Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amekutana na Waandishi wa habari kuelezea mwenendo wa kampeni. Asema Jaribio la kuvuruga Uchaguzi litasababisha watu wapelekwe 'The Hague'

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326

Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekutana na Waandishi wa habari kuzungumzia hali ya ya kampeni zake ilivyo mpaka sasa na kile kinachoendelea kuelekea Uchaguzi Mkuu mnamo tarehe 28/10/ 2020. katika Mkutano huo ambao waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walihudhuria, Tundu Lissu ametolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali.

Aidha, akianza kutoa tathmni ya kile kinachoendelea katika kampeni zao Tundu Lissu alisema "Kwa ujumla tumefanya kazi kubwa sana na nyie ambao mpo kwenye msafara huu mmeona na Watanzania wameona. Tumefanya mikutano mingi kuliko mikutano yote aliyofanya mpinzani wetu Mkuu Rais Magufuli pamoja, Makamu wake pamoja na Waziri Mkuu kwa combined. Yaani mikutano ambayo tumeifanya sisi ni mingi kuliko ambayo wameifanya wao kwa ujumla wao.

Mikutano yetu imekuwa na mafanikio makubwa sana kuliko ambavyo sisi wenyewe tulitegemea mwanzoni, hakuna mkutano ambao imebidi tusafirishe mtu yeyote. Mikutano yetu imehudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya Watanzania ambao wametembea wao kwa miguu yao, wamekuja kwa vyombo vyao wamekuja kwa namna mbalimbali za usafiri kwa kujitegemea. Mikutano yote ya Chama cha Mapinduzi watu wanakwenda kwa kulazimishwa, wanapeleka watoto wa shule baada ya kuwalazimisha kwa kufunga shule, kutisha waalimu, wanafunga Maofisi ya serikali na kulazimisha wafanyakazi kwenda kumsikiliza Magufuli.

Wataalamu wetu wa mahesabu na watu ambao wanafuatilia wanafanya survey za muelekeo wa Upigaji kura wanatuambia kwamba kwa jinsi ambavyo mikutano yetu imekwenda ya kampeni, kwa jinsi ambavyo tumefanya mikutano yaetu tunashinda uchaguzi huu kwa asilimika kati ya 65 hadi 75 huo ni mtazamo wa watua ambao tumewaopa kazi wa kufanya survey ya Wapiga kura nchi nzima.

Hali yetu ni nzuri sana. Kwahiyo, Magufuli nje ya Tume ya Uchaguzi, nje ya wasimamizi wa Uchaguzi aliowateua. Makada wa CCM ndio Wakurugenzi na Wasimamizi wa Uchaguzi, nje ya kufanya vurugu, nje ya kuiba kura hawezi akashinda uchaguzi huu kwa sababu hana kibali cha Watanzania tena. Kwahiyo kwa sababu hana kibali cha Watanzania na kampeni yake inadoda kila mahali tunaona sasa vitendo ambavyo tulivitabiri mwanzoni. Tulisema kwamba hawa watu hawawezi wakashinda Uchaguzi ulio huru na haki na tayari tunaanza kuona dalili hizi aidha kuharibu uchaguzi, au kufanya wizi mkubwa wakitumaini kwamba labda pengine atabaki madarakani.

Daftari la Wapiga kura limetolewa siku chache zilizopita kwa kuangalia haraka haraka wachunguzi wetu wanalifanyia uchunguzi wa kina nataarifa zitatoka kabla ya jumatatu hopefully. Lakini kwa kuangalia tu maeneo machache inaelekea kuna mamilioni ya Wapiga kura hewa ambao wameingizwa katika daftari la kudumu la Wapiga Kura, inaelekea kuna vitu hewa vya kupigia na kuhesabia kura kwa maelfu, wataalamu wetu wanalifanyia kazi na wanaendelea kulifanyia kazi tangu lilipotoka, taarifa ya kina itatolewa si muda mrefu lakini ushahidi wa mwanzo unaonesha kwamba wameandika majina ya watu wasiokuwepo, wameandika majina ya watoto wadogo wa shule na tumeona baadhi yao wakifundishwa namna ya kupiga kura na Hazani Zungu. Kwahiyo, wameandikisha wapiga kura wasioukuwa na sifa na wapiga kura wasiokuwepo kwa mamilioni na vituo hewa.

Sasa hii ni wazi kuwa wanafikiria wanaweza kuuiba uchaguzi ambao hawana uwezo tena wa kuushinda wanataka kufanya hivyo. La pili, ni kutumia vitendo vya kihalifu kama kubadilisha matokeo mahali ambapo wameshindwa, kutangaza wagombea wao kwa nguvu watu wetu wametuambia kuwa wanachoweza kufanya kingine ni hicho.

Vitendo vya tatu ambavyo tumeona vimekuwa vikiongezeka sana ni matumizi ya vyombo vya dola, taasisi za kiserikali kw waziwazi ambao wamekuwa na nia ya kuipitisha CCM au kuhakikisha uwezo wetu wa kufanya kampeni unapunguzwa au tunazuiliwa kabisa kufanya kampeni. Vitendo vilivyotokea jana ni mfano halisi wa vitendo hivyo. Jana ilikuwa tufanye mikutano kumi na kila mahali katika sehemu hizo kumi maelfu kwa maelefu wamekusanywa. Lakini asubuhi wakati tunaondoka uwanja wa ndege kuanza safari yetu pilot wa ndege yetu akaambiwa hawezi akatua Nachingwea, hawezi akatua Nanyumbu akaambiwa kuna kimbunga huko hali ya hewa sio nzuri. Kwahiyo, ili kumwepusha Mgombea Urais na madhara yanayoweza kuhatarisha usalama wake ni marufuku kutua Nachingwea na Nanyumbu baadae wakaongeza vituo vingine ambavyo hatuwezi kutua.

Tulipoanza safari kuelekea Mikutanoni baadae tukaambiwa Polisi wamepiga mabomu Kibiti na Rufiji ikiwa ni pamoja na kuwatawanya watu ikiwa pamoja na kuwanyang'anya vyombo vya matangazo. Kwahiyo, watu ambao tulikuwa tukazungumze nao wamepigwa na Mapolisi na Wanajeshi kwa namna ambayo clearly walikuwa hawataki tukazungumze na watu wa maeneo hayo. Kwa sababu tulipata habari kuwa mikutano imevunjwa kwa namna hiyo tukasema twende ambako mikutano haijavunjwa.

Hivyo, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'

Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"

Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo.
 
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'

Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"

Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo
Naked truth
 
Ha ha ha , yeye pia likitokea la kutokea anaweza kupelekwa depending na uhuska wake katika Jambo Hilo. Asijidanganye kuwa anaweza akahamasisha vurugu watu wakadhurika halafu yeye akabaki salama.

By the way naona anajiamini sana labda kwakuwa wenye Mahakama hiyo ndio wamempa Assignment. Lakini pia akumbuke hiyo Mahakama ni kama imeshajifia tu, kila kukicha uhalali wake unakuwa Questionable.
So aache kuwatisha watu.
 
TENDENI HAKI HILOO TUU.
 
Usione baada ya mauaji Magufuli anamtupia mpira afande Siro ,bashiru polepole na kumtaka wawajibike na wakamatwe wapelekwe huko wakajibu kesi,na kule Unguja anamtosa Sheni na makamo wake wote wakamatwe na katibu wao.

Magu atadai aliwaagiza wafanye uchaguzi wa haki na anaeshinda apewe ushindi wake hawakumsikiliza ,mbinu za mauaji walizopanga hazijui wala hakujulishwa.
 
Naona Prosecutor Bensouda ICC, amevalia njuga hawa viongozi wanaoleta machafuko, Juzi hapa alikuwa ana deal na Al bashir.

Kuna watu wa nyumbani hapa you're next to appear before ICC.

Mark my words!
Mbona juzi kati hapa kapigwa pini na USA na amenywea. Boya Kama Boya Wengine. Ukiona Mtu yeyote kutoka Nchi Maskini Kama Afrika anapewa Position kubwa Kama hiyo, basi ujue, lengo ni atumike dhidi ya Waafrika wenzake. Huyu Bibi na the late Kofi Anan ni mifano hai!
 
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'

Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"

Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo
Hata EL alituaminisha hivi hivi
 
Mkuu Dada yangu mrembo beth , Uchaguzi unaendeshwa na Tume yetu huru ya Uchaguzi, NEC, Rais wa JMT ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, ametoa hakikisho la uchaguzi utakuwa huru na wa haki, haya mambo ya kutishiana 'The Hague' ya nini?, haya sio mambo!.

Kwa vile sio wote wanajua sheria, hivyo mtu mmoja kujua sheria, asitake kuwatisha watu wengine wote na 'The Hague', kuna mambo ya 'The Hague' na mambo ambayo sio ya 'The Hague', uchaguzi ni mambo yetu ya ndani, sio mambo ya 'The Hague', tusitishiane na 'The Hague'.
P
 
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'

Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"

Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo.
yeye ndiyo atakwenda the hegue maana anahamasisha maandamano yatakayo letamaafa
 
Usione baada ya mauaji Magufuli anamtupia mpira afande Siro ,bashiru polepole na kumtaka wawajibike na wakamatwe wapelekwe huko wakajibu kesi,na kule Unguja anamtosa Sheni na makamo wake wote wakamatwe na katibu wao.

Magu atadai aliwaagiza wafanye uchaguzi wa haki na anaeshinda apewe ushindi wake hawakumsikiliza ,mbinu za mauaji walizopanga hazijui wala hakujulishwa.
Hana njia ya kukiepuka hicho kikombe.

Huko mbele ya safari sio wajinga kama tunavyotakiwa au tunavyolazimishwa tuonekane kuwa wajinga hapa nyumbani.
 
Uchaguzi unaendeshwa na Tume yetu huru ya Uchaguzi, NEC, Rais wa JMT ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, ametoa hakikisho la uchaguzi utakuwa huru na wa haki, haya mambo ya kutishiana 'The Hague' sio mambo!.
Kwa vile sio wote wanajua sheria, hivyo mtu mmoja kujua sheria, asitake kuwatisha watu wengine wote na 'The Hague', kuna mambo ya 'The Hague' na mambo ambayo sio ya 'The Hague', uchaguzi ni mambo yetu ya ndani, sio mambo ya 'The Hague', tusitishiane na 'The Hague'.
P
Wewe kwa akili yako, Magufuli anaweza kusimama The Hague akajitetea kama akitakiwa hivyo mana kuongea point tu kwa kiswahili hawezi sembuse kule.

Kinuke tu!
 
Aache ujinga kila saa wazungu wazungu yaani domoni mwake kumejaa wazungu tu ohhh madini tutayaweka rehani kwa wazungu ohhh Amsterdam ohhh the Hague ohhh Mimi najua kingereza

Lisu lazima tumupnyesha kuwa Tanzania ni ya waswahili sio wazungu tarehe 28 October hatumpi kura
 
Back
Top Bottom