Betting addiction inanipotezea utulivu kabisa

Betting addiction inanipotezea utulivu kabisa

Na mjibia ni doctor na ana mchango mkubwa Sanaa humu jukwaani.

NB. Kipindi Fulani tabata nikiwa mwanachuo Kuna brother mmoja doctor muhimbili alikua mlevi na mnywa pombe kupitiliza akafariki kwa ugonjwa wa Figo akiwa kwenye prime age iliniumaga Sanaa YULE BROTHER ALIKUAGA ANATETEMEKA ASUBUH MPAKA ANYWE POMBE NDIO HALI INATULIA. Inashangaza msomi wa afya kuwa addicted na ulevi wa mapombe kupitiliza

SO ADDICTION NI ADDICTION IWE MPIRA, BETTING,NGONO,POMBE E.t.c
So haijalishi hata uwe Raisi wa nchi ama ASKOFU ama doctor.
Isaya 40 : 1 Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu.

2 Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
 
Simu imetupa uraibu sana wengi wetu na hatujui. Binafsi ndicho kitu pekee kwa sasa naona kinanisumbua, japo sijafikia stage mbaya ila simu imeniharibu.
Simu ni lazima utumie simu ni lazima ziite
 
Kukabiliana na urahibu wa kubet (kamari) ni jambo linalohitaji nguvu ya kisaikolojia, msaada wa kijamii, na wakati mwingine msaada wa kitaalamu. Hapa chini kuna hatua muhimu zinazoweza kusaidia:

1. Kukubali kuwa una tatizo​

Hii ni hatua ya kwanza muhimu zaidi. Usijilaumu, lakini kubali hali halisi kuwa kubet kunakuletea matatizo ya kifedha, kijamii, au kisaikolojia.

2. Tambua vichochezi vya kubet​

Fahamu ni nini kinakufanya ubet mara kwa mara:
  • Msongo wa mawazo
  • Upweke
  • Marafiki wanaobet
  • Kutafuta pesa kwa haraka
  • Uvivu wa kufanya kazi nyingine
Ukishajua sababu, unaweza kuanza kutafuta njia mbadala za kukabiliana nazo.

3. Epuka mazingira yanayokuchochea kubet​

  • Futa apps za kubet na block tovuti zao.
  • Epuka marafiki wa kubet, hata kama ni wa karibu.
  • Jiepushe na matangazo ya kubet, ikibidi tumia apps za kusaidia ku-block matangazo hayo.

4. Weka ratiba na shughuli mbadala​

  • Fanya mazoezi, soma vitabu, jifunze ujuzi mpya.
  • Jiunge na vikundi vya kijamii au vya kidini.
  • Tafuta shughuli zinazokupa msisimko au furaha isiyo ya fedha.

5. Weka mipaka ya kifedha​

  • Weka akaunti yako ya benki kwenye udhibiti wa mtu unayeamini (kama mzazi, mwenzi, au rafiki).
  • Jifunze kuweka bajeti na kufuatilia matumizi.
  • Epuka kuwa na fedha taslimu nyingi mkononi.

6. Tafuta msaada wa kitaalamu​

  • Tafuta mshauri wa afya ya akili au mtaalamu wa uraibu.
  • Kuna mashirika yanayosaidia waliopata uraibu wa kubet, mfano:
    • Gamblers Anonymous
    • Hope Rehab Centres
    • Makanisa/madhehebu mengi pia hutoa msaada wa kiroho na ushauri.

7. Jiunge na vikundi vya msaada (Support Groups)​

Kuwa sehemu ya kikundi cha watu waliopitia au wanaopitia changamoto kama zako hukupa motisha, msaada na kuelewa kuwa hauko peke yako.

8. Weka malengo na zawadi za binafsi​

Weka malengo madogo kama:
  • "Sitabashiri kwa wiki moja"
  • "Nitahifadhi 5,000 kila wiki badala ya kubet"

Kisha jizawadie kwa mafanikio yako (mfano: kwenda matembezini, kununua kitu unachopenda).

9. Omba msaada wa kiroho (kwa waumini)​

Kama wewe ni mtu wa imani, sala, maombi, na ushauri wa kiroho vinaweza kuwa msaada mkubwa katika kudhibiti tamaa ya kubet.

10. Usikate tamaa​

Urahibu huweza kurudi, lakini usijione mnyonge ukiteleza. Jifunze kutokana na makosa na endelea kupambana.
 
Ahsante sana mkuu
 
Nilianza na kuacha madeni haya yasiyoeleweka wala kuomba pesa kwa ndugu jamaa kwa kuwa na mpango mkakati wa akiba isiyoguswa nina miaka miwili pasipo kuwa na madeni madogo madogo

Nilikuwa Addicted na p*no na kujichukulia sheria mkononi nimeweza kuacha ni mwaka mmoja na miezi miwili sasa hata picha ya mtu aliyenusu uchi naipita kama sijaiona niko na amani ya nafsi kubwa na kujiamini kwa hali ya juu

Na Sasa nipo kwenye programu ya kuachana na mikeka unaweza kujiunga nami ukaachana na uraibu wowote na ukawa mtu huru uraibu unatufanya tuishi kwenye mawazo badala ya kuishi uhalisia
 
Hapa nimepiga hesabu kupitia diary yangu kwanzia mwezi wa nne mpaka leo nimeliwa milioni mbili laki moja na 89
2,189,000/= ambayo ni wastani wa laki saba kila mwezi hapo sijapigia hesabu toka mwaka umeanza hadi ka suzuki kangu nimeuza
napenda sana cassino hasa spin and win huwa nikiliwa nasema sichezi tena ila nikipata hela tu nakua kama na maruhani yaani lazima nibet tu.

Inanicost mno sometimes mtu unashindwa nunua hata nguo upendeze pesa unalisha wahindi

Sijui nachomokaje kwenye huu uraibu ila kwa kifupi hali ni mbaya
Betting tulifaidi miaka ya 2015 kurudi nyuma tukajenga na kununua bodaboda .

Sasa hivi hakuna mbabe ambaye anakupa tumaini .

Enzi za Manchester united na Chelsea hawa ndo walitupa pesa
 
Nimechoka ngoja niweke mikakati ya kuacha
Kaza Buti mkuu. Mie nilipitia hiyo Hali Tena afadhali wewe hujaathirika kivile. Mie nilliokolewa na familia Hasa mke na mtoto wangu. Kifupi nilitengwa na kuonekana SI baba Bora Wala mume Bora. Nilikonda Kwa madeni ofisini nilidharaulika kiafya nikaathirika . Heshimu uamuzi wako,punguza marafiki wenye huo uraibu, FUTA Kila kitu kinachohusu kubeti. Panga kurudisha ulichopoteza kwenye kubeti Kwa kutumia njia nyingine.kumbuka kubeti hakujawahi kuwa source of income.
 
Back
Top Bottom