Biashara ipi ya kuwekeza kipindi hiki kwa mtaji wa milioni 30 -50?

Duksi

Member
Mar 20, 2019
35
125
Kama mjuavyo kwasasa kuna mdororo wa biashara hapa nchini haswa Dar kutokana na sababu mbalimbali. Kuna mdau anataka mawazo kuhusu mradi upi awekeze, waswahili husema penye wengi hakiharibiki kitu.

Biashara pendekezwa
1. Kununua na Kuuza Spare Parts za magari
2. Hardware ya vifaa vya ujenzi
3. Video & Photography/digital studio business
4. Workshop ya kushona na kuuza nguo kama suti (tailoring)

Mtaji: mpaka milioni 40 kutokana na biashara
Mahali: Dar

Mwekezaji:
Huyu anaishi Dar lakini ana majukumu ya kila siku ya muajiri yanamuweka bize hivyo hawezi kuendesha mradi muda na saa za kazi. Anapendelea kutafuta msimamizi au mshiriki/partner ambae anamuda ili kusimamia mradi/biashara kwa pamoja.

Ushauri unaohitajika:
Ushauri je ni biashara ipi itamfaa kati ya hizo au nyinginezo haswa ukizingatia hana muda na pia hajawahi fanya hizo biashara anatagemea usimamizi wa mtu au mshiriki kama akipatikana. Tafiti zinaonyesha usimamizi hafifu huchangia sana biashara kufa kutokana na hasara.

Wadau wenye biashara ambao hawazisimamii wao wenyewe mnaombwa kutoa uzoefu ili kupata mwazo chanya.
 

mc gregor

JF-Expert Member
Mar 17, 2017
990
1,000
Aende china akafunge mzigo wa spare za pikipiki alete bongo atafte chimbo lake afungue gerage ndogo ya pikipiki awauzie kwa rejareja huku akitengeneza hizo pikipiki.

Kama vipi pia awe anasupply kwenye maduka madogomadogo kwa jumla io ni moja tu nimempa..kama yupo seriouss anicheki mm ndio niwe huyo mtu wa kusimamia miradi yake nina idea kama zote ila tu pesa sinaaa. Mi 40 tutarudisha chap tu aisee daaah
 

Duksi

Member
Mar 20, 2019
35
125
Aende china akafunge mzigo wa spare za pikipiki alete bongo atafte chimbo lake afungue gerage ndogo ya pikipiki awauzie kwa rejareja huku akitengeneza hizo pikipiki. Kama vipi pia awe anasupply kwenye maduka madogomadogo kwa jumla io ni moja tu nimempa..kama yupo seriouss anicheki mm ndio niwe huyo mtu wa kusimamia miradi yake nina idea kama zote ila tu pesa sinaaa. Mi 40 tutarudisha chap tu aisee daaah
Nashukuru mkuu kwa mawazo lakini kama nilivyoainisha tatizo lake kubwa ni muda wa kusimamia mtaji anao ila hana nafasi sidhani kama ataweza kwenda china mara kwa mara. Ntampa idea ya kukucheki, muyajenge.
 

mc gregor

JF-Expert Member
Mar 17, 2017
990
1,000
Nashukuru mkuu kwa mawazo lakini kama nilivyoainisha tatizo lake kubwa ni muda wa kusimamia mtaji anao ila hana nafasi sidhani kama ataweza kwenda china mara kwa mara. Ntampa idea ya kukucheki, muyajenge.
Boss mimi si nipo nakomaa na biashara yeye anatulia zake ofisini jioni anapitia mahesabu na kumpa feedback yeye ni bosi hapaswi kuteseka sana mm ndio nitafatilia kila kitu.

All in all kama hataki kabisa kuteseka na biashara na hatak mtu wa kuingia nae ubia wa kusimamia ila anataka biashara ikue na kupata faida basi ataangukia pua labda kama akanunue hisa uko au kucheza forex ndio anaweza ingiza pesa pasipo ufatiliaji
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
5,981
2,000
Kama ana access ya kupata 40millions kama capital ya biashara anashindwa nini kuachana na hiyo kumtumikia bwana akaingia mtaani akapambana kivyake?

Hapa ndipo naposhindwa kuwaelewa watu wanaosema wamesoma,imani yangu na uzoefu wangu kwa mtaji huo kwa mwezi anaweza kujitengenezea faida nzuri tu kama akitulia kwenye biashara.
 

EGF

Senior Member
Feb 12, 2017
122
500
Kwa ushauri wangu ningependekeza namba tatu kufungua studio ya kupiga picha na mambo yanayohusiana na hayo. Kwa Sasa biashara za mambo ya graphics designing, wedding photography, photoprinting ndo vinasoko Sana na biashara ya studio ya picha ni marachache Sana kula hasara ila changamoto ni gharama za vifaa watu wazoefu wapo hivyo napendekeza no. 3
 

Duksi

Member
Mar 20, 2019
35
125
Kama ana access ya kupata 40millions kama capital ya biashara anashindwa nini kuachana na hiyo kumtumikia bwana akaingia mtaani akapambana kivyake?

Hapa ndipo naposhindwa kuwaelewa watu wanaosema wamesoma,imani yangu na uzoefu wangu kwa mtaji huo kwa mwezi anaweza kujitengenezea faida nzuri tu kama akitulia kwenye biashara.
Kweli mkuu nadhani ndio ana malengo hayo...si unajua kuna msemo usiache kazi kama hujapata kazi...lengo ni ajenge biashara inayolipa zaidi labda aache kazi asimamie lakini hawezi acha tu maana hata huo mtaji anaupata huko nadhani
 

Duksi

Member
Mar 20, 2019
35
125
Kwa ushauri wangu ningependekeza namba tatu kufungua studio ya kupiga picha na mambo yanayohusiana na hayo. Kwa Sasa biashara za mambo ya graphics designing, wedding photography, photoprinting ndo vinasoko Sana na biashara ya studio ya picha ni marachache Sana kula hasara ila changamoto ni gharama za vifaa watu wazoefu wapo hivyo napendekeza no. 3
Hivi kamera zinabei sana ? Au ni zile mac computer? Shukrani kwa mchango
 

Perimeter

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
3,189
2,000
Huyo mtu sio wa mchezo na hana shida ndogo ndogo sooo kwa mimi namshauri ili amantain status yake biashra alizotaka kwa upande wangu namshauri aingie kwenye "Vifaa va ujenzi,Hardware" Hatojutia...

HARDWARE KWA MWENYE MTAJI AINGIE,tamu sana.
 

Mzaleee

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,022
2,000
Achukue baadhi ya hizi ....

1.Aje Dodoma afungue kiwanda cha kufyatua na kuuza tofali,hii biashara inalipa sana watu wanajenga balaa kwa Dodoma,hapa anaweza kuweka na ki min shop cha hard ware.location zipo nyingi sana za kufanya hii biashara.

2.Aje Dodoma afungue kiwanda kdg cha kusaga na kupaki unga wa mahindi,asee hapa pesa ataikimbia mahitaji ni makubwa sana,waliopo wanaofanya hii biashara hawakidhi mahitaji ya wateja kwamba mda mwingi unga haupo mitaani.location zipo za kutosha nawez kwemwelekeza bure kabisa.

3.Anunue tractor la kilimo alipeleke Manyara,hapa pesa ni nyingi sana na ya uhakika.location za kupeleka tractor kwa Manyara zipo nyingi sana na pesa zipo nyingi sana.
 
Top Bottom