Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Kilahunja

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
1,502
341
Nina mtaji wa laki 3 na nusu, wakati natafuta ajira nimeona nijiajiri niuze chips, vipi mtaji unatosha? Any idea ya how to make them in a way it suits me (kisomi)?

Ushauri wenu unahitajika.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------
Maswali kutoka kwa wadau wengine kuhusu biashara hii


Habari wana jamii..
Ninashida ya kupata taarifa ya biashara ya chips.nimepata wazo hili na nina mtaji wa 1M, naishi dar na ninapenda sana biashara hii japo sina ujuzi. Yeyote mwenye kujua naomba anijulishe.
Asante sana.
Habari ndugu wana jamii forum,naomben msaada wa mawazo yenu juu ya kuendesha biashara ya chips na kuhakikisha kila mwisho wa siku unao mchanganuo mzuri wa faida na hasara
Naomba aliyewahi kuifanya aniambie changamoto zake kulingana na eneo alilowahi kufanyia. Nishanunua vifaa na nishampata dogo mmoja, sehemu kuna mchanganyiko wa watu na hela ya kulipia kibaraza sio kubwa maan ninaeka na kafriji!
Sasa nataka kujua ni mambo gani ya kuzingatia, lakini pia nilitaka niweke sehemu kubwa kidogo ila sijapata sehemu ambayo ni classic on the long run nitengeneze brand yangu ya chips, msaada!

Sasa tatizo jingine, nataka kujua changamoto za hii mambo. Japo hii ni biashara yangu ya pili ya msosi ila sio nyanja hii. Please msaada kwa aliyewahi ifanya!

================================================
Michango ya wadau kuhusu mchanganuo wa biashara hii
================================================


1596522140441.png


Jijini Dar es salaam karibu kila mahali utakuta mabanda ya kuuzia chipsi, kwenye maeneo ya kuuzia vyakula kama, migahawani, grocery za bia, mabaa na kuzunguka maeneo mbalimbali ya shule na vyuo.

Kwa ujumla mahitaji ya chakula hiki, chipsi ni makubwa sana kushinda vile mtu unavyoweza kufikiria, na wateja kuna vitu vikubwa vitano vinavyowafanya wanunue chipsi mahali fulani na kuacha mahali pengine, vitu hivyo ni hivi hapa; kwanza Usafi, pili huduma nzuri, tatu ni ufungashaji mzuri, nne ubora na tano ni bei.

1. USAFI.
Usafi ni kigezo kikubwa sana kwa mteja kupenda kununua chipsi mahali fulani na kuacha pengine. Unaweza kukuta mahali fulani wateja hawakauki na wanaweka hadi foleni kusubiria chipsi ili-hali jirani tu kuna mabanda mengine yanayouza chipsi kama hizohizo. Usafi kuanzia wahudumu wenyewe, vyombo mpaka meza na mahali wateja wanapoketi wakila ni muhimu sana. Usafi unatakiwa kufanywa kila siku na kwa ukamilifu wake.

2. HUDUMA NZURI KWA MTEJA
Ukarimu wa watoa/mtoa huduma, ni jambo muhimu mno, wateja hawataki ukali ukali usiokuwa na maana, mteja muda wote anatakiwa achukuliwe kama mtoto mdogo, kamwe haitakiwi aonekane mkosaji, hata ikiwa ana makosa. Kuchukuliwa kwa upole, anaweza akaomba aongewzewe 'vichipsi' kidogo na muuzaji mwenye busara atampa japo punje moja ama mbili naye ataridhika na kesho atarudi tena.

3. UFUNGASHAJI.
Zamani wauza chipsi wengi walizoea kufungia wateja chipsi wakitumia makaratasi ya magazeti yaliyotumika au mifuko ya plastiki maarufu kama mifuko laini. Lakini kwa sasa hivi muelekeo umebadilika baada ya watu wengi kuwa na elimu ya kutosha juu ya madhara ya mifuko ya aina hiyo. Wateja sasa wanapendelea zaidi chipsi zilizofungashwa kwa karatasi ya aluminium(foil). Ukiziweka zinavuta wateja.

4. UBORA.
Ubora hapa ninamaanisha chipsi na mayai au kuku kukauka vizuri, mishikaki iliyoiva sawasawa, kachumbari iliyotayarishwa katika hali ya usafi pamoja na viungo vingine kama vile tomato sauce, pilipili, karafuu nk.

5. BEI.
Kuna wanaoangalia pia bei, ikiwa ni bei ya wastani basi wapo tayari kununua lakini inapokuwa juu sana ya wastani, utawasikia wakisema “anafikiri anawauzia watalii hapa”.
Lakini ukiacha utamu wote huo wa chipsi na vivywaji baridi kuna kitu kimoja cha hatari sana, kinachohusina navyo.Vyakula hivi ni muuaji wa taratibu (silent killer). Ulaji wa chipsi mayai, kuku wa kisasa, chumvi kupita kiasi, sukari kupindukia, mafuta mengi na hata nyama nyekundu unahusishwa kwa kiasi kikubwa na magonjwa makuu ya tabia yakiwamo, kisukari, shinikizo la juu la damu, kansa na kiharusi.



Kijana kwanz umefanya vizuri kuomba ushauri, achana na watu wenye mawazo mgando, mimi ninauzoefu kiasi flan juu ya biashara ya chips. Biashara ya chips inaweza ikakulipa sana tu bt katika mazingira ya fuatayo mbali na mtaji.

1: LOCATION: hiki ni kitu cha msingi sana unaweza kuwa na mtaji wa kutosha bt ukikosea location inakula kwako-tafuta hasa eneo ambalo lina traffic ya watu au sehemu za biashara na maofisi:

2: Usimamizi wa karibu-usimamie wewe mwenyewe au mtu wako wa karibu sana la sivo vijana watakuliza, kuwa makini kutafuta vijana wa kukusaidia kazi zingatia hasa uaminifu.

3: Good customer care na ubunifu kwenye biashara: ukizingatia haya biashara hii inaweza kukulipa net profit ya laki mbili kwa siku :

NB itatemeana na eneo utakalotafuta bt m3 inatosha sana
BIASHARA YA CHIPS IPO HIVI
Biashara hii inafanywa kwa makubaliana ya kumpangishia kijana mahala pakufanyia kazi,mahitajio yote muhimu km viazi, kalai, sahani, jiko, mafuta na pesa, tomato na vingine ikiwezekana na pesa kidogo ya dharura..

sasa kinachotakiwa kwenye mkataba wenu ni kwamba yeye aendeshe hiyo biashara anavyojua yeye ameuza hajauza lazima akupe kiasi fulani ambacho ww utakiona kitafaa kukulipa kwa mtaji uliouanzisha, malipo mtalipana kwa jinsi eneoo la biashara litakavyokuwa aidha kwa siku au kwa wiki is it up to nyinyi..

HAKUNA HAJA YA KUMFATILIA WEWE FANYA SHUGHULI ZAKO,ikifika muda wa kukupa fedha yako fasta usichelewe nenda kaichukue...km itakuwa anakupa pungufu ya ile mliokubaliana mvumilie kwa kipindi fulani tu nasi mda mwingi,lingine hakikisha unapata muda wa kuhakiki mtaji km unaendelea vizuri.
Mtaji wa 1M kwa chips Dar es salaam ni mdogo kv ukitaka eneo zuri hiyo 1M inaweza kuishia kwenye kukodi eneo! Kwa mfano, kodi ya laki 1 kwa mwezi utapata eneo la kawaida sana ambalo linaweza lisiwe na biz mzuri! Na hata ukipata eneo zuri kwa hiyo bei, hapo utahitaji laki 7 kulipia ( + laki ya dalali ) which means kwenye 1M unabaki 300K!

Kufanya biashara ya chips kisasa unaanzia na mazingira; which means hiyo 300K itaishia kwenye kuandaa mazingira bora na ya kisasa!!
Kutokana na huo mchanganuo utaona ni namna gani 1M isivyotosha!

REMEMBER: Bei ya laki 1 kwa mwezi utapata eneo la kawaida sana!! Mbaya zaidi; wamiliki wa haya maeneo ya kawaida ni maskini wenzetu lakini waliojawa tamaa! Wewe mwenyewe ukishaona tu biz inaenda vizuri basi jiandae kutafuta eneo lingine kv anaweza kukuchomolea kuongeza mkataba!! Anaona unapata kwahiyo anaingia tamaa wewe uondoke afanye yeye/wao wenyewe!
 
Laki 3, yaweza tosha kwa kuanzia tu japo mradi wako hautakuwa na mvuto sana mfano muonekano wa banda, vyombo kwa mfano kabati zuri la kioo pekee ni laki unusu, meza, viti, jiko n.k...i thnk umenielewa kwamba u can localy bt nt modernly.

Thanx, bt stafs like meza, viti na mahitaj mengne ntachukua home cz my mama ana duka so alinunua meza na vit vya kutosha, kabat la kioo nshapata la laki moja, futi 2.
 
Ushauri mzuri ukipata sehemu ambayo unaweza kuuza viazi kwa debe kwa siku mbona utafurahi maishani kaza mwendo kamanda kazi inalipa sana hiyo.

Thank u dear one..(kuna kijana ntamuweka), am a gal so nimetafuta kijana ninae mfaham ambae ana xperienc na iyo k2.
 
Habari wana jamii.

Ninashida ya kupata taarifa ya biashara ya chips.nimepata wazo hili na nina mtaji wa 1M, naishi dar na ninapenda sana biashara hii japo sina ujuzi. Yeyote mwenye kujua naomba anijulishe.

Asante sana.
 
Habari zenu wanaJF,

Ebwana mimi ni graduate wa mwaka 2013 katika course ya banking and finance (degree) from IFM, nimetafuta internship katika benks bila mafanikio nakama kigezo ni gpa nina overall gpa ya 4.1 , hivo ninafikiria kufungua banda la chips, wadau ninaomba mawazo yenu juu ya hii biashara ninayo fikiria, what should i put in my business to attract customers.

My contact ni +255719058458
 
By tpmazembe
wewe graduate wa finance na banking unahitaji ushauri wa kufungua banda la chips kweli?


Ni kweli anahitaji kwa sababu si hypocrite. He is being honesty with himself.

Mpen sa ushauri mwenzenu kuna utofauti wa elimu ya darasani na reality, so his degree shouldnt prevent him from asking for ushauri.aftall they say aulizae c mjinga.
 
Chipsi inalipa mbona mie mpishi nimesoma nje nimerud tz nauza chps kama nilizokua namlisha mzungu nimeboresha sio kabanda nimechukua frem nafanya mambo ndani. Mfano hai nenda uwanja wa taifa kuna rasta anauza chips na source za ajabu ule ujuzi aliupata kwa wa portugues .

Mkuu nenda pale minazini bar ongea na yule ras gebo ndo bosi we mwambie kanipa maelekezo ras dona mueleze mawazo yako na angalia mapish yake viungo vya kuku na vingine venye umuhmu kila laheri.
 
chpz inalipa mbona mie mpishi nimesoma nje nimerud tz nauza chps kama nilizokua namlisha mzungu nimeboresha sio kabanda nimechukua frem nafanya mambo ndani.mfano hai nenda uwanja wa taifa kuna rasta anauza chips na source za ajabu ule ujuzi aliupata kwa wa portugues .mkuu nenda pale minazini bar ongea na yule ras gebo ndo bosi we mwambie kanipa maelekezo ras dona mueleze mawazo yako na angalia mapish yake viungo vya kuku na vingine venye umuhmu.kila laheri

Dah haya ndo maneno sasa ushauri ka huu ndo mpango mzma.c maswala yakukatisha tamaa.
 
Wana jamvi,
nna shilingi laki nne nataka nianze biashara ya chips ,kwa aliye na uzoefu naomba anipe mchanganuo na kama mtaji huu utatosha!
 
Mkuu Habari,

Unaweza kuongeza details zaidi ili iwe rahisi kutoa ushauri. Umefikirria kuhusu haya yafuatayo?

1. Una sh laki nne, Je una mahali pa kufanyia hiyo shuguli tayari ama unataka kukodi? Hapo utakapo kodi kuna gharama za ziada? (Umeme, Ulinzi.. n.k) unaa vifaa vya kufanyia hiyo shuguli.

2. Soko lako umemlenga nani, wanafunzi wa chuo? Mtaani kwenye bar? Ama maofisini mchana?

3. Mzigo wako wa viaizi utautoa wapi? Kariakoo? Ama watu wa malori wa pale manzese utakuwa ukiwaagiza?

4. Umepata nafasi ya kutembelea mtu anayefanya kazi kama hiyo kwa sasa kubadilishana mawazo ili ujue changamoto zilizopo kwa sasa na jinsi utakavyozikabiri?


Shukrani,
 
Mpen sa ushauri mwenzenu kuna utofauti wa elimu ya darasani na reality, so his degree shouldnt prevent him from asking for ushauri.aftall they say aulizae c mjinga.
tpmazembe,
kwani i ajabu kama yeye ni graduate na akauliza?kama ukisoma vitafu utaona bussiness is something ese. sio kitu rahisi kama unavyokifikiria na ukadhani elimu inaa plly kila mahali, vitu vingine ni lazima uulize wazoefu kwani si kila kitu ni darasani unapata.so the guy is right ro ask anything bwana,
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom