Mchele super kutoka Kilombero

Mchele super kutoka Kilombero

mchele Super

New Member
Joined
Jul 1, 2026
Posts
3
Reaction score
1
BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM

Habari wana JamiiForums,

Natafuta mnunuzi wa jumla au mshirika wa biashara ya mchele.

Mimi ni mfanyabiashara mdogo kutoka Bonde la Mto Kilombero, Morogoro. Kwa sasa nina gunia 30 za mpunga tayari ghalani, na lengo langu ni kujenga ushirikiano wa muda mrefu na wanunuzi au wasambazaji wa mchele.

Mpunga ni mbegu ndefu, ikiwemo Mbawa Mbili na Kalimata, huku Sarro 5 ikiwa kwa kiwango kidogo. Hivyo ninategemea kupata mchele wenye ubora mzuri, nafaka ndefu na unaokidhi mahitaji ya soko.

BIASHARA HII NATARAJIA TUIFANYE SOKO LIKIWA ZURI KUANZIA NOVEMBER
Ninatafuta:

  • Mnunuzi wa jumla wa mchele.
  • Wakala au msambazaji wa mchele.
  • Mshirika wa biashara mwenye masoko ya uhakika, hasa Dar es Salaam.

Nipo tayari kujadili bei, namna ya usafirishaji na ushirikiano wa muda mrefu wenye manufaa kwa pande zote.

Kama una interest au unafahamu mtu anayehitaji mchele wa ubora mzuri, tafadhali nitumie DM.

Asanteni sana, na Mwenyezi Mungu awabariki.
 

Attachments

  • 20260629_151048.jpg
    20260629_151048.jpg
    678.1 KB · Views: 7
  • 20260629_223717.jpg
    20260629_223717.jpg
    529.7 KB · Views: 7
Back
Top Bottom