mpambanaji1
Member
- Dec 31, 2013
- 36
- 32
USHAURI: MTAJI, FAIDA NA USIMAMIZI
Nitatoa maelezo kulingana nauelewa wangu na uzoefu wangu japo si sana.
Kuhusu mtaji
Mtaji unatofautina kulingana na uwezo wa mtu as wapo wenye mitaji midogo na mikubwa! Wapo wanaoanza ata na laki 2 na kuendelea na wapo wasafirisha kupeleka huko Mtwara, Tunduma adi congo lakini hao ni wenye mitaji mikubwa na pia inahitajika uwe na soko ambapo ukichukua mzigo unajua utapeleka wapi nautakua ni kiasi gani cz huwezi kuchukua tu mzigo na kusema napeleka dodoma itakula kwako cz watu wengi wanakua wanachukua mizigo kwa oda na pia kulingana na soko alilonalo.
Kuhusu faida
Kiukweli dagaa inafaida tena nzuri tu sema inategemea na ukubwa wa mzigo na ubora mda unaokua umetumia kuanzia kununua, kusafirisha adi kuuza na pia wanaochukua mizogo mikubwa hua wanakua na faida kubwa na pia faida inatofautiana kulingana na mzigo uliochukua na bei ya soko unapouzia as bei zinatofautina sehemu na sehemu cz bei ya dom na Dar ni tofauti kabs kadhalika na masoko mengine.
Kuhusu uzimamizi
Usimamizi unahitajika sana hasa wakati wa ununuaji wa mzigo cz ndo wakti unapotakiwa kuangalia ubora wa mzigo nikimaanisha wa wawe wamekauka vizuri, wasiwe na mchanga mwingi na pia!! Usimamizi unahitajika wakati wa kupakia mzigo kwenye gari as mpakiaj anatiwa ahakikishe anamkabidhi dereva au mpakiaji kwa maandishi pia inatakiwa mpokeaji ajulikane na unakabidhi mawasiliano yako!!!! Vikwzo vipo kwenye sana kwenye kupata mtu mwaminifu ambaye unaweza kufnya nae kazi na pia mchanga hua unasumbua saaana.
Kwa maelezo hayo machache ni matumaini yangu kua mtakua mmepata mwanga na pia kama yupo mwenye maelezo ya tofauti au nyongeza anakaribishwa.
Kwa maelezo ziada kama bado unamaswali namba yangu nimeshaitoa call me me any time.
Karibuni