Biashara mpya Tanganyika: Majeneza used

Biashara mpya Tanganyika: Majeneza used

image_3845fa12.jpg
 
Majeneza ya Kukodi (Casket Rental).. Haya ni sawa na kusema ni 'used'

Kitu pekee kitu pekee sana na chenye faida kubwa lakini hakipatikani kwa urahisi nchini Tanganyika.. Hiki ni kile kinachojulikana kama Rental Caskets (Majeneza ya Kukodi), ambayo hutumiwa zaidi katika nchi za Magharibi:
  • Jinsi yanavyofanya kazi Familia hukodi jeneza la kifahari kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili (viewing/funeral service).
  • Ndani yake: Mwili huwekwa ndani ya sanduku maalum la mbao hafifu au kadibodi (cardboard box/liner) ambalo ndilo huingizwa ndani ya lile jeneza kubwa la kifahari la kukodi.
  • Baada ya ibada: Lile sanduku la ndani lenye mwili hutolewa na kwenda kuzikwa au kuchomwa, huku jeneza la nje la kukodi likisafishwa na kusafishwa kwa dawa (disinfected) ili likatumiwe tena na mtu mmwingine
Je mnaonaje hii biashara wakuu.. Haina tofauti sana na magari ya kukodi kwenye sherehe ama magauni ya kukodi

CC: Muuza Majeneza Used

Pia soma:
(1,758) Majeneza ya kukodi na makaburi ya kupanga | Page 2 | JamiiForums Tanzania https://share.google/cLc9voUXgSsc4xVaEView attachment 3670655View attachment 3670525
Idea nzuri, labda nisichoelewa, ni kipindi gani katika mazishi ambacho hayo hufanyika?

Je hilo jeneza la kukodi huingizwa hadi kaburini ndipo lile jeneza la kuzikia huondolewamo kubakia kaburini kuzikwa?
 
Idea nzuri, labda nisichoelewa, ni kipindi gani katika mazishi ambacho hayo hufanyika?

Je hilo jeneza la kukodi huingizwa hadi kaburini ndipo lile jeneza la kuzikia huondolewamo kubakia kaburini kuzikwa?
La kukodi linabeba la kuzikia mpaka pale kaburini.. Wakati wa mazishi lile linaondolewa linabaki linaloenda na mwili..

Ni idea nzuri kwakweli
 
Back
Top Bottom