Biashara inataka moyo sana

Biashara inataka moyo sana

Mimi ni graduate nilipata kazi nikafanya kwa muda wa miaka kama saba hivi kupata mtaji then nikaamua kuanzisha biashara,unajua biashara kuanzisha si kazi ukiwa na mtaji,kazi ngumu kwenye biashara ni kuifanya iendelee kuwepo.

Sasa wakati biashara inaanza mara nyingi inaanza vizuri but ukifika muda unakuta mambo hayaendi kabisa number ya wateja wako basic unakuta ghafla hawapo na hakuna wateja wapya wanaoingia dukani kwako aisee hii kitu usiombe unafanya kila kitu unachoweza kufanya kwa usahihi alafu matokeo hupati apa ndio nikajua kwa nini watu wanaenda kwa waganga.

Mashekhe au kwa wachungaji ili kuweza kupata msaada, kuna kipindi biashara inakua ngumu mpaka unaona bora urudi kwenye mshahara wa laki tano kwa mwezi big up sana kwa wafanya biashara walioweza kukuza mitaji hii kitu siyo rahisi mazee
Hapo inategemea na biashara yako na location uliyopo.
Mfano mie biashara yangu ya majeneza nimeweka office jirani na eneo la hospital halafu nna connection na madaktari na manesi wa hospitalini hapa ili wawe wananiunganishia wateja wapya kila siku na huwa wanahakikisha nauza kila siku maana kila anayeleta mteja ana percent yake
 
Nimeonja chungu na tamu ya biashara rangi zote nimeziona! Mpk nilipopigwa juju la maana tena na best nikapalalaiz upande mmoja docta ulienisaidia popote ulipo Mungu akubariki maana bila wewe kunisaidia na kupata matibabu sahihi ningekua kilema leo hii. Sikukoma nikaanza tena biashara safari hii nafanya tofauti ni kibabe tena nimepata connection ya chimbo la vifaa ni kuhesabu hela tu. Lakini Tanzania watu wake na biashara zake ni zaidi ya uyajuavyo.
 
Sasa wakati biashara inaanza mara nyingi inaanza vizuri but ukifika muda unakuta mambo hayaendi kabisa
Unatakiwa ufahamu hii kanuni : "Hakuna hela/fedha rahisi", ukilijua hili hutapata tabu hapa duniani!

Ili upate hela/fedha unahitaji kutoa sadaka.Hapa namaanisha sadaka ya muda, jitihada, nguvu, maarifa, jasho,damu, machozi, mtaji, akili, nidhamu, uthubutu, ujasiri n.k!

Hapa Watanzania wengi hatukuandaliwa katika misingi hiyo! Misingi ni ile nenda shule faulu halafu maisha mazuri! Halafu elimu yenyewe unakaririshwa!

No Easy Money: You never win playing by the rules (Dale Hunter)​

Hapo inategemea na biashara yako na location uliyopo.
Mfano mie biashara yangu ya majeneza nimeweka office jirani na eneo la hospital halafu nna connection na madaktari na manesi wa hospitalini hapa ili wawe wananiunganishia wateja wapya kila siku na huwa wanahakikisha nauza kila siku maana kila anayeleta mteja ana percent yake
Duuh hatari,yaani sisi tugome kula wewe uuze majeneza!
 
Hapo inategemea na biashara yako na location uliyopo.
Mfano mie biashara yangu ya majeneza nimeweka office jirani na eneo la hospital halafu nna connection na madaktari na manesi wa hospitalini hapa ili wawe wananiunganishia wateja wapya kila siku na huwa wanahakikisha nauza kila siku maana kila anayeleta mteja ana percent yake
Duh
 
Kwa huku biashara n uwendawazimu kwa sababu wateja wenyewe pesa za kulenga tungekua na uchumi wa Kati wa ukweli biashara zingenyooka.Ukopaji ungekoma(hii ndio inakimbiza uteja),uwezo wa kununua ungeimarika,ubora ungezingatiwa pamoja na wingi.
 
ghafla hawapo na hakuna wateja wapya wanaoingia dukani kwako aisee hii kitu usiombe unafanya kila kitu unachoweza kufanya kwa usahihi alafu matokeo hupati apa ndio nikajua kwa nini watu wanaenda kwa waganga.
Kama umekwenda shule epuka mno kuanzisha biashara ambazo hata ambao hawajaenda shule wanaweza kufanya, ni lazima utakwama tu.
Biashara kama Genge la vyakula na mbogamboga, Mangi shop, Bar, maduka ya ujenzi, Mama niwekee, - hizi biashara achana nazo kabisa kama umekwenda shule.
 
Usikatae ajira kwasababau una biashara,ndio maana unapopata kazi ni vizuri ukaoa ili mwenzako muweze kusaidiana kama utakuwa umeanzisha biashara,mfumo wa biashara unahusisha kupanda na kushuka,sasa kipindi unapokuwa imeshuka kama una ajira bado maisha yataendelea....
 
Tulia wewe ,hujui kitu
We unaona hizo biashara zimesimama unadhani hizo biashara ndio zinagenerate faida si ndio ?
Watu wanafanya mambo yao meusi pembeni hizo biashara ni changa la macho tu
Watu wanafanya utakatishaji pesa , ukwepaji kodi , Rushwa , kuuza bidhaa feki , kupunja na kufanya Magumashi kibao
Mfumo wa nchi hii ni wa ovyo mno
Hairuhusu private sector na ujasiriamali kuthrive ,kama unaona hizi ni stories anzisha biashara halafu ulete mrejesho hapa
naweza amini biashara ngumu sana aisee.

mtu kkoo ana frem yenye mtaji 5mil,kodi kwa mwezi 500k,bado umeme,malipo ya msimamizi,nauli nk,ukikaa ukafikiria unaona kabisa kuna kitu hakiki wazi😃😃😃
 
Mimi ni graduate nilipata kazi nikafanya kwa muda wa miaka kama saba hivi kupata mtaji then nikaamua kuanzisha biashara,unajua biashara kuanzisha si kazi ukiwa na mtaji,kazi ngumu kwenye biashara ni kuifanya iendelee kuwepo.

Sasa wakati biashara inaanza mara nyingi inaanza vizuri but ukifika muda unakuta mambo hayaendi kabisa number ya wateja wako basic unakuta ghafla hawapo na hakuna wateja wapya wanaoingia dukani kwako aisee hii kitu usiombe unafanya kila kitu unachoweza kufanya kwa usahihi alafu matokeo hupati apa ndio nikajua kwa nini watu wanaenda kwa waganga.

Mashekhe au kwa wachungaji ili kuweza kupata msaada, kuna kipindi biashara inakua ngumu mpaka unaona bora urudi kwenye mshahara wa laki tano kwa mwezi big up sana kwa wafanya biashara walioweza kukuza mitaji hii kitu siyo rahisi mazee
Kazi zoto ni nyepesi kazi ngumu ni kuanzisha biashara ikakua huku watoto wakienda shule na baadhi ya maendeleo unayafanya huku mtaji ukiongezeka,ndio maana matajiri wanaitwa wachawi
 
Back
Top Bottom