Waziri wa Mambo ya Ndani: Tanzania kuna upunguzu wa Vituo vya Polisi 470

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Taarifa ya upungufu wa vituo vya polisi Nchini Tanzania imewaibua wadau wa haki za binadamu, wakidai kuwa chanzo ni kukosekana kwa haki.

Jana Aprili 5, 2022, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni aliwasilisha bungeni taarifa ya upungufu wa vituo vya Polisi vya daraja B vinavyohitajika nchini kwa ajili ya shughuli za kiulinzi.

Alisema Tanzania inahitaji kuwa na vituo vya daraja B 563, lakini vilivyopo ni 93 kwa nchi nzima, hivyo kuwa na upungufu wa vituo 470, kiwango ambacho ni kikubwa kutokana na uhitaji kwa shughuli za kiulinzi.

Waziri alitoa hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Mchinga, mama Salma Kikwete aliyehoji lini Serikali itajenga vituo vya polisi katika tarafa mbili za jimbo lake.

"Katika shughuli za ulinzi na usalama wa nchi yetu na nchi nyingine yoyote, polisi ni kitu muhimu sana kwenye kazi hiyo taarifa, katika Jimbo la Mchinga lenye kata zaidi ya 12 lina tarafa nne na kati ya hizo tarafa mbili hazina kabisa vituo vya polisi," alihoji Mama Salma.

Waziri alisema mahitaji ni makubwa, hivyo Serikali itaendelea kujenga vituo vya Polisi kadri ya upatikanaji wa fedha, huku akiwaomba wabunge kushiriki katika ujenzi wa vituo kwa ushirikiano na wananchi.

Tuna upungufu mkubwa wa vituo vya polisi, kwa mfano vituo vya polisi daraja B tunavyo 93, lakini mahitaji ni kuwa na vituo 563, niwaombe wabunge kuiga mfanoo wa wabunge wengine, akiwemo Angelina Mabula ambaye amewashirikisha wananchi kujenga," alisema Masauni.

Mkurugenzi wa zamani wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk Hellen Kijo Bisimba akizungumza na Mwananchi, alisema takwimu hizo zinatia shaka na kuonyesha kuwa, Taifa halina vipaumbele vyake kwenye mambo ya msingi.

Dk Kijo Bisimba alisema kwa zaidi ya miaka 60 Taifa kuwa na vituo vya polisi ambavyo havifiki hata nusu wakati inajulikana kuwa idadi ya watu inakua, ni jambo la aibu ambalo mwisho wake si mwema.

Mchambuzi wa mambo ya siasa, Edwin Soko alisema: “Kama watu badala ya kutembea dakika saba kufika kituo cha Polisi, wanatumia dakika 45 ni madhila gani yanayomkuta njiani, baadhi ya watu wanaweza kumpiga kabla ya kufika katika mfumo wa haki jinai.”

Chanzo: Mwananchi
 
Makubwa kwani uhalifu umeongezeka? Hadi vitu vya polisi viongezeke? Au vinaongezeka tu kutegemea population inavyoongezeka?
 
Back
Top Bottom