Nicholas
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 25,260
- 7,195
Comrede Nico!
Nilichogundua siku nyingi ni kuwa unaweza kumpa mtu majibu mafupi yaliyonyooka akashindwa kukuelewa; na hata ukimpa marefu ya kueleweka ataona uvivu kusoma na ataendelea kubaki kuwa asiyejua 'Mjinga'..
Huyu jamaa ana tatizo la kawaida sana ambalo watawala wengi kama Wasirra na Lukuvi wanalo; hudhani kuwa wao ndio wanaojua kila kitu na hakuna anayeweza kuelewa na kufanya vitu vya msingi kuliko wao. Najaribu kumjibu kwa ufupi sana kwa sababu najua hata nikimjibu marefu hatakubali ukweli wala kuelewa.
Well said..... hilo tatizo limepata mbolea katika utawala wa CCM.Ndio maana ni salama sana kutumia media km JF.kwani ungeongea nao directly,akiwa na kundi la watu wenye fikra kama zake, wangekushambulia kwa makelele, na fujo nyingi na kupoteza muda mrefu kuulizia vyeti, historia na ujinga mwingine mwingi tuu kwa vitu vya kumaliza katika fikra tuu.
Kinachoumiza ni kwamba kwa jinsi walivyo kifikra na mamlaka waliyopewa ni hatari sana kwa uhai wa taifa na watu wake.Ni kama raia makini anavyoona hatari "kiziwi aliyepofuka aliyeomba na kupewa kazi ya ulinzi katika fuel station.Halafu akaenda mbali zaidi kutaka apewe jiko la mchina la kupikia kwa kisingizio kuwa ataweka number ya fire brigade ili awapigie hatari ikitokea,bila kujua hatoweza pata taarifa katika simu siku wengine wanaona hiyo hatari"