Biashara Jamani.

Kibwagizo

Senior Member
Mar 21, 2012
130
8
Nina kamtaji kangu kama 5,000,000.00.Wabunifu wa biashara msaada wenu.Biashara ipi inalipa.Help please
 
Nina kamtaji kangu kama 5,000,000.00.Wabunifu wa biashara msaada wenu.Biashara ipi inalipa.Help please
 
wakubwa ni tatizo la mtandao ukiwa down.Isipo kubali mara moja unajikuta ukirudia kumbe ndo matatizo ya post kujirudia.I'm sorry.
 
Ahalan wa sahlan maalim. Wazo zuri lakini, nafikiri ingekua bora urudishe hizi fedha huko ulikozikopa. Pindi upatapo hio biashara au shughuli unatayoamua kuifanya, rudi ukazikope tena. Unajua fedha fedheha, bwana.

Halafu ustadhi, ningependa kujua kitugani, au jambo gani wewe hapenda kufanya unapokua hauko kazini? yaani kitu ambacho unaweza kufanya bure bili kulipwa hela na ukaridhika? kwa mfano kuingia mtandaoni ni moja wapo. Kuna Jamaaa aliwahi nambia yeye hupenda kukutana na gurupu lake wakaimba nyimbo na kumsifu Bwana.
 
Jaribu hii mkuu kutokana na mtaji wako bado ni mdogo na bado haujakomaa kibiashara(uzoefu) unaweza kufanya biashara ya mahindi kutoa vijijin na kwenda kuuza maeneo ambayo bei ni kubwa,au mayai unanunua kwa jumla kijijin na upeleke mjin au matunda ni ww tu kuangalia ipi inalipa haraka ila usipende kuanza mwenyewe tafuta mzoefu wa biashara hiyo na umuombe ufanye kujiweka ubavun kwake mfano kama ni mahindi unaongea nae mnaweka kwenye gari moja bei itapungua na ukifika sokon umuombe akuunganishe na wateja wake paka utakapo pata uzoefu.ni ushauri tu si lazma kuufuata
 
Kwa hako kamtaji kako ulikokopa, inflation ya JK, tena hujui ufanye nini... Jiandae kwa kuuzwa kwa ile dhamana uliyoiweka kwa ajili ya mkopo. Kwa sababu wewe ni MPUUZI, katika dunia ya leo huwezi kopa fedha wakati 'hujui utaifanyia nini'... Umenikera sana!
 
Mi siamini ktk mtu kumbunia biashara mtu mwingine, ila inataka kwanza, ufikiri cha kufanya then pata ushauri na utafiti makini wa kile unachoamini unataka kufanya, then tafuta fedha kutokana na vile ulivotafiti kwa makini baada ya hapo anza kuifanya hio biashara, huwezi kufanikiwa sana kwanza kwa kuwa na fedha then uanze kutafuta cha kufanya. Biashara ni zaidi ya fedha, panga kwanza tena fanya utafiti wa kutosha, sio umeenda kwa kinyozi Jumamosi ukakuta watu wengi wananyoa na wengine wanasubiri ukadhani hii biashara ni nzuri ili uwe na uhakika nenda J3,j4,5,alhamisi, ijumaa na jumapili, mwanzo wa mwezi na kati na mwisho wa mwezi, usiige biashara wala usiongozwe na biashara yenye faida kubwa ina risk kubwa pia, Pia nilazima uipende hio biashara, na fanya ukiamini ndiyo hiyo itakayokutoa usiwe na tamaa ya kubadilibadili biashara, Yapo mengi na wengi wamefanikiwa sana na Ukumbuke kutoa sadaka kwa kuombea kile unachotaka kufanya, usitoe kama Mungu ni Maskini) eg, Bwana Mungu Natoa Sadaka hii iwe mbegu bora yenye kuzaa matunda mengi na yenye manufaa kwangu na jamii yangu.) na utakapotaka kufanya Biashara yako na Uombe kwa kusema, Mungu naomba uikumbuke sadaka yangu na Kuitabakari) basi utafanikiwa sana.
 
Na mimi nataka kufanya biashara ya mkaa niko mbezi beach Tangibovu. Naombeni msaada ni vipi nitapata mkaa wa bei nzuri. Kama kuna mtu anasupply mkaa ni Pm tafadhali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom