Historia Na Shujaa: Dkt. Hellen Kijo Bisimba, Afrika Na Uafrika Vol 1

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
mashujaa east africa16.jpg


Dk Kijo-Bisimba amekuwa Kinara wa harakati za haki za binadamu nchini Tanzania , akiwa kama mlinzi wa haki za binadamu kwa muda mrefu amekua mwenye ushawishi mkubwa na kuwa chachu ya vijana wengi wachanga kuingia katika uwanja wa sheria kwasababu yake.

Alizaliwa mnamo mwaka 1954 katika mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania. Morali ya kuwa mwanaharakati aliipata miaka ya 1970 akiwa mwanafunzi katika shule ya Korogwe huko Tanga. Baada ya walimu kumtuhumu kuwa alimwandikia barua ya kumchafua mkuu wa shule hiyo. Mama Bi Simba, alijiudhulu nafasi yake ya dada mkuu msaidizi na kupewa adhabu ya kukaa nyumbani kwa muda. Baba mzazi wa Bi SIMBA alimwombea msamaha lakini walimu hawakukubali mpaka pale alipoomba mwenyewe msamaha kwa kukiri kosa ambalo hakulitenda.

“Niliadhibiwa kosa kubwa ambalo sikulitenda ningali dada mkuu msaidizi, kwanini hawakuniamini kuwa sikufanya kosa hilo licha ya wao kuniamini mimi kuongoza kama dada mkuu msaidizi”?

Mwaka 1996
, Bibi Hellen alikua ni moja ya viongozi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na akiwa kama mmoja wa waanzilishi. Alitakiwa kuchukua nafasi ya ukurugenzi na kuwa na jukumu la kutetea masuala ya jinsia, rangi na dini, Anasema kwake ilikua ni kazi ambayo aliipenda kwa moyo wake wote. “Niliipokea nafasi ile ii niwatumikie watanzania”. Anasema hata watoto wake wanne huishi na kujiamini kwa kumtazama mama yao akiwa kama mama mchapakazi. “Nimekuwa mjane toka mwaka 1994 lakini watoto wangu ni imara na wanafanya kazi zao kama ninavyowajibika mama yao.

Kabla hajajiunga na LHRC , Dr Hellen alikua mwalimu wa kingereza na kiswahili katika taasisi ya elimu ya watu wazima. Ambapo alifanya kazi kwa miaka 10. Alihamasika kusoma sheria kutoka kwa marehem mumewake na wakati alipoanza kufanya kazi LHRC alikua bado anajitolea katika shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani afrika WILDAF. Ni shirika ambalo aliliwakilisha katika mkutano wa kimataifa wa Beijing katika maendeleo ya wanawake mwaka 1995.

Mwaka 2001, Dr Kijo Bisimba alisimama kama mwanamke wa kwanza kutoa tamko la kuipinga serikali baada ya wananchi kuuawa huko Zanzibar kwasababu ya mgogoro wa kisiasa. Ujasiri huo ulimpelekea kupata tuzo akiwa kama mwanamke wa kwanza kutoka nchini Tanzania , kupata tuzo ya Woman of Courage ambayo ilitolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 2008. Bibi Hellen anasema, “kila mtu ana haki ya kuishi hata kama akiwa ni mkosaji”

Mwaka 2008-2011 alichukua mapumziko kwaajili ya kusoma PHD nchini uingereza na kumfanya kuwa mmoja kati ya wanawake wa chache nchini Tanzania kuwa na PHD haswa kwenye suala la haki za binadamu pamoja na sheria. Research yake ilijikita kwenye masuala ya haki za watoto. KWANINI HAKI ZA WATOTO? “Nimetaka kuwapatia watoto wa kiafrika sauti na kuona ni namna gani wanautazama mfumo wa serikali katika nchi, na ninadhani kuelewa na kuwatambua watoto ni msingi mzuri wa baadae kwa serikali” anaongeza kwa kusema “ watoto wa leo ndio viongozi wa baadae” Dr Hellen.

"Ni mama mzuri ambaye anafanya lile analolihubiri na hakuna kinachoweza kumstopisha pale anapohitaji kufanikisha jambo" Alisema Mwalongo ambaye alifurahishwa na upendo wa Dr Hellen kwa watoto ambapo licha ya kuwa mjane, bado anatunza watoto wasio na wazazi (yatima) nyumbani kwake na pia ni memba wa umoja wa wasio na wazazi katika kanisa lake.

26 June 2012 Mida ya usiku aliwahi kupigiwa simu na madaktari ambao walikua kwenye mgomo na kumpa taarifa ya kupotea kwa mwenzao Dr Stephen Ulimboka, alishangazwa na kushtuka kwakua hakutambua kosa lake zaidi ya kupambana kwa maslahi yao wao kama madaktari

Kigo-strike-2012-300x200.jpg


Alikaa na madaktari na kuitaka serikali kufanya uchunguzi na kumjua ni nani alikua nyuma ya tukio hili la kinyama na kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake. Hili sio tukio pekee lililowahi kumkuta mama huyu kwaajili ya kupambania haki.

Mwaka 2018, Dr Hellen, alikemea vikali kama mzazi tulio la mwanafunzi wa chuo kikuu cha usafirishaji Dar es Salaam (NIT) ambaye alifariki baada ya kupigwa risasi ya kichwa kimakosa na afisa wa polisi aliyekuwa anajaribu kutuliza ghasia za waandamanaji wa kisiasa wa CHADEMA mnamo tarehe 16 Februari siku ya Ijumaa, 2018 huko Kinondoni.

Mnamo mwaka wa 2019 Waziri wa Mambo ya Ndani wa muda huo nchini Tanzania Kangi Lugola alisema kuwa anashindwa kuelewa ni kwanini Kijo-Bisimba hajatunzwa na nchi yake.

Lugola Aliyasema hayo alipofungua ofisi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu siku ya alhamisi ya tarehe 26 Septemba 2019.

Ni mfano wa kuigwa pale linapokuja suala la kutetea haki za binadamu kwenye nchi yake. Alikua anaamini na nadhani mpaka sasa anaamini katika usawa wa haki za binadamu. Kusema ukweli sijui ni kwanini hajapewa tuzo kwenye nchi yake. Alisema Kangi Lugola.

ESpbDvwXsAAuUfB.jpg


Dr Hellen Kijo Bisimba ametumikia kituo cha sheria na haki za binadamu toka mwaka 1995 mpaka alipostaafu mwaka 2018.

Dr Hellen anaamini ya kuwa, Tanzania ni nchi nzuri na ya amani, ila kuna baadhi ya mambo yanajitokeza sasa yanaweza kuleta matatizo makubwa hapo baadae. Anasema suala la ukabila na udini ni mambo yanayojitokeza kwa kasi sasa wakati zamani hayakuwapo. "Ninaamini hii ni changamoto ambayo serikali inapaswa kuifanyia kazi, ili ncho yetu iendelee kujivunia amani na umoja ambao tunao" Dr Hellen
 
Back
Top Bottom