Biashara stahili kwa Serikali ni kujenga nyumba bora za bei nafuu za kulipia kwa mwezi mmoja mmoja

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,581
46,176
Serikali imekuwa ikijinasibu kufanya biashara mbalimbali kwa lengo la kujenga uchumi, kusaidia raia wake, uzalendo n.k. Tumeshuhudia serikali ikejenga hotel za kitalii, ikimiliki mashamba, viwanda vya dawa, ikinunua korosho,na ikiendelea kwa kasi kununu ndege kuendelea na biashara ya usafiri wa anga.

Tatizo ni kwamba hizi biashara zote serikali inazofanya haziyagusi maisha ya mwananchi wa kawaida moja kwa moja na pia serikali haijawa na haitakuwa na ufanisi kufanya biashara za aina hii.

Biashara ambayo serikali ingejikita kuifanya na ikawa na mguso wa moja kwa moja kwa wananchi walio wengi ni ya kujenga nyumba za kupanga kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kati na chini.

Tanzania inakabiliwa na uhitaji mkubwa wa makazi bora na ya bei nafuu hali inayofanya raia wengi hasa wafanyakazi kukimbilia kununua viwanja na kujenga nyumba kwa muda mrefu hata kwa mikopo ghali. Hali hii si nzuri katika kukuza uchumi kwa kasi sababu kiasi kikubwa cha pesa ambazo zingetumika kama mitaji kupitia uwekezaji wa kibiashara katika sekta nyingine kinazikwa chini kupitia ununuzi wa viwanja na ujenzi wa muda mrefu sana.

Badala ya kupeleka matrilioni katika ndege serikali ijenge nyumba ambazo ni chanzo cha uhakika wa uwekezaji kurudi huku maisha ya raia wengi yakiboreka.Nyumba hizo za serikali zipangishwe na ziwe zinalipiwa kwa mwezi 1, miezi 2,3,4,5 n.k kulingana na kipato cha mpangaji husika.
 
Miradi ya NSSF nyumba zimetelekezwa, Watumishi House na zile za gharama nafuu ziko tayari pale Morocco Square.

Kaguse uone hiyo bei yake inayoitwa gharama nafuu.
 
Haiwezi kusimamia miradi ya namna hiyo. Wafanyakazi wasio na huruma wala maadili kwa wananchi hawawezi kusimamia mradi wa namna hiyo kwa haki.

Wakurugenzi wasimamizi watahodhi hizo nyumba na gharama za upangaji zitaongezeka na mwisho wa siku watapangishiana wenyewe kwa wenyewe.

Hivi wewe bado ni mgeni hapa Tanzania?
 
Hii inakuwa ni biashara ya shirika la nyumba na shirika ndilo linakuwa mtafutaji mkuu wa vyanzo pesa vya hiyo miradi kupitia mabenki na ufadhili na sio kutegema pesa za serikali, shirika pia lihusike kuhakikisha linakusanya mapato stahiki. Hii ni biashara rahisi sana kwa serikali isiyohitaji akili wala nguvu kubwa .
 
Wazo bora sana ndugu yangu umeliwaza.
Lakini wasiwasi ni aina ya muundo wa serikali yetu hii kama kweli wana nia ya kugusa mwananchi wa hali ya chini katika muktadha wa kumuinua.

Badala yake imeweka kila sababu ya kumkandamiza chini na wale wenye afadhali ndio wana zidi kuwa bora.

Nyumba za shirika la nyumba la taifa hazigusiki kwa mwananchi wa kawaida, nina mfano wa nyumba za Bunju mabwepande huku, nyingi zimetekelezwa na zimekuwa magoti lakini kuna watu hawana uhakika wa kupata nyumba bora ya kuishi.
 
Hii inakuwa ni biashara ya shirika la nyumba na shirika ndilo linakuwa mtafutaji mkuu wa vyanzo pesa vya hiyo miradi kupitia mabenki na ufadhili na sio kutegema pesa za serikali, shirika pia lihusike kuhakikisha linakusanya mapato stahiki. Hii ni biashara rahisi sana kwa serikali isiyohitaji akili wala nguvu kubwa .
Hicho kitu hakiwezekani ndugu yangu. Lini umewahi kuona shirika lolote la serikali lenye manufaa kwa wananchi wa hali ya chini?
 
Unajua NHC kazi yake ilikuwa nini na ilipaswa ifanye nini kabla ya watu kuibadilisha eti ianze kufanya biashara ?

Anyway mwisho wa siku, siku si mbali tutakwenda tu kwenye mfumo wa Mortgage huenda kujenga isiwe tena viable..., mwendo wa tozo na gharama za majengo maintanance n.k. usishangae baada ya miaka kadhaa watu kukimbia nyumba zao..., na ukifa ukiacha urithi nyumba kwa mtu wako (panga la kodi linakuhusu pia) huko ndio tunakoelekea... Uchumi wa Juu!!!!
 
Hii inakuwa ni biashara ya shirika la nyumba na shirika ndilo linakuwa mtafutaji mkuu wa vyanzo pesa vya hiyo miradi kupitia mabenki na ufadhili na sio kutegema pesa za serikali, shirika pia lihusike kuhakikisha linakusanya mapato stahiki. Hii ni biashara rahisi sana kwa serikali isiyohitaji akili wala nguvu kubwa .

Kwa serekali ya CCM hakuna litakalokua mkuu
 
Back
Top Bottom