Bibi Tina wa Mwananyamala

Bibi Tina wa Mwananyamala

Kuna siku nilienda kumsalimia kaka yangu miaka ya nyuma maeneo ya banana nikiwa mwanafunzi wa chuo kikuu..

Usiku wa kwanza tu usiku wa manane nilishtuka na kwa macho yangu nikaona watu wawili chumbani nilibaki kama nimepigwa na ganzi ila taratibu walipotelea kwenye pembe ya ukuta..

Hakika tangu siku hiyo niliamini uchawi upo.

Na cha ajabu kesho yake asubuhi kuwasimulia wakanieleza wanaelewa ni jirani yao ana hiyo michezo maana kila wakijaribu kufuga mbwa lazima mbwa afe ila wataipata tu dawa yake
 
Siku zote mchawi aliyekamatwa usithubutu kumgusa lazima likupate jambo. Otherwise ukifanya hivyo uwe nawe umechemshwa kwenye pipa la ukweli ukaiva.
 
Inaendelea......
Askari kufikishwa Mwananyamala hana tatizo ila mkono haukunjuki.. Huku nyumbani bibi akabembelezwa yaishe hapelekwi polisi.. Alipokubali tu na kutoka nje kule hospital mambo poa... Askari hakurudi tena kwa bibi.

Ila wakaja askari vichaa.. Nani wa Mwananyamala anamkumbuka Henjewele wa Oysterbay? Huyu ndio alimtia bibi Tina pingu na kumpeleka lupango... Akafunguliwa kesi ya trespassing... Akakaa mpaka kesho yake tukamtoa na mwalimu akahama wiki ileile

Bibi Tina kuna kijana mpangaji alikuwa anampenda sana anaitwa Evarist.. Huyu kijana alikuwa anafanya kazi maeneo ya vijana.. Kwahiyo alikuwa anadamka alfajiri na kurudi usiku.

Hakuwa na demu wala mchumba.. Basi huyu alikuwa anachotewa maji na bibi na sometimes hata kupewa chakula... Baadae alikuja kuhamia binti wa ndugu yake bibi Tina, alikuwa anamuita bibi mama mkubwa.. Huyu akapewa chumba cha ndani next to Evarist.

Taratibu na kwa siri wawili hawa wakawa wapenzi... Bibi hakupenda kabisa hii habari

Kwanza akamuita Evarist na kumkandia sana yule binti kuwa ni malaya nknk... Lakini jamaa hakuelewa somo... Kisha akamuita binti na kumkandia jamaa kuwa hana kitu ni fukara.. Lakini haikusaidia.. Siri ya kutaka kuwaachanisha ni kwamba bibi alikuwa anajisevia usiku kwa Evarist... Jamaa alikuwa haishiwi na ndoto za ngono... Bibi aliwafanyia visa mpaka walihama alfajiri... Na maranyingi alipenda sana kutuma panya na nyoka weusi..

Yani saa kumi na mbili jioni panya anaingia kwako na kukuuma au usiku anakuja na kukuvuta kende.... Visa vilikuwa vingi mpaka wakatimkia Tabata
Huku episodes zikawa haziishi.. Kuna wakati wapangaji tulikuwa tunaamka wote tuko hoi sana na tuna matope ama michanga miguuni....

Huku na huku mara paaap nikaopoa mtoto wa kingazija mweupe pee kama Mwarabu wa muscut... Hapa ndio mambo yakawa motoooo... Ilianza kwa yeye kuja weekend tunaenda Jolly club pembeni ya las Vegas kucheza kuch kuch hotae.. Halafu tunarudi home kumalizia na KWICHI KWICHI hatari.

Jumamosi yote hatutoki ndani... Hili jambo bibi hakulipenda ila akawa mvumilivu
Mtu wangu huyu akanifundisha na kunifunulia mengi nikaongeza na ya kwangu basi ikawa ni michezo ya kuwindana na kushindana.... Yani bibi Tina ilikuwa ni lazima usiku atembelee wapangaji wake vyumbani na kucheza nao sometimes katitu

Mngazija wangu akahamia rasmi... Moto ukawa ndio kama umetiwa petrol.. Ikawa yeye ni mwendo wa UDI na marashi makali... Basi ukija bibi yuko hoi... Siku moja akaniita... Akaniambia babu nakupenda sana lakini huyu mvaa pedi wako sitaki kumuona hapa ATANIUA.. niko tayari nikupe hela akapange kwingine lakini siko tayari kumuona tena hapa.

Hili lilikuwa kubwa kuliko tulihama wiki ile ile bila taarifa... Mimi nilidamka kwenda kazini huku mwenzangu kajifungia ndani anapaki kimya kimya... Kuja saa sita nikaenda kumuaga bibi.. Niliacha kodi ya miezi miwili.. Cha ajabu akaniambia anajua kuwa nahama... Sikujali nikaita gari

Wakati wa kutoa vyombo akafunga mlango mkubwa akatutaka tutolee mlango mdogo just imagine.... Lakini wakati tunatoa vyombo akawaita wale wazee wawili mmoja wapo ni huyo hapo pichani.. Wakaanza kufagia pale nje kwa pozi sana..
Kwahiyo kama mmebeba kabati inabidi muwasubiri.. Halafu wanachofagia hakionekani.. Vyombo vya kutoa dk 20 tulimaliza lisaa kwa kero zao za kufagia visivyoonekana.

Bibi alikuwa na watoto watano lakini kila mwaka alikuwa anakufa mmoja... Wa mwisho ni mama Whit alikufa 2012.. Huyu alikuwa anaishi hapo hapo... Bibi Tina alikuwa ni never miss Kanisani akivaa msalaba mkubwa kama wa nabii Tito na miwani kubwa kama sight mirrors za land rover 110
Kesho nitaenda kumsalimia kama bado yuko hai


JamiiForums naomba kuunganisha hii part B na ile A
Kumbe ukichoma udi mchawi hasogei!!! , mi nimepanda mzaituni pembeni, wachawi nawasikia mtaa wa jirani huku hawasogei
 
wanakusonya kama nawaona
Siku nitayomkamata mchawi, atajuta kuzaliwa. Nina bakora ya mpira wa tairi itamuishia mwilini. Actually huwa siwaogopi kabisa wachawi, nina confidence sana kwa wachawi ila sijui ni kwanini nakuwa na huu ujasiri
 
Siku nitayomkamata mchawi, atajuta kuzaliwa. Nina bakora ya mpira wa tairi itamuishia mwilini. Actually huwa siwaogopi kabisa wachawi, nina confidence sana kwa wachawi ila sijui ni kwanini nakuwa na huu ujasiri
ndo maana huwakamati kwani unadhani nao hawana akili
 
ndo maana huwakamati kwani unadhani nao hawana akili
Et kwanini manyaunyau akimkamata mchawi anamnyoa nywele? Na Mimi nikimkamata nikamnyoa na kumtembezea kichapo si ndo itapendeza zaidi? Au mpaka unywe damu ya paka?
 
Et kwanini manyaunyau akimkamata mchawi anamnyoa nywele? Na Mimi nikimkamata nikamnyoa na kumtembezea kichapo si ndo itapendeza zaidi? Au mpaka unywe damu ya paka?
nywele hubeba chaja ya nguvu za giza
 
Back
Top Bottom