Biblia kwa Jicho Jingine

Mkuu umegusia jina la Yesu ningependa unisaidie jambo mfano Yesu kwa kiswahili ukienda nchi nyingine unakuta anaitwa Yashuah au uingereza utakuta ni JESUS.... Na kuna maeneo mengine duniani kama Asia Yesu au Jesus ina maana tofauti kabisa na wanatumia jina tofauti kumaanisha Yesu...

Sasa nachojiulizaga inayofanya kazi ni LILE jina la mwana wa Mungu tunalotaja kwa makabila Yetu au ni ile imani kichwani inayotengeneza connection kati ya sisi wanadamu na mwana wa Mungu (bila kujali anaitwa Yesu kiswahili au yashuah kiebrania)....

Naomba unisaidie ingawa nimetoka nje ya mada
popote pale unapotaja jina la YESU haijalishi
unataja kwa kilugha au kwa kibongo
but mapepo yana Hali ya utambuzi
na jina la YESU NI fireee kweli kweli.
so mapepo yatatambua kuwa umemgusia YESU mwana wa MUNGU
kuna tofauti kubwa Kati ya YESU mwana wa Mungu na issa bint Maryam
dats Y? kwa waislamu hata ukisema kwa jina la issa bint Maryam Pepo hazitapata tabu sanaaa
but washa moto kwa kibwagizo cha jina la YESU KRISTO mwana wa Mungu aseee.
Ni sawa na kusema kwa damu ya YESU na kwa damu Ya issa
All in all Jina la YESU litaendelea kuwa Kubwa kuliko hata jina la Mtume (SAW)
 
umejibu kimajivuno sana.ebu peleka nyavu zako katika kina kirefu ili uweze kuwapata Samaki wengi zaidi .
 
MKUU lipo jina linalofanya nijibu hivyo
tangu nizaliwe mpaka nakuwa hivi
SIJAWAHI SIKIA JINA LA MTU LIKIPONYA/KUTOA PEPO/KUOGOPEKA
ZAIDI YA JINA MOJA TU......
nadhani unalifahamu siyo ngeni kwako bali ni jina la YESU KRISTO MWANA WA MUNGU
hata ukileta battle Kati ya
jina la YESU vs Mtume (SAW)
la mtume lazima litakaaa
hivi hujawah jiuliza Y? jina la YESU ni fireee compare to Mtume(SAW)????
Najivunia kuwa na jina la YESU lenye NGUVU...
 
Pingamizi zangu za kimantiki kuhusu uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa kiingereza "proof by contradiction", bado hazijapata majibu ya kuziondoa.

Hivyo, Mungu hayupo.

Kama mtu anasemayupo, athibitishe kwa kuanza kuondoa contradictions zilizopo katika habari ya kuwapokwake.

Mungu anatakiwa asiwe na contradiction. Huyu Mungub wa Biblia na Quran kwa mfano, mtu akiweza kuniondolea contradictions zote zilizopo katika habari zake, sio tu nitakubali, bali pia nitafurahi sana. Contradictions hizo ni hizi.
Kwa uchache.

1. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na utakatifu wote, kaumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kutokea, wakati alikuwa ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezi kutokea? Naomba jibu lisiwe kusema maovu yapo kwa sababu ya shetani. Swali linauliza kabla shetani hajaumbwa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezi kuwepo. Jibu la swali lisiseme maovu ni matokeo ya dhambi za watu. Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani. Jibu lisiseme free will, hatuna hiyo inayoitwa free will katika mengi sana na hata kui define tu watu hawawezi.

2. Inakuwaje Mungu awe ndiyo mtoa rehema ya kumjua, anachagua mwenyewe nani amjue na nani asimjue, halafu mtu akishindwa kumjua Mungu, kwa sababu Mungu hajamchagua huyo mtu kumpa neema yake Mungu ya kumjua, huyo mtu aonekane ana makosa, ahukumiwe kuchomwa moto? Baba anawezaje kumhukumu mtoto ambaye hajui kusoma, kama mtoto hajui kusoma kwa sababu baba ndiye aliyemnyima nafasi ya kwenda shule?

3. Inakuwaje mahakama za watu tu zinakataza mtoto kuhukumiwa kwa makosa ya mzazi, lakini vitabu vya Mungu vinasema Mungu anahukumu watoto na wajukuu vizazi hata vizazi? Kwa kosa la mzazi wa zamani sana? Huyu Mungu mbona haki yake haijafikia hata haki yetu watu tu?

4. Mnasema Mungu anajua yote. Anayajua maisha ya mtu yote mwanzo mpaka mwisho kabla hata mtu hajaishi. Na anachojua huyo Mungu kitatokea, ni lazima kitokee. Anavyojua si kama utabiri wa hali ya hewa kwamba kuna 80% ya mvua. Yeye anajua kitu kamili hakina utata. Sasa kama anajua hivyo, ina maana mtu muuaji, alimjua huyu atakuwa muuaji kabla hata hajazaliwa. Na muuaji huyo hawezi kuepuka kuua hata afanye nini. Kwa sababu kuepuka kuua wakati Mungu kashajua huyu ataua ni kum prove Mungu wrong. Sasa kama huyu mtu anaenda kuwa muuaji, na hana jinsi ya kuepuka hilo, tutasemaje ana uhuru wa kuamua na anaua kwa uamuzu wake na atahukumiwa motoni kwa uuaji?

5. Mbona hivyo vitabu vinavyosemwa ni vya Mungu vina contradictions lukuki?

6. Mbona huyo Mungu mnayemsema yupo hathibitishiki? Anajificha asijulikanw vizuri kwa nini? Kwa nini hakufanya ulimwengu uweze kumjua vizuri bila uwezo wowote wa kuwepo ubishi juu ya uwepo wake?

7. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Akiweza kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote, maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kulibeba. Akishindwa kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kuliumba.

8. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ameruhusu kifo kitenganishe wapendanao, baba na mama, wazazi na mtoto, marafiki etc, wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo?

Kwa nini watetezi wa Quran waajitapa sana kusema vitu fulani vichache vimethibitishwa kisayansi, kuinadi Quran kama kitabu cha ukweli, wakati vingi sana vina contradictions ama vinapingana na sayansi ama havijathibitishwa kisayansi, hawasemi vinapingana nansayansi au havijathibitishwa kisayansi?

10.Kama kuna Mungu kweli, kwa nini karuhusu confusion ya dini nyingi tofauti kuwa na vitabu vingi tofauti vyote vinasema vya Mungu wa kweli?

Kwa leo tuishie na maswali haya 10.

Unaweza kujibu ?
Mkuu sina majibu kwa haya maswali yako ila najitetea kwa kile ninachofahamu ingawa pia sina hakika nacho, kwamba Mungu yupo, ila vielelezo vinavyomuekezea labda havipo sahihi.

Lakini kama umemsoma mtoa mada sehemu ya kwanza na ya pili utajua kwanini Mungu hajidhirishi kama unavyotaka wewe Kiranga ila kuna watu amejidhihisha kwao,na hao aliojidhihirisha ni kwa kiwango cha uwezo wao na si kama alivyo.

Maoni yangu Mungu hatujamjua bado na hatutamjua kwa maana hatutaki kumjua ila JUA YA KWAMBA MUNGU YUPO ZAIDI AJULIKANAVYO.
 
Huna majibu ya maswali yangu na huna uhakika na unachojitetea nachokwa sababu Mungu hayupo.

Unaandikavitu usivyona uhakika navyo.

Kwa kauli yako mwenyewe umekubali hili.
 
Pingamizi zangu za kimantiki kuhusu uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa kiingereza "proof by contradiction", bado hazijapata majibu ya kuziondoa.

Hivyo, Mungu hayupo.

Kama mtu anasemayupo, athibitishe kwa kuanza kuondoa contradictions zilizopo katika habari ya kuwapokwake.

Mungu anatakiwa asiwe na contradiction. Huyu Mungub wa Biblia na Quran kwa mfano, mtu akiweza kuniondolea contradictions zote zilizopo katika habari zake, sio tu nitakubali, bali pia nitafurahi sana. Contradictions hizo ni hizi.
Kwa uchache.

1. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na utakatifu wote, kaumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kutokea, wakati alikuwa ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezi kutokea? Naomba jibu lisiwe kusema maovu yapo kwa sababu ya shetani. Swali linauliza kabla shetani hajaumbwa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezi kuwepo. Jibu la swali lisiseme maovu ni matokeo ya dhambi za watu. Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani. Jibu lisiseme free will, hatuna hiyo inayoitwa free will katika mengi sana na hata kui define tu watu hawawezi.

2. Inakuwaje Mungu awe ndiyo mtoa rehema ya kumjua, anachagua mwenyewe nani amjue na nani asimjue, halafu mtu akishindwa kumjua Mungu, kwa sababu Mungu hajamchagua huyo mtu kumpa neema yake Mungu ya kumjua, huyo mtu aonekane ana makosa, ahukumiwe kuchomwa moto? Baba anawezaje kumhukumu mtoto ambaye hajui kusoma, kama mtoto hajui kusoma kwa sababu baba ndiye aliyemnyima nafasi ya kwenda shule?

3. Inakuwaje mahakama za watu tu zinakataza mtoto kuhukumiwa kwa makosa ya mzazi, lakini vitabu vya Mungu vinasema Mungu anahukumu watoto na wajukuu vizazi hata vizazi? Kwa kosa la mzazi wa zamani sana? Huyu Mungu mbona haki yake haijafikia hata haki yetu watu tu?

4. Mnasema Mungu anajua yote. Anayajua maisha ya mtu yote mwanzo mpaka mwisho kabla hata mtu hajaishi. Na anachojua huyo Mungu kitatokea, ni lazima kitokee. Anavyojua si kama utabiri wa hali ya hewa kwamba kuna 80% ya mvua. Yeye anajua kitu kamili hakina utata. Sasa kama anajua hivyo, ina maana mtu muuaji, alimjua huyu atakuwa muuaji kabla hata hajazaliwa. Na muuaji huyo hawezi kuepuka kuua hata afanye nini. Kwa sababu kuepuka kuua wakati Mungu kashajua huyu ataua ni kum prove Mungu wrong. Sasa kama huyu mtu anaenda kuwa muuaji, na hana jinsi ya kuepuka hilo, tutasemaje ana uhuru wa kuamua na anaua kwa uamuzu wake na atahukumiwa motoni kwa uuaji?

5. Mbona hivyo vitabu vinavyosemwa ni vya Mungu vina contradictions lukuki?

6. Mbona huyo Mungu mnayemsema yupo hathibitishiki? Anajificha asijulikanw vizuri kwa nini? Kwa nini hakufanya ulimwengu uweze kumjua vizuri bila uwezo wowote wa kuwepo ubishi juu ya uwepo wake?

7. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Akiweza kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote, maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kulibeba. Akishindwa kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kuliumba.

8. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ameruhusu kifo kitenganishe wapendanao, baba na mama, wazazi na mtoto, marafiki etc, wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo?

Kwa nini watetezi wa Quran waajitapa sana kusema vitu fulani vichache vimethibitishwa kisayansi, kuinadi Quran kama kitabu cha ukweli, wakati vingi sana vina contradictions ama vinapingana na sayansi ama havijathibitishwa kisayansi, hawasemi vinapingana nansayansi au havijathibitishwa kisayansi?

10.Kama kuna Mungu kweli, kwa nini karuhusu confusion ya dini nyingi tofauti kuwa na vitabu vingi tofauti vyote vinasema vya Mungu wa kweli?

Kwa leo tuishie na maswali haya 10.

Unaweza kujibu ?

Mkuu mimi nilianza kusoma haya maswali yako zamani sana tangu ile mada ya yule jamaa aliyesema 'Mungu yupo; majibu kwa wasioamini' japo sikuwahi kucomment.

Mada kama hii ukiisoma hali unasikiliza kutoka ndani ya moyo wako hakika utajua Mungu yupo pamoja na ukuu wake.
 
MKUU Hawa ambao wanakifanya ni atheist achana nao
maadamu umewapa ukweli kuwa yupo Above all na kama kagoma basi hutokuwa na hatia ya damu yake
lakini pia hata sauli (Paul) before hajawa mtumishi wa MUNGU naye alikuwa na minajili tofaut so MUNGU na uhakika ipo day atambadilisha kiranga
 
Mkuu mimi nilianza kusoma haya maswali yako zamani sana tangu ile mada ya yule jamaa aliyesema 'Mungu yupo; majibu kwa wasioamini' japo sikuwahi kucomment.

Mada kama hii ukiisoma hali unasikiliza kutoka ndani ya moyo wako hakika utajua Mungu yupo pamoja na ukuu wake.
Sijauliza uniambie utajua nini moyoni mwako.

Nina maswali 10 hapo juu, hujayajibu.
 
Nadhani mkuu zitto upo correct japo utaeleweka kwa tabu niliwahi gusia hili jambo nikapingwa kabisa. Tumesahau hilo ni jina tu na kuna mahali halitumiki hivyo. Nafikiria zaidi Imani ndiyo kila kitu
Mkuu umegusia jina la Yesu ningependa unisaidie jambo mfano Yesu kwa kiswahili ukienda nchi nyingine unakuta anaitwa Yashuah au uingereza utakuta ni JESUS.... Na kuna maeneo mengine duniani kama Asia Yesu au Jesus ina maana tofauti kabisa na wanatumia jina tofauti kumaanisha Yesu...

Sasa nachojiulizaga inayofanya kazi ni LILE jina la mwana wa Mungu tunalotaja kwa makabila Yetu au ni ile imani kichwani inayotengeneza connection kati ya sisi wanadamu na mwana wa Mungu (bila kujali anaitwa Yesu kiswahili au yashuah kiebrania)....

Naomba unisaidie ingawa nimetoka nje ya mada
 
Hili bado liko kiimani zaidi, vile dini zingine wao wakieleza huwa ni different stori
 
Huna majibu ya maswali yangu na huna uhakika na unachojitetea nachokwa sababu Mungu hayupo.

Unaandikavitu usivyona uhakika navyo.

Kwa kauli yako mwenyewe umekubali hili.
Ninauhakika na ninacho kitetea ila sina hakika KAMA KILE KINACHOMUELEZEA NI SAHIHI AU LA! ambacho ni maandiko kwenye vitabu vitakatifu.
Nimesema nimekosa majibu ya maswali yako ndugu yangu kwa sababu ya aina ya majibu unayotaka.

Ila jua Mungu yuko zaidi ya vile tunavyodhani.
 
Unajuaje una uhakika? Unathibitishaje hili ni lahakika?
 
Sijauliza uniambie utajua nini moyoni mwako.

Nina maswali 10 hapo juu, hujayajibu.

Hapo ndio tatizo lilipo mkuu kiranga, si kila jambo unasikiliza kwa ufahamu Wa kwenye ubongo.

Yapo mambo mengi hautapata jawabu la kisayansi lakini moyoni unajua hili ndio jibu.

Labda nikuulize swali, unaamini kuwa mtu ana roho? Kuna kitu chochote kinachotoka na kuondoka inapotokea mtu amefariki? Nini hasa kinasababisha mtu afe? Bado sijaenda nje ya mada maana natamani ndugu uanze kuyatazama maisha kutoka ndani ya moyo wako. Yatosha sasa kwako kutumia tu ubongo ulio very limited.
 
Rafiki Leo nimejtahd Nimesoma Yote..
Lakin swali LANGU Ni kwamba Mungu anajua kitakachotokea baada ya mda kadhaa au hajui?
 
Back
Top Bottom