Biashara ya hewa ya ukawa ina manufaa kwa mtu mwenye shamba dogo la miti?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,416
7,394
Nina shamba la ekari 21 mkoani Kigoma. Mwezi uliopita, nilimwachia mtu mmoja jukumu la kupanda miti kuzunguka mpaka wa shamba.

Nilipokuja kulikagua hivi karibuni, nilikuta kaotesha tofauti na nilivyomwelekeza. Kakata eneo la ekari tatu na kufanya shamba la miti.

Sikumgombeza. Wala sikumwonesha kuwa nimechukizwa na alichokifanya.

Muda mfupi baada ya kufika shambani, nilipata taarifa ambayo ilinifanya nimwone aliyeotesha miti kinyume na maelekezo yangu kuwa kafanya vizuri sana. Niliambiwa kuwa kuna Wazungu wanaozunguka mashambani kuandika majina ya watu wenye mashamba ya miti ili wawaweke kwenye utaratibu wa malipo. Kwa taarifa niliyopewa, hao Wazungu watarejea tena mwezi huu wa nne. Tayari nimeshaongea na mmoja wa wenyeji kuwa wajapo wakamwoneshe na la kwangu pia.

Hivi sasa ninataka niongeze tena miti mingine, eka moja miti ya MIKARIBEA na eka nyingine moja ya miti ya MIKARATUSI.

Kwenye ekari tatu zilizokwishaoteshwa, kuna miti iitwayo MITI KUNUKA ekari moja na MITIKI ekari 2.

Ninaipenda miti. Kwa hiyo hata kama hakutakuweko na hiyo program ya kulipwa, bado nitaendelea kuitunza kwa kadiri niwezavyo. Itakuwa na manufaa huko mbeleni.

Lakini kama huo mpango upo, ninaamini itanihamasisha kuongeza mashamba mengine ya miti. Fedha itakayopatikana kwenye hiyo program itasaidia kuuimarisha na kuupanua huo mradi wa miti.

Kwa hiyo, ninaomba mwenye taarifa anijuze yafuatayo:
1. Ni kweli huo utaratibu upo?

2. Kuna watu waliokwishanufaika na huo mpango?

3. Miti inayowekwa kwenye utaratibu wa malipo inapaswa kuwa na umri gani?

4. Kwa shamba la miti lenye ukubwa wa ekari moja malipo yake ni kama shilingi ngapi?

5. Malipo yanafanyikaje? Kwa mwezi au kwa mwaka ?

6. Miti gani inapewa lipaumbele katika malipo?

7. Mit ya matunda kama parachichi na miembe nayo inaweza kujumuishwa kwenye huo mpango wa malipo?

Ni hayo tu.

Naomba kuwasilisha!
 
Mmh mkuu ni kweli biashara hiyo ipo sana haswa Kwa mikoa ya rukwa ni kweli wazungu hulipa ila nahisi eneo liwe kubwa sana labda kina Sao hill watanufaika maana ingekuwa rahisi hivyo huku Lindi vijiji vina mapori makubwa vinahifadhi ila program hiyo haijawafikia mfano maeneo chini kidogo ya rondo plateu
 
Mods naomba heading isomeke "... HEWA YA UKAA..." na siyo "...HEWA YA UKAWA...".

Asante.
 
Mmh mkuu ni kweli biashara hiyo ipo sana haswa Kwa mikoa ya rukwa ni kweli wazungu hulipa ila nahisi eneo liwe kubwa sana labda kina Sao hill watanufaika maana ingekuwa rahisi hivyo huku Lindi vijiji vina mapori makubwa vinahifadhi ila program hiyo haijawafikia mfano maeneo chini kidogo ya rondo plateu
Sina uhakika sana na hilo mkuu, ila kwa jinsi nilivyoambiwa na wenyeji wangu, si lazima uwe na shamba kubwa. Hata aliyeniaimulia naye ana eneo dogo lakini aloshasajiliwa, ila malipo hayajaanza kufanyika.

Kwa kuwa imesemekana watarejea tena mwezi huu, ngoja nione kama na mimi nitasajiliwa.
 
Mmh mkuu ni kweli biashara hiyo ipo sana haswa Kwa mikoa ya rukwa ni kweli wazungu hulipa ila nahisi eneo liwe kubwa sana labda kina Sao hill watanufaika maana ingekuwa rahisi hivyo huku Lindi vijiji vina mapori makubwa vinahifadhi ila program hiyo haijawafikia mfano maeneo chini kidogo ya rondo plateu
Kuna mtu kanimambia leo kuwa ni kweli huo mradi upo pia Kigoma, lakini miti inayoingizwa kwenye utaratibu wa malipo ni yenye umri wa kuanzia miaka mitatu.

Ingawa anafanya kazi TFS, sijaamini alichoniambia kuhusu bei. Kasema kila mtu huweza kulipwa zaidi ya dola mia moja kwa mwaka.

Sidhani kama hilo ni kweli. Kachanganya mafaili. Dola mia moja kwa mti mmoja kwa mwaka ni hela nyingi.
 
Kuna kiasi kinalipwa ila kwa ukubwa wa eneo sidhani kwa mti mmoja
 
Kwa watu binafsi bado...vumilia kidogo Makampuni yanakuja

Kijiji kama kina msitu wa asili wenye miti iliyo shiba sio vichaka ukubwa zaidi ya hektari 20 kama unawanyama au miti kama Mpingo mninga nk = dili hiyoo
 
Back
Top Bottom