa uumbaji wa viumbe vya kimwili, pia Mungu akaamua kuweka baadhi ya viumbe vya kiroho na kimwili kusimamia kazi zake za uumbaji, kusimamia mifumo yake ya Kiuungu, kusimamia tabia na makuzi ya viumbe vya kiroho lakini pia akatoa wasaidizi chini ya kila aliyepewa jukumu la kusimamia.

Sphere za Kiroho
Katika uumbaji wa Sphere za Kiroho kuna spheres ndogo ndogo nyingi sana huenda zikawa mabilioni kwa sasa kwa uwa kazi ya uumbaji inaendelea na ni ya milele na milele.
Spheres hizi zina vipande vitatu,
• Kipande cha ndani kabisa
• Kipande cha katikati
• Kipande cha Nje

Kipande cha ndani kabisa ambacho wengi tunakifahamu kama Mbingu ya Mwenyezi Mungu, Mbingu hii ndipo mahali ambapo kiti cha enzi cha Mungu kipo na ndio hasa headquarter ya uumbaji wote maana ndiko ambako Mungu yupo.

Muundo wa kipande hiki au Mbingu hii umegawanyika pia katika sehemu kuu tatu.
1) Ya Kwanza ni sehemu ya Uungu inayoanza kwa Kiti cha Enzi cha Mungu kilicho upande wa Kaskazini wa Mbingu, kiti hiki kiko juu ya kila kitu kwa maana ya height na hakuna kitu kinachoruhusiwa kukaa nyuma yake, kiti hiki kimezungukwa na viumbe vinne vyenye uhai ambavyo vimejaa hekima na ukuu na utiisho wa ajabu kwa sababu ya kuwa karibu na Mungu muda wote na viumbe hivi vina act kama waangalizi wa kiti hiki lakini pia Uungu wa Mungu.

Mara baada ya kiti hiki cha Enzi kuna Sehemu ya Roho ambazo zinasimamia tabia kuu za Mungu ambazo ni 1) Amani , 2) Upendo, 3) Utukufu mkuu, 4)Nguvu , 5)Uzima, 6 )Hekima ,7) rehema. Baada ya hapo kuna uwazi mkubwa sana kama bahari ya kioo na mbele yake kuna wazee 24 ambao nao wako katika sehemu ya Uungu wa Mungu, hawa ni kama “baraza” la Umungu, kumi na wawili wakiwa mkono wa kuume wa Mungu na Kumi na wawili wakiwa mkono wa Kushoto wa Mungu.

2) Sehemu ya Pili ni sehemu ya ibada ya Uungu ambapo kuna madhabahu ya dhahabu ya kutoa uvumba, madhabahu hii iko pembei kidogo mara baada ya kutoka kwenye viti vya wazee 24. Hapa ndipo ambapo sala zote na dua zote na shukrani zote za wanadamu na viumbe vyote aivyoviumba Mungu hupelekwa na kufukizwa kama harufu ya manukato kwa Mungu, harufu hii kupelekwa moja kwa moja kwa Mungu mwenyewe kwenye kiti che enzi bila kiumbe yeyote kugusa maana hii ni haki ya Mungu pekee.

Katika sehemu hii ya pili pia mbele ya kiti cha enzi husimama malaika wakuu 7 wa Mungu ambao huutazama uso wa Mungu daima wakipokea amri za kutekeleza kulingana na jukumu la kila mmoja alilopangiwa, majukumu haya yanahusisha control ya galaxies zote ambazo zinakadiriwa kuwa zaidi ya Bilions, usimamizi wa Mifumo ya Uungu na utawala na majukumu mengineo kulingana na nyakati na ratiba ya Mungu. Sehemu hii ya pili pia ni sehemu ya kila kiumbe ambacho kinataka kuwa na audience na Mungu awe ni malaika au viumbe vya rohoni au Adam enzi hajaanguka au yeyote anayetaka kujihudhurisha mbele za Mungu hapa anaruhusiwa kusimama na kuonana na Mungu moja kwa moja bila urasimu wowote.

3) Sehemu ya tatu ni sehemu kama ”mji” au city center ambapo kuna shuguli mbali mbali zinaendelea za kiofisi lakini pia za kimakazi kwa baadhi ya viumbe ambavyo vimepata nafasi ya kuishi mbinguni moja kwa moja kulingana na level yao ya ukuaji wa kiroho. Hii ni sehemu iliyo busy sana na iliyo na “kelele nyingi” kila “mtu” akiwa na lake, ikiwa ni sehemu ya kuingia na kutoa na pilika pilika za kutosha kila mmoja akifanya lililompeleka makao makuu. Kuna idara nyingi sana katika eneo hili ikwemo idara ya sifa, idara ya uumbaji, idara ya vita, idara inayohusika na wanadamu, idara za hukumu na mipangilio mingine mingi.

Kama nilivyosema kuna makazi huko mbinguni ya viumbe alivyoviumba Mungu, haya si makazi ambayo Yesu aliyaahidi kwa wafuasi wake, na ni wenye Uungu tu waio na makazi mbinguni lakini kila kiumbe kingine kina makazi yake, Mungu tu ndiye anayeishi na kukaa kwenye kiti chake cha enzi. Hili Nitalielezea kwa mapana nikifika kwenye kipengele cha malaika na maisha ya malaika.

Katika spheres za kiroho kitu kinachitukuzwa sana ni Nuru au mwangaza wa utukufu, kwa maana kuwa ukuu wa kitu unaakisiwa na kiwango cha Nuru uliyo nayo, kuna viumbe vina nuru kubwa sana vingine vinayo ndogo, ukuu wa nuru unategemeana na ukaribu wako na Mungu lakini pia dimension ya ukomavu wako wa kiroho na viwango vyako vya rohoni.

Mara baada ya kipande cha Ndani kuna kipande cha kati kati ambacho ni kipande kilichotengwa maalumu kwa ajili ya makuzi ya kiroho, makuzi haya hutegemea na kusudi ambalo Mungu amemuumba kiumbe wake, wapo walioumbwa kuwa wakuu wa usimizi wa vitengo mbali mbali, wapo walioumbwa kuwa wakuu wasaidizi, wapo walioumbwa kuwa “raia wa kawaida” na kadhalika. Sphere hizi za kati kazi ni nyingi sana na hupokea viumbe vinavyokuwa na kukuwa kiroho kila siku, makuzi ya kiroho hayadhihiriki katika umri ila katika kiwango cha nuru uliyo nayo katika ulimwengu wa roho.

Nje kabisa ya spheres hizi za kiroho kuna sphere yenye maisha ya kawaida ya viumbe vya Mungu ambavyo aliviumba, hapa ndipo mwanzo wa kila kitu alichokiumba, hapa ndipo akila kilichoumbwa kwa dimension yake kinakaa, wanadamu kwa dimension yao na spheres zao, malaika kwa dimension yao na spheres zao, viumbe vingine pia vya rohoni vina dimension yao na spheres zao vile vile na kila kimoja kikiwa kinaishi bila kukiingilia kingine wala kukibugudhi kingine kwa mipaka aliyioweka Mungu kwa hekima yake.

Katika sphere hizi ikitokea mfano malaika akataka kuingia katika sphere ya wanadamu itambidi ajibadilishe awe kama wao kwa kuvaa umbo lao vinginevyo hataonekana nao. Vile vile ikitokea mwanadamu akataka kuingia kwenye dimension ya malaika inabidi avue mwili avae roho vinginevyo malaika hawana uwezo wa kui nterract nao na kuna portal maalumu za kuingilia si kuvamia vamia tu. Ikitokea umechakachua na ukaingia kwenye sphere isiyokuhusu kwako ni kosa na unatakiwa kuhukumiwa, na Hiki ndicho kisa hasa cha wale malaika 200 waliovaa miili wakaja kuishi na wanadmu wakasababisha dunia kuchafuka kwa maasi yaliyopelekea gharika.

Spheres za Kimwili
Mara baada ya spheres za kiroho kuna spehere za kimwili ambazo nazo zimegawanyika katika vipengele saba, vyote hivi ni kwa ajili ya makuzi ya kiroho na kimwili ya viumbe vya mwilini. Adamu alipopewa kuishi kwenye Bustani ya Edeni alipewa jukumu la yeye na viumbe vyake alivyokabidhiwa kukua katika sphere hizi zote saba akianzia katika sphere ya kwanza kabisa ambayo tunaiita bustani ya Edeni, bahati mbaya sana jamaa akajichanganya mapema kabisa.

Mara baada ya anguko la Lucifer iliundwa sphere nyingine inayojulikana kama sphere ya tatu au sphere ya giza au war sphere , ilichukua kama theluthi moja ya spheres zote za uumbaji wa Mungu kwa wakati huo.
Sphere hii ya giza kwa makosa ya Adam ikajitanua mpaka kwenye dunia yetu hii na kupelekea mwanadamu kuwa kiumbe mwenye Umungu na Ushetani ndani yake.

Nuru na giza vikawa ndani yake matokeao yake maisha yake yakawa ni mapambano na mahangaiko ya wema na ubaya vikiishi kwa pamoja ndani ya mtu mmoja kila kimoja kikishindaba kuvutia upande wake.
Juu ya dunia tunayoishi kwa sasa kuna sphere za nuru nne ambazo wengi wa wanadamu wanaokaribia kufa huziona na huona kama vile wanapita katika tunnel ya mwanga au njia Fulani ndefu sana ya mwanga tupu na kuelekea huko kwenye spheres za juu.

Wengi waliopata nafasi ya kufika kwenye sphere hizo za juu ya dunia walidhani wameishaingia mbinguni, na mara nyingi spheres hizo za nuru za juu ya dunia huwa zina ufanano na dunia hii isipokuwa zinakuwa ziko perfect sana na hazijachakachuka na giza kama tulilonalo huku, wengi wanaoingia hapo hupaita paradiso, lakini kimsingi hata paradiso yenyewe bado.

Chini pia ya dunia kuna spheres mbili za giza moja ikiwa ni giza tupu lililosheheni ushetani wa hali ya juu ambapo waovu wa dunia hii huenda kuchukua nguvu za giza kuja kuiharibu dunia, ni shemeu ambapo mapepo mengi sana yanapatikana na roho za wandamu waliokufa katika giza hugeuzwa kuwa maajenti wa kuzimu kuja kuvuruga maisha huku duniani, na hapa ndipo kuna kitu kinaziliwa kinaitwa majeshi ya wafu, vibwengo, vinyamkera , aliens na mengineyo.

Chini kabisa kuna sphere moja iliyo na giza kuu ambalo ndipo Lucifer mwenyewe yupo anaishi, huko ndiko kuzimu hasa ambapo ni makao makuu ya uovu wote kukisheheni hekima yote ya kishetani na viwanda vikubwa vya uharibifu na ubunifu wa kila namna lengo likiwa ni moja tu kumkomoa Mungu na viumbe vyake.
Nitaizungumzia Kuzimu kwa mapana yake baadaye mara baada ya kuwachambua malaika na maisha yao kwa upana wake.

Kabla ya hapo tuyazungumzie maisha ya ulimwengu wa kiroho kabla ya kuumbwa kwa dunia yetu, maisha yanayojumusiha pia uasi na anguko la Lucifer.

Sehemu ya Pili itafuata soon…
 
SEHEMU YA PILI

Kwa miaka trilioni na trilioni mambo yalikwenda vizuri kabisa katika ulimwengu wa roho na spheres zake.
Kila kitu kiliishi kwa kufuata mifumo na mipaka aliyoiweka Mungu kuruhusu baadhi ya viumbe vilivyokuwa na juhudi ya kukua kiroho kuendelea kukua na kuimarika.

Kwa muktadha huo Uliwengu wa roho ulikuwa ni kama mmoja usio na matabaka matabaka zaidi ya ile miundo aliyoiumba Mungu kwa design yake.

Kwa ujumla wake ulimwengu wa kroho na kimwili uligawanyika katika maeneo makuu matatu.

Eneo la kwanza lilijulikana kama Pristine Universe, eneo la pili lilijulikana kama Boundary Universe na eneo la tatu lilijulikana kama Raw Universe.

Pristine Universe lilikuwa hasa ni eneo ambalo uumbaji ulikuwa umeshafanyika na kugawanyika kwa kadiri Mungu alivyoona inafaa kwa kufuata dimensions mbalimbali za kiuumbaji.

Boundary Universe hili lilikuwa ni eneo "tupu" au vacuum ambalo halikuwa na roho wa mwili wowote unaoishi huko, ni eneo ambalo lilikuwa kama uwanja usiojengwa au shamba lisilolimwa linalotegemea soon kulimwa pindi mwenye shamba atakapoamua kupanua mashamba yake. Katika Boundary Universe hakuna kiumbe chochote kingeweza kuishi iwe ni maaika au viumbe vingine vya kiwmili au kiroho isipokuwa Mungu pekee na baadhi ya malaika waliopewa kulitunza eneo hilo na kuliandaa kwa ajili ya uumbaji utakao tokea, kila aliyejaribu kuingia eneo hili alipoteza uhai mora moja.

Raw Univese hili lilikuwa ni eneo a uumbaji ambapo Mungu alikuwa analitumia kama karakana au kiwanda cha ya uumbaji, eneo hili lilitawaliwa na giza na kila kilichoumbwa na kikasubiri kuzinduliwa rasmi kwa nyakati zilizoamuliwa na Mungu mwenyewe kiliwekwa huko. Ni Mungu pekee na wasaidizi wake maalumu wa sekta ya uumbaji waliokuwa na access na eneo hilo.

Sasa basi Mungu alipoanza kuumba aliumba viumbe mbali mbali na vingi sana vya rohoni kwa mapana yake wa kwanza kwanza wakiwa wazee ishirini na nne na baadaye wakafuatia malaika wa ibada(worshiping angels), kwa kuwa jukumu la kila kiumbe lilikuwa kumuabudu Mungu.

Baadaye wakafuata malaika wengine na viumbe vingine vingi. Ikumbukwe kuwa si kila kiumbe cha kiroho alichoumba Mungu kina Muundo kama wa binadamu, vingine vina muundo wa ajabu ajabu kama fimbo, ukienda huko mbinguni unaweza kukutana na fimbo ina macho au kiumbe kina sura ya ng'ombe na kinatimiza majukumu yake kama kawaida.

Katika malaika hao akaumba malaika wasimamizi wa galaxy mbali mbali akiwemo malaika maarufu sana kwa jina la Uryaluzzael ambaye ndiye alikuwa muangalizi wa dunia kabla Mungu hajaweka viumbe hai kuishi humu ndani.

Pia akaumba malaika wa hekima ambao walikuwa wamejaa maarifa na uwezo wa ajabu sana wa akili na ufahamu mpana sana kutoka kwa Mungu moja kwa moja wakisimamia kweli za Mungu. Mbinguni malaika wanaoheshimika sana ni malaika wa Hekima na malaika wa Upendo na malaika wa Sifa na Ibada na malaika wa Hukumu za Mungu kwa kuwa hao ndio wanaougusa moyo wa Mungu moja kwa moja.

Pia Mungu akaumba maserafi na makerubi na walioko chini yao. Katika hilo kundi hilo la Makerubi akamuumba kiumbe mmoja mzuri sana akampamba kwa kila aina ya nakshi na kila nguvu ya kiroho lakini pia akmpa kitengo nyeti sana cha kuzikusanya sifa zote za Mungu kutoka Spheres zote za kiroho na kimwili na kuzipeleka kwa Mungu moja kwa moja.

Kiumbe huyu aliitwa Lucifer, liyekuwa kerubi mzuri mwenye kupendeza kweli kweli anayejua kumsifu Mungu mpaka akafurahi, lakini pia anayejua kuzichambua sifa zinazoletwa kwa Mungu kutoka kila angle ya uumbaji ili zimfikie Mungu kwa mpangilio mzuri kabisa. Chini yake akampa malaika wengi sana wa kumsaidia kazi yake hiyo.

Katika Kundi hili la makerubi pia akamuumba malaika muhimu sana anayeitwa Melkizedeki ambaye naye alikuwa rafiki mkuu sana wa Adam, akimsaidia katika ukuaji wake wa kiroho lakini pia katika kuitawala na kuisimamia dunia kama Mungu alivyotaka. Melkizedeki huyu ndiye aliyepewa jukumu la kuilinda njia ya kwenda Bistani ya Edeni Adam alipoanguka.

Na kwa kuwa alikuwa kama guardina angel wa Adam, hata mara baada ya anguko la Adm ndiye aliyeishi naye duniani akiendelea kumsaidia mambo mbali mbali, na mara baada ya Adam Kufa akaruhusiwa kuuvaa mwili wa kawaida akawa kama mwanadamu akiishi na wanadamu kwa ruhusa ya Mungu mpaka pale Ibrahimu alipokutana naye kama Biblia inavyosema kwenye kitabu cha mwanzo.

Lucifer alikuwa malaika mwenye ngazi ya kerubi, tofauti yake na wengine ni kuwa yeye alikuwa kwenye kitengo muhimu sana cha sifa kwa Mungu, kitengo kilichompa access ya kuingia kwa Mungu moja kwa moja bila kufata protocol yoyoye.

Watu wengi hudhani mbinguni kuna Mungu na malaika tu, lakini kuna viumbe wengi sana zaidi ya malaika na generally wanajulikana huku kwetu kama “viumbe vya kiroho” lakini jina lao hasa hatujafunuliwa.

Wapo malaika waliokuwa na nguvu kubwa sana zaidi ya Lucifer hata kabla ya uasi wake, kilichompa charti shetani ni majukumu aliyokuwa nayo maana alikuwa center ya sifa kwa Mungu, na hapo ndipo hasa kwenye “moyo” wa Uungu wa Mungu wetu.

Kutokana na majukumu aliyokabidhiwa Lucifer ya kuzikusanya sifa zote na utukufu kutoka angle mbali mbali na kuzipeleka kwa Mungu na pia akapewa uwezo wa kusifu lakini alianza taratibu kuzitamani sifa zile akaziona ni zake na ana haki nazo yeye.

Tararibu moyo wake ukaanza kujiinua akaanza kujiona ni mkubwa kuliko malaika wote, miaka ilivyokwenda akajiona ni mkubwa kuliko makerubi wenzake wote, baadaye akajiona ni mkubwa kuliko malaika wote wa kitengo cha hekima baadaye kuliko wazee ishirini na nne. Miaka ilivyozidi kwenda akajiona ni mkubwa kuliko maserafi wote.

Baadaye akajiona ni mkubwa kuliko Roho wa Mungu baadaye akajiona ni mkubwa kuliko Neno na akaanza kuutamani Uungu. Mara baada ya tamaa ya Uuungu kumuingia mwanzoni akataka kuchukua nafasi ya Neno, akidhani ataweza kuwa muumbaji kama Neno.

Ni kama Mkurugenzi mkuu wa TRA akabidhiwe jukumu la kukusanya kodi zote za nchi na kuziwasilisha serikalini huku akiwa analipwa mshahara mzuri na ulinzi wa serikali na marupu rupu ya kutosha lakini taratiibu akaanza udokozi wa kodi za wananchi na kuziona kodi zote ni zake yeye kama Mkurugenzi, si za wananchi wala si za serikali, na kwa msingi huo aanze kuandaa plot ya kutaka kuchukua kiti cha Ikulu awe Rais yeye huku akisahau kuwa yeye ni mteuliwa tu wa Rais na sifa na marupurupu aliyonayo ni kwa sababu ya nafasi aliyo nayo kama mkurugenzi na yamepangwa na Rais wake.

Akaanzisha uasi akapata baadhi ya malaika na kuwatoa katika Pristine Universe kwenda kuvuka kwenye Boundary Unverse ili ajitegemee na aanishe mbingu yake na utawala wake. Kikosi kile cha jwanza kabisa cha malaika kilipovuka tu mipaka ya Boundary Universe kikateketea chote kwa kuwa huko hakuna aliyeweza kuishi zaidi ya Mungu pekee maana ndiye chanzo cha uhai wote na yeye ndiye uhai wenyewe.

Mara baada ya Lucifer kuona imeshindikana kuvuka akajipanga upya kutaka kuja na mpangowa wa pili, yaani Plan B.

Plani B ilikuwa kumpindua Mungu hapo hapo alipo kwa kiburi kuwa naye anafaa kuwa kama Mungu. Akaja na therty moja kuwa Mungu si chanzo cha nguvu zote kama wengi wanavyodhani ila amewazidi ujanja wenzio kwa kukaa mahali ambapo uhai wote unatokea yaani kiti cha enzi na kwa msingi huo yoyote yule ambaye ataweza kumtoa hapo atakuwa na uwezo kama wake.

Lakini pia akaja na wazo kuwa Mungu si kwamba ni muumbaji wa kila kitu kwa amri yake, ila ni kwa kuwa ni mambo yote yanatokea kwa sababu ya "evolution process" ambayo ni natural na Mungu ameihodhi na kujifanya kuwa yeye ndiye chanzo cha yote.

Hivyo kama malaika wakimuunga mkono akaweza kumpindua Mungu pale alipo na kuchukua nafasi yake, basi anao uwezo wa kuunda mfumo mpya kabisa wa maisha ambao hautakuwa unamtukuza "mtu" mmoja tu ambaye ni Mungu ila kila mtu atakuwa na portion ya utukufu wake, jambo ambalo lilikubalika sana kwa wenye uchu wa ukuu huko mbinguni.

Tangu kuanza kwa tamaa ya Lucifer mpaka uasi wake ilichukua miaka milioni moja ya kimbingu sawa na miaka Bilioni moja ya kidunia.

Hatimaye siku ya siku ikafika ya kufanya mapinduzi haswa haswa. Hapo ndipo kikosi maalumu kambacho hakikutarajiwa kabla kikaundwa na malaika Mikaeli ambaye mwanzoni hakuwa malaika wa vita, mwanzo alikuwa malaika anayesimamia kuwakuza viumbe vya kiroho katika spheres zote kukua katika tabia za Kimungu kama Upendo, haki, huruma na tabia nyingine za "Utu mwema" maana kila kiumbe kina dimension yake ya tabia hizi na hukua hatua kwa hatua mpaka kufika kabisa kiwango ambacho Mungu anakiona kinafaa kwa kiumbe hicho kuingia katika sphere nyingine kwa ajili ya maisha ya dimension nyingine.

Katika kuuzima uasi hule ili kuhakikisha kuwa maeneo nyeti ya ibada za kimbingu hayatiwi unajisi na Lucifer na kundi lake maaika Phanuel ambaye jukuma lake la kwanza kabla ya uasi ule lilikuwa kuutunza na kusimamia Uwepo wa Mungu na Utakatifu wake hasa maeneo ya Ibada akashirikiana na Gabriel kuhakikisha kuwa maeneo nyeti ya ibada hayanajisiwi huku Mikael akipambana moja kwa moja na Lucifer.

Vita ikapangwa Mbinguni Lucifer na malaika zake na Mikaeli na malaika zake, vita ile ilihusisha mapigano ya moja kwa moja, mapigano ya ushawishi kuhakikisha viumbe vinavutiwa kila kimoja upande mmoja lakini pia vita ya panga pangua ya Ulimwengu wa roho maana Lucifer alifanikiwa kumega theluthi moja ya ulimwengu wa roho wa Pristine Universe na kuziweka upande wake, huku Mungu akibaki na theluthi 2 ya ulimwengu huo kwa wakati huo.

Mwisho wa siku Mikaeli aliibuka mshindi akafanikiwa pia kufanya tukio la ajabu sana lililoushangaza ulimwengu wa kiroho, tukio la kukata ulimwengu wa roho wa Lucifer na kuutenga pembeni kabisa na kutengeneza mkusanyiko uliojulikana kama War Universe. Bahati mbaya sana dunia yetu na Sola Sstem yetu na Galaxy hii ikaangukia katika hio War Galaxy.

Na sababu kuu ni kuwa kulikuwa na race ya viumbe kabla ya Adam kuumbwa vilivyoishi hakika ulimwengu huu ambavyo vilikubali kushirikiana na Lucifer na kumuasi Mungu, hivyo vikajikabidhi kwa Lucifer japo si kwa kiwango kikubwa kama kile cha malaika na sehemu Nyingine.

Vita ikaisha Mungu akapanga na kupangua safu yake upya na kuweka mfumo mpya wa majukumu kwa kila kiumbe kilichobaki ikiwemo kuwapandisha baadhi ya malaika ngazi na kuwapangia majukumu mengine, na hapo ndipo malaika Mikaeli akapewa jukumu la kuwa mkuu na mwangalizi wa hii War Universe na akajulikana kama malaika mkuu.

Katika ulimwengu war oho kuna viumbe vya roho vikubwa sana na pia vyenye nguvu sana na vitiifu kwa Mungu kweli kweli ambavyo vimepewa usimamizi wa galaxies zote vingine vikiwa ni malaika na vingine vikiwa si malaika ila vinajulikana tu kama viumbe vya rohoni.

Lucifer alipoasi aliweka makao makuu yake nje ya Solar System yetu hii katika War Sphere japo Solar System yetu nayo ilikuwemo katika War Sphere hiyo ila haikuwa makao makuu ya Lucifer.

Tayari dunia na Solar System yetu hii ilikuwa inakaliwa na uzao mwingine ambao haukuwa uzao wetu huu wa Adam, katika uasi ule wao waliamua kujiunga na Lucifer lakini si kwa kiwango cha Ushetani ule maana viumbe waliokuwa wanakaa katika dunia hii hawakuwa wa kiroho ila wa kimwili.

Mungu akaamua kuwafutilia mbali na kuwanyang’anya mwili na kuwabakiza kuwa wa kiroho tu huku akiwaacha baadhi kukaa katika dunia hii hii ila katika dimension ya kiroho, lakini mpaka leo wanapambana kutafuta miili kwa kuwapagaa wanadamu kwa kuwa kwa maoni yao Mungu aliwadhulumu dunia yao na kuwanyang’anya miili yao, wengi wa wanadamu huwaita viumbe hawa kama mapepo, lakini ni roho zenye ubinadamu ndani yake zinazosihi katika ulimwengu wa roho.

Ikumbukwe kuwa si kila Shetani ni mapepo, kwenye ushetani kuna Majoka(hawa wengi wao huwa wakuu wa giza na mamlaka za giza), kuna mizimu(haya huwa ni mashetani yanayosimamia koo fulani na huku Afrika ni maarufu sana) kuna Miungu(hawa huwa ni wafalme wa giza) na kuna majini ambayo huwa ni mashetani yaneyoendana na mila za kiarabu.

Chini hapo kuna majeshi ya wafu, kuna viumbe vya rohoni vya giza ambavyo ni hybrid ya wanadamu na mashetani ambavyo huumbwa hasa kwa matendo ya zinaa za kishetani kama zinaa za majini mahaba, kuna vikaragosi, vinyamkera, vinwengo na madudu kibao.

Pia kuna mapepo

Roho zote hizi zinafanya kazi katika kambi ya Lucifer kwa sasa.

Mungu wetu ni Mungu wa mipango ambaye huwa ratiba yake na mapenzi yake hayavurugwi na yeyote, kwa hiyo baada ya vita ile akaamua kuendelea na zoezi lake la uumbaji kama hapo awali, zoezi ambalo linaendelea na litaendelea milele na milele kwa kuwa hana mwisho.

Hivyo Mungu akawatuma badhi ya Malaika zake wenye nguvu kuja kuangalia maeneo ambayo hayakuthiriwa sana na ushetani ili aendelee na uumbaji wake au kuyarekebisha marekebisho ya hapa na pale kuyarudhisha katika kusudi lake la awali.

Mmoja wa malaika wenye nguvu ambao Mungu aliwatuma hapa dunia kwa ajili ya kuisafisha dunia na solar Sstem hii kwa ajili ya Mungu kuendelea na mipango yake kama Muumbaji alikuwa anaitwa malaika Uryaluzzael.

Uryaluzzael huyu alikuwa mmoja wa malaika wenye nguvu sana wa kuweza kusimamia “Solar System” yote peke yake.
Kitendo cha Mungu kumtuma aje hapa duniani kilimshtua sana Lucifer na kumpa picha kuwa Dunia hii ni sehemu muhimu sana kwa Mungu na huenda anataka kufanya jambo zito sana, kwa hiyo akapambana na yeye akaja hapa hapa duniani kuanzisha empire yake.

Kitendo kile cha Lucifer kuhamishia makao hapa duniani kilifanya kuongezeka kwa giza katika Solar System na hivyo kumfanya Mungu kutoa hukumu ya haki ambapo dunia ilikuwa awali na miezi mitatu, miwili ikaharibiwa na kubakiza mmoja tu ambao tunao kwa sasa..

Malaika Uryaluzzael alikuja haa duniani kwa ajili ya kuianda dunia kwa ajili ya kuifinyanga upya ili kuumba uzao mpya kuikalia Galaxy yetu hii huku makao makuu yake yakiwa katika Solar System hii tuliyopo.
Yalikuwa ni maandalizi ya awali kabisa ya kuumbwa kwa Adam na uzao wake.

Maandaizi ya kuleta uzao mpya na kuufungua ukurasa mpya wa maisha mapya ambao sisi kwetu tunauita mwanzo. Na hapo ndipo Mungu alipoichukua dunia na mbingu zake na kuirudisha katika Creation Sphere au Raw Sphere ambayo kimsingi huwa imefunikwa na giza na maji huku Roho wa Mungu akiendelea na hatua za kwanza kabisa za uwezeshaji wa uumbaji ili pale Neno tu atakapofika kuanza kazi yake, uumbaji uanze mara moja.

Na ndipo maandiko yanapoanza kwa kusema hapo Mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na nchi, nayo nchi likuwa giza tena utupu, na Roho wa Mungu akatulia juu ya uso wa maji.

Kabla ya kuanza kusimulia mchakato wa uumbaji nitaanza kuuchambua ulimwengu wa roho wa Mbingu za Mungu na malaika zake halafu nitaenda kuichambua kuzimu ya Shetani na malaika zake na mifumo yao ya maisha jinsi walivyo.

Itaendelea.....
 
Mkuu Bilionea Asigwa

Kuna utofauti gani kati ya yesu na Mungu,

Maoni yako tafadhari
Mkuu sehemu ya Kwanza nimeelezea wa upana sana hio kitu hapo juu.

Ukienda ITV pale Mwenge utakuta kampuni haiitwi ITV ila ni IPP Media.
Kampuni hio kwa nje inajulikana kama ITV kama brand name iliyo maarufu, lakini kiuhalisia ni sehemu tu ya IPP Media.

Yesu ndiye Neno la Mungu na Jina Yesu halina muda mrefu kuanza kutumika, ni kama miaka 2000 tu imepita, lakini Neno alikuwepo kabla ya Jina Yesu kuanza kutumika na amefanya mambo makubwa sana kwa kuwa ndiye mtendaji mkuu wa Serikali ya Mungu.

Lakini kwa kuwa serikali ya Mungu ni ya Kifalme , Yesu au Neno huyo ndiye right hand man wa Ufalme wa Mungu au wa Serikali ya Mungu.

Yesu ni Mungu kwa cheo chake.
Yesu ni Mtendaji mkuu wa Serikali ya Mungu kwa utendaji wake.
Yesu ni mwokozi wa wanadamu huku duniani.
Lakini Yesu pia ndiye kamanda mkuu wa vikosi vyote vyma mbinguni kivita kwa kuwa wanadamu hupata mamlaka ya kuwaamuru malaika kwa kutumia Jina la Yesu, au wamepewa uwezo wa kiutendaji kwa kujificha chini ya Jina la Yesu.
Yesu pia ndiye Hekima kama kitabu cha Mithali kinavyomtaja.

Ila nikwambie tu siri moja ambayo ulikuwa huijui, inawezekana kabisa siku ukaenda Mbinguni usimkute Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu kwa utofauti wao kama tunavyoelewa huku duniani, ila Ukamkuta Yesu tu kwa kuwa hawa ni wamoja ila pia wao ni tofauti.
 
Mkuu sehemu ya Kwanza nimeelezea wa upana sana hio kitu hapo juu.

Ukienda ITV pale Mwenge utakuta kampuni haiitwi ITV ila ni IPP Media.
Kampuni hio kwa nje inajulikana kama ITV kama brand name iliyo maarufu, lakini kiuhalisia ni sehemu tu ya IPP Media.

Yesu ndiye Neno la Mungu na Jina Yesu halina muda mrefu kuanza kutumika, ni kama miaka 2000 tu imepita, lakini Neno alikuwepo kabla ya Jina Yesu kuanza kutumika na amefanya mambo makubwa sana kwa kuwa ndiye mtendaji mkuu wa Serikali ya Mungu.

Lakini kwa kuwa serikali ya Mungu ni ya Kifalme , Yesu au Neno huyo ndiye right hand man wa Ufalme wa Mungu au wa Serikali ya Mungu.

Yesu ni Mungu kwa cheo chake.
Yesu ni Mtendaji mkuu wa Serikali ya Mungu kwa utendaji wake.
Yesu ni mwokozi wa wanadamu huku duniani.
Lakini Yesu pia ndiye kamanda mkuu wa vikosi vyote vyma mbinguni kivita kwa kuwa wanadamu hupata mamlaka ya kuwaamuru malaika kwa kutumia Jina la Yesu, au wamepewa uwezo wa kiutendaji kwa kujificha chini ya Jina la Yesu.
Yesu pia ndiye Hekima kama kitabu cha Mithali kinavyomtaja.

Ila nikwambie tu siri moja ambayo ulikuwa huijui, inawezekana kabisa siku ukaenda Mbinguni usimkute Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu kwa utofauti wao kama tunavyoelewa huku duniani, ila Ukamkuta Yesu tu kwa kuwa hawa ni wamoja ila pia wao ni tofauti.
Kuna hawa watu wa dinibya MASHAHIDI WA YEHOVA walinukuta nimetulia zangu,

Nikasema ngoja niwasikilize,
Wao wanasema yesu aliumbwa na mungu hivyo basi yesu sio mungu wakanionyesha na vifungu vingi sana,

Nami nikakubaliana nao ili nipate muda wa kuchunguza hoja zao,

Kimsingi nilichokuja kukigundua hili swali nililo kuuliza ndio chanzo cha kuibuka kwa dini zingine ndogo ndogo.
 
Mkuu sehemu ya Kwanza nimeelezea wa upana sana hio kitu hapo juu.

Ukienda ITV pale Mwenge utakuta kampuni haiitwi ITV ila ni IPP Media.
Kampuni hio kwa nje inajulikana kama ITV kama brand name iliyo maarufu, lakini kiuhalisia ni sehemu tu ya IPP Media.

Yesu ndiye Neno la Mungu na Jina Yesu halina muda mrefu kuanza kutumika, ni kama miaka 2000 tu imepita, lakini Neno alikuwepo kabla ya Jina Yesu kuanza kutumika na amefanya mambo makubwa sana kwa kuwa ndiye mtendaji mkuu wa Serikali ya Mungu.

Lakini kwa kuwa serikali ya Mungu ni ya Kifalme , Yesu au Neno huyo ndiye right hand man wa Ufalme wa Mungu au wa Serikali ya Mungu.

Yesu ni Mungu kwa cheo chake.
Yesu ni Mtendaji mkuu wa Serikali ya Mungu kwa utendaji wake.
Yesu ni mwokozi wa wanadamu huku duniani.
Lakini Yesu pia ndiye kamanda mkuu wa vikosi vyote vyma mbinguni kivita kwa kuwa wanadamu hupata mamlaka ya kuwaamuru malaika kwa kutumia Jina la Yesu, au wamepewa uwezo wa kiutendaji kwa kujificha chini ya Jina la Yesu.
Yesu pia ndiye Hekima kama kitabu cha Mithali kinavyomtaja.

Ila nikwambie tu siri moja ambayo ulikuwa huijui, inawezekana kabisa siku ukaenda Mbinguni usimkute Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu kwa utofauti wao kama tunavyoelewa huku duniani, ila Ukamkuta Yesu tu kwa kuwa hawa ni wamoja ila pia wao ni tofauti.
Mkuu Kwa maandishi haya nimejifunza kwamba ni vigumu mwanadamu kumuona Mungu Kwa macho haya ata macho ya roho pia .kwakua inaonyesha utawala Wa Mungu una muundo kama tawala za kidunia yaani namaanisha ni sawa na Leo Mwananchi Wa kawaida atoke nyumbani kwake na kwenda ikulu eti anataka kuonana na magufuli ni ngumu sana.

nimesema hivyo kwakua uandishi wako inaonyesha kuwa kuna ata malaika ambao hawana uwezo wakuonana na Mungu au kuwajibika Kwa Mungu moja Kwa moja isipokuwa Kwa kupitia kwa wasaidizi wake Wa karibu.
 
Kuna hawa watu wa dinibya MASHAHIDI WA YEHOVA walinukuta nimetulia zangu,

Nikasema ngoja niwasikilize,
Wao wanasema yesu aliumbwa na mungu hivyo basi yesu sio mungu wakanionyesha na vifungu vingi sana,

Nami nikakubaliana nao ili nipate muda wa kuchunguza hoja zao,

Kimsingi nilichokuja kukigundua hili swali nililo kuuliza ndio chanzo cha kuibuka kwa dini zingine ndogo ndogo.
Mkuu Mashahidi wa Yehova wamechakachua mambo mengi sana.

Kwanza wanaamini Roho Mtakatifu si nafsi hai, bali ni nguvu ya Uungu inayotenda kazi ambayo kimsingi ni nguvu mfu.
Kama ambavyo gravitational force ni nguvu inayotenda kazi japo ni mfu, gravitational force hapa duniani huvuta vitu vyote kuelekea kwenye centre ya dunia, japo haina utashi wa kuamua wala hisia wala chochote ni just nguvu tu.
Hivyo hivyo kwa Roho Mtakatifu kwao ni nguvu tu ya kiroho, na wao wanamuita Roho huyu kuwa ni Roho Takatifu.

Pili hawaamini katika Mbingu mpya na dunia mpya baada ya Kiama, wanaamini katika Mungu kufagia tu uovu duniani na kubakiza wema, kwa msingi huo wanaamini hata majumba yaliyojengwa na wanadamu kama yale ya Posta pale Dar es Salaam yatabakizwa mara baada ya kiama kwa kuwa Mungu "si mjinga kihiivyo" kuivuruga dunia, na ndio maana makanisa yao yanaitwa JUMBA LA UFALME wakiamini kuwa yatadumu milele na milele.

Yapo mambo mengi sana nyuma ya pazia kwa kuwa Shetani amebuni mbinu mpya ya kuwadanganya wanadamu ambayo ni kuuchanganya uongo na ukweli, anachukua nusu uongo anamiksi na nusu ukweli, hapo ndipo upotofu mzito sana unatokea.

Lakini Ukisoma Biblia kwa mapana yake utaona kuna mapungufu mengi sana.
 
Mkuu Kwa maandishi haya nimejifunza kwamba ni vigumu mwanadamu kumuona Mungu Kwa macho haya ata macho ya roho pia .kwakua inaonyesha utawala Wa Mungu una muundo kama tawala za kidunia yaani namaanisha ni sawa na Leo Mwananchi Wa kawaida atoke nyumbani kwake na kwenda ikulu eti anataka kuonana na magufuli ni ngumu sana. nimesema hivyo kwakua uandishi wako inaonyesha kuwa kuna ata malaika ambao hawana uwezo wakuonana na Mungu au kuwajibika Kwa Mungu moja Kwa moja isipokuwa Kwa kupitia kwa wasaidizi wake Wa karibu.
Unachokisema ni kweli kabisa mkuu.

Hata Malaika wanayeishi na Mungu huko juu hawamuelewi huyu Mungu ni nani.
Katika kozi ambazo haziishi mbinguni ni kozi inayoitwa "Kumuelewa Mungu".

Hii ni kozi inayosomwa milele na milele na milele yote na kila kiumbe alichokiumba Mungu, si Malaika wala si wanadamu wala si kiumbe chochote cha kiroo kinaweza ku-graduate katika kozi hii.

Huko mbele nitaelezea concept moja makini sana ambayo kwa kifupi ni kuwa Mungu hujifunua kwa kila kiumbe chake kwa Level ya kiroho waliyo nao hao viumbe wake kwa kuwa yeye ni mkuu mno huwezi kumuelewa akija kama alivyo.

Na ni kweli kuwa Mungu ana mfumo wa utawala kama ulioko huku duniani, lakini yuko accessible kwa kila kiumbe chake, hakuna protocol ngumu ya kumuona kama ilivyo huku duniani, ila angalizo ni moja tu kuwa Mungu huyo unayemuona wewe si Mungu yule anayemuona Serafi au Kerubi, ndio maana wenye uhai wanne wale husihi tu kuimba mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu milele yote.

Si kwa sababu wanapenda kumsifu sana ila ni kwa sababu Kila siku wanamuona katika version mpya ambayo walikuwa hawajawahi kuiona, na katika hili kazi yao kuu ni kuitaja sifa kuu waiyoiona kwa wakati huo.
Na kwa kuwa daima anapanda katika viwango kwao kulingana na ufahamu wao, wao huishia tu kusema Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu maana hata wao wanashindwa kumuelewa.

Kwa hiyo ukienda Mbinguni leo ukataka kuonana na Mungu utapelekwa moja kwa moja na utakaa karibu naye kabisa, ila perception yako kwake italingana na uwezo wako wa ku conceive mambo ya Kiroho kwani wakati unadhani unamfahamu kumbe hata bado hujaanza kumfahamu.
 
What are source for these informations so that we also get their proof proof that these are not fake informations.
Nitaweka source hapo chini baadaye kidogo mkuu.
Uandishi wa kamala unachukua muda sana kuhakikisha accuracy ya kila unachokiandika.
Nitaweka tu sources zangu zote baadaye kidogo, usiwe na wasi wasi.
 
Mkuu sehemu ya Kwanza nimeelezea wa upana sana hio kitu hapo juu.

Ukienda ITV pale Mwenge utakuta kampuni haiitwi ITV ila ni IPP Media.
Kampuni hio kwa nje inajulikana kama ITV kama brand name iliyo maarufu, lakini kiuhalisia ni sehemu tu ya IPP Media.

Yesu ndiye Neno la Mungu na Jina Yesu halina muda mrefu kuanza kutumika, ni kama miaka 2000 tu imepita, lakini Neno alikuwepo kabla ya Jina Yesu kuanza kutumika na amefanya mambo makubwa sana kwa kuwa ndiye mtendaji mkuu wa Serikali ya Mungu.

Lakini kwa kuwa serikali ya Mungu ni ya Kifalme , Yesu au Neno huyo ndiye right hand man wa Ufalme wa Mungu au wa Serikali ya Mungu.

Yesu ni Mungu kwa cheo chake.
Yesu ni Mtendaji mkuu wa Serikali ya Mungu kwa utendaji wake.
Yesu ni mwokozi wa wanadamu huku duniani.
Lakini Yesu pia ndiye kamanda mkuu wa vikosi vyote vyma mbinguni kivita kwa kuwa wanadamu hupata mamlaka ya kuwaamuru malaika kwa kutumia Jina la Yesu, au wamepewa uwezo wa kiutendaji kwa kujificha chini ya Jina la Yesu.
Yesu pia ndiye Hekima kama kitabu cha Mithali kinavyomtaja.

Ila nikwambie tu siri moja ambayo ulikuwa huijui, inawezekana kabisa siku ukaenda Mbinguni usimkute Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu kwa utofauti wao kama tunavyoelewa huku duniani, ila Ukamkuta Yesu tu kwa kuwa hawa ni wamoja ila pia wao ni tofauti.
...haya maelezo yameegemea zaidi zile ngano za kwenye biblia ,sidhani kama Quran na vitabu vya iman zingine vina story hizi mkuu
...my point is_una uhakika gani kama hizi story za biblia ndio sahihi kumuelezea Mungu wa kweli na kuona story za tamaduni zingine kama ni za Miungu,Mizimu,Mapepo etc

......sidhani kama wasio wakristo wataelewa hizi mambo unazoeleza hapa mkuu....nafikiri hizi zilifaa zaidi kuelezea kanisani coz uhakika wake pia ni questionable kwa watu wasio amini biblia ambao ni wengi tu
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom