Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Ni too expensive
Upo Nchi Gani? Hivi unajua kutizama Mechi Banda Umiza ni 1000 iwe Mechi Moja double au Tatu kwa pamoja, na idadi ya watizamaji sometimes hufikia hata 100. Endapo wakiingia wateja 30 unaingiza elfu elfu 30 sasa kutizama Mpira ni gb kama moja au mbili.
 
Habarini za muda wanajukwaa wote.

Kwa uchache tu, mimi ni kijana ambaye ningependa kujihusisha na biashara ya kuonesha mpira kwenye "vibanda umiza" kwa maana ya mipira ya Bongo na Ulaya kupitia runinga.

Sasa ningependa kwa yeyote mwenye ujuzi ama uzoefu na hii biashara anipe mwongozo juu ya kiwango cha chini kabisa cha mtaji, gharama za awali na changamoto zake.

Nitangulize shukrani.
 
Inategemea banda unajenga la ukubwa gani unalipaje kodi ndan viti au mabenchi ya mbao au vipande vya miti(mabenchi yasiyohamishika) n.k

Lakini kuna gharama zilizo wazi kama ifuatavyo;

1.dishi mbili kwajil ya game za ndan na mbele-99k+135k=?
2.Tv flat atleast inch 32+ andaa japo 300k used kitonga
3.Kulipia packages 129k+18k=?
4.Spika-?

Inalipa sana ukipatia sehemu maana mpira ugonjwa ukishakuwa shabiki hutaki kupitwa, nina malengo ya kufungua hii mungu akinijaalia nimepata ushawishi kutokana na kuwa naokotaga ela ktk banda la anko
 
Kama ukiwa sehemu nzuri unatengeneza hela tafuta screen flat , pamoja na projector angalau moja mechi za usiku unaweza kutumia projector ...ukumbi ukiwa fulll

Pia nakushauri uwe na pannel angalau moja ya sollar watt 40 kwa ajili ya emergency umeme ukikata unatumia solar , tafuta decoder ya AZAMU ,NA DSTV NA DISH MOJA FREE TO AIR HD DECODOR

sent from toyota Allex
 
Kipengele chengine kipo kwenye ujenzi wa banda, gharama zake sijui zinakuwaje..
Maana kila nikitafuta sehemu ya kukodisha sipati
 
Hiyo paneli gharama yake ikoje? Maana kijenereta kidogo tu kuna sehemu nimeulizia wanauza kama 300 hivi
Sikushauli jeneretor panel na betri yake pamoja na chager controler ni laki 3 , generetor ndogo zinaua sana tv za flat .....halafu gaharama ya mafuta kumbuka hiyo ni kwa emegerncy

Kama nikiamua kuanza kiugumu ugumu itakuaje? Kuna uwezekano wa kuwapoteza wadau?
 
Chukua mchanganuo huu hapa Gharama ya ujenzi banda milioni 3 pamoja na mabenchi flatscreen kuanzia mbili za nchi 43 moja sh laki 6 dstv vinga'muzi viwili laki na 60 na package yake inadepend azamu ving'amuzi viwili laki 3 na package yake 36 startimes ya dish ving'amuzi 2 sh laki na 60 generator sh 400,000/= mafeni ya mtumba sh 40,000/= 1* chukua kuanzia 3 Mimi ndo biashara yangu since 2014 mpaka leo na ni biashara ambayo haina ushindani na inalipa kinyama kama utakuwa mvumilivu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inalipa sana naskia. Nina wadau wangu wanapiga hiyo nao.

Sasa kuanzia jenereta isipopatikana mambo yanakuwaje. Mana huu umeme wa bongo mzee ukisema uusubirie utapoteza wateja.

Nikisema labda niwe nakodi jenereta gharama itakuwaje?
 
Back
Top Bottom