Betting addiction inanipotezea utulivu kabisa

Betting addiction inanipotezea utulivu kabisa

DR SANTOS

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
14,248
Reaction score
32,098
Hapa nimepiga hesabu kupitia diary yangu kwanzia mwezi wa nne mpaka leo nimeliwa milioni mbili laki moja na 89
2,189,000/= ambayo ni wastani wa laki saba kila mwezi hapo sijapigia hesabu toka mwaka umeanza hadi ka suzuki kangu nimeuza
napenda sana cassino hasa spin and win huwa nikiliwa nasema sichezi tena ila nikipata hela tu nakua kama na maruhani yaani lazima nibet tu.

Inanicost mno sometimes mtu unashindwa nunua hata nguo upendeze pesa unalisha wahindi

Sijui nachomokaje kwenye huu uraibu ila kwa kifupi hali ni mbaya
 
Pole ndugu usiwaze ulichopoteza kuwa njia pekee ya kurudisha ni kubet badilisha mwelekeo maana wahenga wanasema hasira hasara kadri unavyotamani kurudisha ndio unapoteza
Nikajua nikiblock betpawa na sportybet nitakua nimepumua lakini wapi sahizi nacheza had ofisi za premierbet naliwa huku nimesimama
 
Hapa nimepiga hesabu kupitia diary yangu kwanzia mwezi wa nne mpaka leo nimeliwa milioni mbili laki moja na 89
2,189,000/= ambayo ni wastani wa laki saba kila mwezi napenda sana cassino hasa spin and win huwa nikiliwa nasema sichezi tena ila nikipata hela tu nakua kama na maruhani yaani lazima nibet tu

Sijui nachomokaje kwenye huu uraibu ila kwa kifupi hali ni mbaya
Kubeti ni kujitia kiberiti
 
Hii inshu nilishaipitia ila mdogo mdogo naelekea kupona ,ila majuz tena nimejikuta nimerudia ujinga nikapigwa 30,000 chapu

Ilifikia mpaka nikawa nabetia pesa za watu,nimelipa mdogo mdogo sahv nimebakiza kama laki 1.5 nililiwa kama laki 5 ya watu,

Betting ya sasa ukitaka ufe beti high stake,tunakuzika mapema tu
 
Back
Top Bottom