vitenge vya kigoma hutokea DRC hata Burundi wanavipata kutokea DRC, DRC au congo vitenge ni tsh 15000 bei ya jumla lkn vikishafika Burundi au Kigoma huuzwa 20000 tsh.
wauzaji wa kigoma watakueleza kabisa vitenge vya katoro au buseresere ni feki kwa kua ni wafanyabiashara wa kiganda huenda china kutoa copy ya maua na vinaingia kupitia ziwa victoria kimagendo.
sehemu za kufikia ni nyingi mfano ukifika maeneo ya BIMA mweleze mtu akupeleke zanzibar hill, hapo vyumba ni 20000 kuna usalama na ni karibu na mjini vinakopatikana vitenge, ujue kutofautisha zanzibar lodge na zanzibar hill
kusafirisha unaongea na makonda wa mabasi kama Saratoga au adventure hizi gari hupiga route za Dar kigoma ni rahisi kusafiri na mzigo hasa wkend days watakuchaji kwa boksi na mzigo wako utafika salama lkn uwe na uhakika wa njia yako
kwa wasafirishaji wa vitenge kwenda Arusha, Moshi , Manyara hutumia mabasi ya NBS au KIAZI KITAMU yanayofanya safari zake kigoma Arusha ni mara tatu kwa wiki.
Dada siku izi biashara yataka ujanja na ina ujanja mwingi sana ukienda kwa pupa hivo vitenge utaviacha munzani......
Nimeona mtu kakushauri nenda mwenyewe fanya utafiti na mm nakushauri hivo.
Na ukitaka biashara biashara yako ya vitenge tumia malori kusafirishia Sababu kwenye bus ni lazima watakuchoma na hio gharama yake unaweza ukawaachia tu!!
Ushauri
K/koo ukiingia kwenye maduka ya jumla kuna vitenge vizuri na copy ni nyingi naona wadada wa mjini ndo wanaviuza insta!! Na huko burundi rwanda kigoma angalia sana wakiona hujui vitenge wanakuuzia feki inayofanana na original kwenye soko itakupa shida ukikutana na mteja anaejua vitenge.
Kila la heri katika mipango yako..
piece moja ya pande tatu tumesema ni 23000 hadi 25000 hapo utapata variety za vitenge vingi na kuna vitenge mikoani huuzwa 30000 lakini kigoma bei ya jumla ni 14000 hadi 15000
nauli za kutoka Dar to Kigoma ni 60000 kwa basi kwa treni 37000tsh km sijasahau, Nauli za mwanza kigoma ni 27000 hadi 30000 kama sijasahau, Arusha kigoma ni 55000tsh hadi 60000tsh kama sijasahau.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.