Biashara ya Bond za magari iko vipi?

Biashara ya Bond za magari iko vipi?

So kunaweza kuwa na gari Yard Dar. Mtanzania na Mzambia wakazinunua kwa bei moja. Mtanzania akapigwa kodi na TRA na Mzambia akaenda nayo kupigwa kodi huko kwao akalipia tu kuivusha kwenda kwao?
Ulikuwepo huo mtindo ila ulikuwa na mwanya wa kukwepa kodi, Tra wamekuja na sheria inayomtaka kila mtanzania anayeagiza gari nje aambatanishe na Tin namba yake kwenye documents za manunuzi.
Zamani wenye yard walikuwa wnaaagiza magari wakisema ni ya transit hawalipi kodi halafu wanayauza hapahapa kimchongo, siku hizi kilangari inayoshika melini inajulikana inakokwenda.
 
Kumbe kwa uwepo wa hizi bonded warehouse hamna haja ya mtu gari yake kuuziwa bandarini.
Yeah
Ile presha ya kusubiri document na kuogopa storage siku hizi ni labda utake tu mwenyewe. Kwanza dp world storage anaanza kuhesabu siku ya tano tu sio saba . Pia napandisha sana gharama za storage, kuna magari ukiona limekaa mwezi bandarini gharama za storageni bora uliache tu ununue jingine.
 
Bond warehouse ni dhamana ambayo mfanyabiashara anaipata kupitia Bima na ambayo kiasi cha dhamana urakayoweka ndio itakupa uwezo wa idadi ya magari utayoweza kuweka kwenye hiyo warehouse yako..

Bond warehouse ya magari haisumbui kuipata tofauti na ya vitu tofauti tofauti.
Sifa za warehouse iwe ni eneo lililozungushiwa ukuta TRA wana vipimo unavyotuhusiwa na iwe na ofisi ndogo kwa ajili ya kutunza taarifa za hiyo warehouse na wao wakitaka kuja iwe rahisi kwao pia..

Unaweza ukawa unanunua magari nje na kutunza kwenye warehouse yako unafanya kuongeza muda kama gari haijapata mnunuzi kila baada ya miezi sita hawawezi kupiga mnada gari iliyo chini ya dhamana kinachotakiwa ni kutoa taarifa sahihi tu.

Kwa kuwa na eneo la dhamana pia unaweza kuchukua gari za wafanyabiashara wengine au walioagiza gari nje na kutunza kwenye warehouse yako huku ukiwachaji gharama kwa mwezi hata usd 200 ambayo haiupunguzi kitu kutoka kwenye bond uliyowekewa na bima kupitia TRA..

Kwa kodi za TRA sasa hivi kuwa na bond ni moja ya biashara nzuri kwa Watanzania..
 
Niongeze swali. Ikitokea mtu ana yard. Ananunua magari Japan kwa ajili ya kuyauza nje ya nchi, huko Zambia, Malawi etc. Kabla hao wamalawi au wazambia hawajaja kununua, mwenye yard anayalipia kodi TRA?
Kwa mfumo wa kodi wa sasa kila mtanzania anayeagiza gari ni lazima litumike hapa hapa.
 
Back
Top Bottom