Kuna mikondo ya pesa wengi wetu hapa tunaisotea kwa udi na kwa uvumba! Wengine wanaroga kabisa ili waweze kuikamata. Kuna mitandao haramu ya biashara yenye faida za kufuru madini yanasubiri!
Vitenge biashara iliyohitaji elimu kubwa na uwekezaji wa wataalam ni biashara kubwa yenye mitandao ya kutisha inaguka kuwa biashara haramu sasa.. Maana watu wameshanogewa lakini mamlaka nazo sasa ndio zinakumbuka shuka asubuhi kukiwa kumeshapambazuka
Kuna nguvu ya kimamlaka inajaribu kuuvunja huu mtandao lakini bila kujitoa na kuongeza nguvu kubwa hawatafika popote. Watakamata vidagaa tuu na pumzi itakata
Ona hii magazijuto Kisha jiongeze!
Mwanamama kakamatwa Dodoma na mamlaka ya mapato kwa kosa la kutodai risiti ya mzigo wa vitenge alivyonunua .. Anashtakiwa kwa makosa mawili
1. Kutodai risiti
2. Kutotoa ushirikiano kwa maofisa alipotakiwa kuonesha mahali aliponunua mzigo
Huyu ni mbuzi wa kafara tuu... Hiyo mizigo wanaipata kimagumashi.. Mitandao ndio inafanya kazi..hakuna vituo rasmi ni kupeana juu kwa ju!
Siku mbili nyuma zimekamatwa gari na mzigo mkubwa wa vitenge mkoani lindi.. Mzigo haukuwa na nyaraka na ikasadikika ni mzigo wa magendo.. Mikwara mingi sana ikapigwa!
Mwezi uliopita zilikamwata container zenye mzigo wa kutosha wa vitenge .. Mzigo uliandikwa ni mashuka yako transit kumbe ni vitenge vinaenda kushushwa Tabata na wakahusishwa wazito hasa wakubwa
Tengeneza hilo picha la pyramid kuanzia Dar, Lindi mpaka Dom uone namna huo mtandao ulivyo mkubwa!
Je vijana wenye uchungu na nchi yao wanaojaribu kujitolea mustakali wao wauvunje huu mtandao wa biashara haramu ya vitenge watafanikiwa?