Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,582
- 46,180
Serikali imekuwa ikijinasibu kufanya biashara mbalimbali kwa lengo la kujenga uchumi, kusaidia raia wake, uzalendo n.k. Tumeshuhudia serikali ikejenga hotel za kitalii, ikimiliki mashamba, viwanda vya dawa, ikinunua korosho,na ikiendelea kwa kasi kununu ndege kuendelea na biashara ya usafiri wa anga.
Tatizo ni kwamba hizi biashara zote serikali inazofanya haziyagusi maisha ya mwananchi wa kawaida moja kwa moja na pia serikali haijawa na haitakuwa na ufanisi kufanya biashara za aina hii.
Biashara ambayo serikali ingejikita kuifanya na ikawa na mguso wa moja kwa moja kwa wananchi walio wengi ni ya kujenga nyumba za kupanga kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kati na chini.
Tanzania inakabiliwa na uhitaji mkubwa wa makazi bora na ya bei nafuu hali inayofanya raia wengi hasa wafanyakazi kukimbilia kununua viwanja na kujenga nyumba kwa muda mrefu hata kwa mikopo ghali. Hali hii si nzuri katika kukuza uchumi kwa kasi sababu kiasi kikubwa cha pesa ambazo zingetumika kama mitaji kupitia uwekezaji wa kibiashara katika sekta nyingine kinazikwa chini kupitia ununuzi wa viwanja na ujenzi wa muda mrefu sana.
Badala ya kupeleka matrilioni katika ndege serikali ijenge nyumba ambazo ni chanzo cha uhakika wa uwekezaji kurudi huku maisha ya raia wengi yakiboreka.Nyumba hizo za serikali zipangishwe na ziwe zinalipiwa kwa mwezi 1, miezi 2,3,4,5 n.k kulingana na kipato cha mpangaji husika.