Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Assalamualaikum warahmatullah wabarakatu kwema ndugu zangu mi Nina changamoto Moja nafanya biashara ya chips lakini tangia nianze hakuna faida yyte ninayopata sasa nilikuwa naomba msaada wa ushaur Nini nifanye kuboresha biashara yangu Ili nipate faida
Location yako ni wapi?

Mtaji wako kiasi gani?

Mauzo yako ni kiasi gani kwa siku na ulipendelea kuuza kiasi gani?

Una muda gani tangu kuanza kwa hiyo biashara?
 
Hodi wanajamvi....
Nianze kwa kutoa shukrani za dhati kwa jukwaa hili kwani naanza kukuona mwanga japo Kuna kigiza katika kuisimamisha biashara yangu ndogo..
Nianze kwa kutoa story fupi Kwanza..

Mimi Sina uzoefu katika kufanya biashara yoyote Ila nimekua na mawazo ya kuanzisha biashara na ndipo mwaka huu nikafanikiwa kuanzisha genge dogo kwa ajili ya chips ikiwa ni safari ya kuelekea kufungua Fresh Pub kwa ajili ya juice na maziwa tu hii ndio ndoto yangu kibiashara.

Basi nikapata kijana Analia shida sana kwani siku Kama 34 nyuma Tajirii yake aliyumba hivyo akawa Hana kazi tukapambana tukaanzisha biashara hiyo ya chips ambayo kwake yeye ni mzoefu wa muda mrefu na anajulikana sanaaa kwa Hilo eneo.

Sikutaka kumbana Kama kijana mwenzangu nkampa Uhuru na swali lilikua JE UTANIPA SHILINGI NGAPI KWA SIKU KWA UWEKEZAJI HUU...??
MAJIBU YAKE YAKAWA NI 25,000/- nikamuuliza unauhakika Hapo utapata pesa pia kuendesha maisha yako?? Akajibu NDIO pasi shaka... TUKAANZA KAZI Kama siku 20 nyuma.

Mwanzo ukawa nzuri hela ikaanza kuflow Kila siku sa tatu asubuhi anatuma Ila sasa siku Kama 6 nyuma Mambo yameanza kubadilika hela haiji kwa wakati... Kijana anasumbua Mara mi sipati chochote....
Mara wenzangu wananiloga Mambo mengiii na siku zingine hatumi chochote... Jamaa ni mshikaji Ila ananizingua...

Kwa ufupi kwa siku
Anauza kilo 30 za viazi
Mayai kati ya trei moja na nusu Hadi mbili
Nyama kilo tano
Samaki hapa inategemea na siku
Ndizi za kukaanga

Wajuzi nisaidieni hapa huyu mtu anaingiaza kiasi gani Ila ameshindwa kuzalisha 25k tu.

Leo nimegombana nae sanaaa nawaza kumtimua au la nimpelekee mtu wa mauzo na manunuzi abaki kuwa mkaangaji tu.

Wadau hebu nishaurini nini nikifanye kiukweli eneo Lina mzunguko mkubwa wa pesa na watu pia Ila huyu kiumbe ananikwamisha na mbaya zaidi huku Sina ndugu na Mimi muda wa kusimami sina
Nadhani hapo umempa mpishi kazi ya uhasibu so akiziona pesa anazuzuka. Kuna watu wapo hivyo hawana uwezo wa kujicommit na kujicontrol hadi wapelekeshwe kama punda.

Kosa unafanya ni kukogambana na mtu ambaye ni muajiriwa wako, umeona wapi CEO anagombana na mfagia ofisi au karani wa kampuni.

Tafuta vijana wengine wa ziada ambao utawaamini, m'moja mpe kazi ya kuchukua oda na kuwapelekea wateja yaani kama waiter na mwingine mpe kazi ya kuchukua pesa na kurejesha chenji.

Shida ya wajasiriamali wanataka waone biashara ikikua ila gharama za uendeshaji zikibakia pale pale bila kupanda hata mia.
 
Kuna braza mmoja nilimweka kwenye hicho kitengo, sasa kwenye mishe zangu nikuwa narudi jioni. Ninapofika naona yupo busy balaa ila ananiambia leo mdogo wangu hali mbaya yaani wateja ndio wameanza kuja sasa hivi wewe unapofika.
Kila siku ikawa hivyo hivyo. Lakini cha ajabu utakuta muda wa usiku amekaa na warembo wanapiga banana wakati anasema hali mbaya.
Sasa kuna siku nilimwotea, nikaondoka asubuhi, halafu ghafla nikarudi. Duh! Nikaona jamaa amenunua maviazi mara 2 na nusu ya kawaida wakati hela niliyomwachia ni chache. Hiyo siku nilikomaa naye nikamlamba na faida ya viazi alivyonunua kwa hela yake na akshindwa kunibana.
Kuanzia hiyo siku tukapigiama hesabu alete kumi na tano per day na ndio ikawa suluhisho la kuibiwa.
Dah ingawa huu uzi ni wa muda mrefu ila nimecheka balaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom