Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Hapa naweza kucheki channel 2 kwa dekoda moja, kwenye dekoda niweke supersport 3 na kwenye laptop nicheki supersport 4 ???

Account moja ya DSTV now inasemekana(sijajaribu) inaweza tumika mpaka 4 devices simultaneously excluding ile inayotumia decoder...namaanisha wale wanao stream!

Account niliyonayo inatumika na watu wanne ambacho sijawa na uhakika nacho ni kama tunatazama simultaneously maana kila mtu ana interest zake!
 
Asante sana kaka kwa ushauri, japo nipo Arusha kwa sasa naona kama gharama ya TV na usafirishaji kwa ujumla itakuwa kubwa zaidi.
Mpambanaji nmefatilia huu uzi nasubir mrejesho kama umeanza kupga mzigo na vipi response ya biashara,kama bado usiliache wazo lako lifanyie kazi brother.
 
Mtaji kwa biashara hii unaweza ukaanza na sh m5 ujenzi wa banda milioni 2 tv za flatscreen mbili milioni 1.4 vinga'muzi vinne I mean vya dstv viwili cha startimes 1 na cha azam 1 vitakucost kama laki 7 plus na vifurushi vyake fedha itakayobaki kuna vitu vingine mafeni ya mtumba moja linauzwa sh40,000/*3 itakuwa sh 120,000/ kwa ajili kupunguza joto bila kusahau generator kubwa sh 400,000/ fedha iliyobaki utalipa kodi eneo ulilokodi
Vipi mapato kwa siku kama sehemu imechangamka?
 
Hivi hii biashara bado inauzika, kweli Tanzania ni kubwa, maana huku kwetu Mpitimbi watu wanaonesha mpira kwenye Bar kiingilio bia yako; unaonaje hilo eneo ukifungua bar ukawa unaonesha mpira ligi zote kubwa!!..ni wazo tu mkuu.
Kwenye banda la video unaweka vinywaji pia na movie za Kiswahili.
 
Kiongozi kwa kweli hii biashara mimi ilinishinda yaani nilikuwa nalipia 92 elfu kwa compact + halafu mwisho wa mwezi napata hasara kama ya 20 elfu hapo bado wananzengo wanakopa mechi kulipa ndo mbinde ila naumiza akili nikija kuibuka watanielewa tu kwa nitakachokifanya.
Ulifanyia town sana au?
 
mkuu,nipe uzoefu wa kutumia projector wkt wa mechi za mchana.
Kwa mchana epson eb s41 itakufaa, kwani ina resolution nzuri hata kunapokua na mwanga. Pia usitumie kitambaa kuoneshea kwani projector kwenye kitambaa haing'ai kama kwenye ukuta mweupe
 
Msaada nimenunua Led smart tv, najaribu ku connect n wireless kutoka kwa hotsport ya cm lkn inanambia "bad network, not in range" ilhali mtandao upo vizuri. Au nakosea kuunganisha?
 
Sio reliable, Mashabiki wenye hasira Kali wanaweza kuvunja TV ikianza kunata nata hasa timu ikiwa imefungwa. Na unaweza unaangalia mpira mwenyewe ikaonesha fresh tu Ila watu wakijazana kwenye Banda signal nazo zikaanza kuleta tabu na speed kudrop.

Kuna jamaa wa canal watu wanatumia Bei zao Ni affordable.

Pia DStv Wana DStv now unaweza ukajaribu kwa decoder moja na service ya DStv now uangalie Kama online inaweza kuwa nzuri.
Kama una uelewa mzuri na hii canal mkuu unisaidie nilitaka chukua hii je ina option ya kubadili lugha ya Uingereza yale matangazo ya mpira.
 
Kama Unaconnection direct ya Fibre cable unaweza la sivyo watakuua meku.

CTV wana connection ya fibre ila usichukulia masihara na Biashara. Utaharibu
 
Back
Top Bottom