Dada siku izi biashara yataka ujanja na ina ujanja mwingi sana ukienda kwa pupa hivo vitenge utaviacha munzani......
Nimeona mtu kakushauri nenda mwenyewe fanya utafiti na mm nakushauri hivo.
Na ukitaka biashara biashara yako ya vitenge tumia malori kusafirishia Sababu kwenye bus ni lazima watakuchoma na hio gharama yake unaweza ukawaachia tu!!
Ushauri
K/koo ukiingia kwenye maduka ya jumla kuna vitenge vizuri na copy ni nyingi naona wadada wa mjini ndo wanaviuza insta!! Na huko burundi rwanda kigoma angalia sana wakiona hujui vitenge wanakuuzia feki inayofanana na original kwenye soko itakupa shida ukikutana na mteja anaejua vitenge.
Kila la heri katika mipango yako..