Biashara ipi ya kuwekeza kipindi hiki kwa mtaji wa milioni 30 -50?

Biashara nzuri unatakiwa kuwekeza kweny kituo cha afya cha eternal kitakuwa kinakuingizia hela kila siku pamoja zawadi nyingi waweza nitafuta kwa namba 0672295499 nikuelekeze hiyo fursa ya kufungua kituo na faida zake
 
DM nikupe fursa ya kufungua kituo cha afya ambacho kitakuwa kinakuingizia million 20 na zaidi kwa mwezi
 
Achukue baadhi ya hizi ....

1.Aje Dodoma afungue kiwanda cha kufyatua na kuuza tofali,hii biashara inalipa sana watu wanajenga balaa kwa Dodoma,hapa anaweza kuweka na ki min shop cha hard ware.location zipo nyingi sana za kufanya hii biashara.

2.Aje Dodoma afungue kiwanda kdg cha kusaga na kupaki unga wa mahindi,asee hapa pesa ataikimbia mahitaji ni makubwa sana,waliopo wanaofanya hii biashara hawakidhi mahitaji ya wateja kwamba mda mwingi unga haupo mitaani.location zipo za kutosha nawez kwemwelekeza bure kabisa.

3.Anunue tractor la kilimo alipeleke Manyara,hapa pesa ni nyingi sana na ya uhakika.location za kupeleka tractor kwa Manyara zipo nyingi sana na pesa zipo nyingi sana.
Nimeipenda sana hii idea
 
Msim ni mda gan mkuu? Miezi mingap toka upi adi up?
Mawazo mazuri sana ila yote yanahitaji uwepo wake..haswa no3 ila angeweza kukuza mtaji wake kidogo awe na kama 60m achukue trekta mpya kabisa na jembe lake aingie ata Turiani apo Moro uhakka wa kulaza atleast 18m kila msimu wa kulima
 
Ningekuwa mimi japo pia ni wazo ambalo ninalo siku nikikamata pesa kama hiyo.

Ningetafuta vijiji 4 ambavyo vipo mbali na mradi wa Rea

Ningefunga mitambo ya kuzalisha umeme wa upepo au maji ambayo inahamishika.

Ningeomba kibali cha kusambaza umeme kwenye vijiji hivyo.

Kila nyumba angalau kwa siku inipe 400 kwa siku yaani chini ya unit 1 kwa siku.

Nitafute nyumba 50 tu kila kijiji

Kila mwezi kila kijiji nitakua nikilaza 600,000/- hivyo kwa vijiji vinne = 2.4 m

Kwakua umeme ni wa upepo sina haja ya kufikilia mafuta au petrol.

Hiyo ni rafu tu.

Biashara zinazolipa ni zile vijijini mjini kumedoda.

Kama mjuavyo kwasasa kuna mdororo wa biashara hapa nchini haswa Dar kutokana na sababu mbalimbali. Kuna mdau anataka mawazo kuhusu mradi upi awekeze, waswahili husema penye wengi hakiharibiki kitu.

Biashara pendekezwa
1. Kununua na Kuuza Spare Parts za magari
2. Hardware ya vifaa vya ujenzi
3. Video & Photography/digital studio business
4. Workshop ya kushona na kuuza nguo kama suti (tailoring)

Mtaji: mpaka milioni 40 kutokana na biashara
Mahali: Dar

Mwekezaji:
Huyu anaishi Dar lakini ana majukumu ya kila siku ya muajiri yanamuweka bize hivyo hawezi kuendesha mradi muda na saa za kazi. Anapendelea kutafuta msimamizi au mshiriki/partner ambae anamuda ili kusimamia mradi/biashara kwa pamoja.

Ushauri unaohitajika:
Ushauri je ni biashara ipi itamfaa kati ya hizo au nyinginezo haswa ukizingatia hana muda na pia hajawahi fanya hizo biashara anatagemea usimamizi wa mtu au mshiriki kama akipatikana. Tafiti zinaonyesha usimamizi hafifu huchangia sana biashara kufa kutokana na hasara.

Wadau wenye biashara ambao hawazisimamii wao wenyewe mnaombwa kutoa uzoefu ili kupata mwazo chanya.
 
Ningekuwa mimi japo pia ni wazo ambalo ninalo siku nikikamata pesa kama hiyo.

Ningetafuta vijiji 4 ambavyo vipo mbali na mradi wa Rea

Ningefunga mitambo ya kuzalisha umeme wa upepo au maji ambayo inahamishika.

Ningeomba kibali cha kusambaza umeme kwenye vijiji hivyo.

Kila nyumba angalau kwa siku inipe 400 kwa siku yaani chini ya unit 1 kwa siku.

Nitafute nyumba 50 tu kila kijiji

Kila mwezi kila kijiji nitakua nikilaza 600,000/- hivyo kwa vijiji vinne = 2.4 m

Kwakua umeme ni wa upepo sina haja ya kufikilia mafuta au petrol.

Hiyo ni rafu tu.

Biashara zinazolipa ni zile vijijini mjini kumedoda.
Hii biashara ni nzuri kwenye makaratasi ila uhalisia haupo .
 
Kuanza biashara na kumuachia ngozi nyeusi ni sawa na kutupa hizo hela
 
Turiani msimu wa kilimo unaanzaga mwezi wa ngapi. Na ekari moja wanalima shiling ngap

Kwa Turiani kuanzia October watu wanaanza kulima mpaka mwezi March apo mwishoni ndo wanapumzika kulima na kwa sasa bei ya trekta kulimiwa kwa eka ni elf 40 kwa 45 kutegemea na hali ya shamba
 
Mtoa mada anaogopa kusema ni yeye ana hofu watu wasije mkaba maana ni hatari m40 sio mchezo kwa sisi makapuku,yaan nikiwa nayo hyo umasikini ndo bye bye,ukiwa huna hela unakuwa na idea nzuri za biashara ila ukishakuwa na hela idea zinapotea,ndomana nina utaratibu wa kuandika nilifikirialo ili nikija kupata mpunga iwe rahsi kutusua
 
Kwa Turiani kuanzia October watu wanaanza kulima mpaka mwezi March apo mwishoni ndo wanapumzika kulima na kwa sasa bei ya trekta kulimiwa kwa eka ni elf 40 kwa 45 kutegemea na hali ya shamba
Mashamba yapo ya kutosha bila shaka. Vipi uhitaji wa trekta kwa maeneo hayo? Wanayataka kweli au wengi wanayo wanamiliki?
 
Huyo mtu sio wa mchezo na hana shida ndogo ndogo sooo kwa mimi namshauri ili amantain status yake biashra alizotaka kwa upande wangu namshauri aingie kwenye "Vifaa va ujenzi,Hardware" Hatojutia...

HARDWARE KWA MWENYE MTAJI AINGIE,tamu sana.
Mkuu fafanua kidogo utamu wake?
 
Mashamba yapo ya kutosha bila shaka. Vipi uhitaji wa trekta kwa maeneo hayo? Wanayataka kweli au wengi wanayo wanamiliki?

Matrekta yapo mkuu ila bado hayatoshelezi mahitaji demand ni kubwa mno kipindi cha msimu ndio maana nasema mpaka msimu unaisha uhakika wa kulaza kati ya 18-22m kwa trekta mpya
 
Matrekta yapo mkuu ila bado hayatoshelezi mahitaji demand ni kubwa mno kipindi cha msimu ndio maana nasema mpaka msimu unaisha uhakika wa kulaza kati ya 18-22m kwa trekta mpya
Kwa siku trekta linalima heka ngapi?
 
Back
Top Bottom