Bibi harusi atimua mbio katikati ya harusi

Bibi harusi atimua mbio katikati ya harusi

Tatizo siyo la binti. Mwenye makosa ni uwongo wa kijana. Kwa nini hakuwa mkweli? Kama kadanganya suala la ajira ambalo liko ni la kawaida na liko nje, ataaminika vipi kwa mengine? Kumbuka katika kujenga familia kuna masuala makubwa na ya muhimu kuliko ajira. Akiwa mwongo kwenye ajira, tena wakati wa uchumba, atakuwa mkweli vipi kwa mengine?

Huyu binti nimempenda sana. Anaona maisha ya jianaume liongo ni jehanum. Mshahara wa udanganyifu!. Mtu mwongo haaminiki kwa lolote!
Afadhali wewe umeona kwa jicho lingine....
 
kama mtu huna kazi si useme tu ulishwe mjini hapa? mbwembwe za nini? oooh manji mjomba wangu sema kasafiri,ooh mengi shemeji wa jirani yetu yupo kwenye kikao
oooh atm imevunjika? ooooh account imefungiwa kumbe huna lolote
hata mimi ningekimbia maana kama umempendea mtu hela kumbe hana utasubiri nini? semeni kweli nyie wanaume
kwani huwa mnatufuata kwa sababu ya mengi,manji na ATM! kumbe huwa mnaolewa na pochi siyo wanaume
 
Watu walipigwa na mshangao mkubwa nchini Nigeria baada ya bibi harusi kutoroka kanisani alipogundua mume wake mtarajiwa sio mfanyikazi wa kampuni moja ya ya kitajiri ya kuuza mafuta.

Je ungekuwa wewe mwanamume ama mwamamke umeachwa mataani kwenye harusi yako mbele ya watu kibao familia ,ndugu na marafiki na maadui waanza vipi??

13939492_919033928207921_4159767238860158401_n.jpg


13935057_919034014874579_4641078331574013128_n.jpg

Naona Mkuu Amavubi unafuata nyayo za Msaga Sumu sio!
 
Get angry get inspired... Jamaa aliekimbiwa atakuja kuwa milionea kwa hasira alizopata hapo
 
Umetumia uongo ili umpate mkiingia ndoani na muendelezo wa uongo akivurunda utamlaumu?
Akijipata ameshatekwa nyara hana ujanja, kinachofuata hapo ni ubabe sio ubaby tena, hakuwa anajua kama namiliki bastola sasa atajua hata na bunduki ninayo, yani yeye mwenyewe akijitizama anakubali yaishe.
 
Akijipata ameshatekwa nyara hana ujanja, kinachofuata hapo ni ubabe sio ubaby tena, hakuwa anajua kama namiliki bastola sasa atajua hata na bunduki ninayo, yani yeye mwenyewe akijitizama anakubali yaishe.
Nani atakubaliana na huo ubabe sasa?
 
Back
Top Bottom