Enzi hizo bana PROFESSOR J ft LADY JAYDEE anaichambua Bongo ya enzi za mzee ruksa
Niliupenda sana huu wimbo
BONGO DAR ES SALAAM
Ndani ya bongo mambo super hapana uongo, ingawa some times bongo chungu kama sifongo
Nafanya makaratee kama machinga mtaa wa kongo, na kimtindo mtindo nakata ngebe MC manyongo
Kamata matata kitu roho inapenda utapata, Bongo Dar es salama ni mpeto wa kutakata
Nenda viwanja vikali vya Bongo ustaajabu,na pita slip way blueparm ama mambo club
Kama hujazowea naweza ukavunja shingo, mambo ya isidingo watu mkononi nokia ringo
Huwezi jua yupi mototo wa geti yupi changu, wote wanameremeta kama mamtoni mwanangu
Deal zinapo yeyuka wabongo tunalia ukata, subiri kichapo chake pale mbongo anapozipata
Mwendo ni kiti kirefu jirani na nyama choma , na toto mbili tatu za geti ama au zakona
Hii watu wabongo tunasema napoteza mawazo, lakini matajiri hutokea wakati unazo
Wakati wa jua kali saa moja shuka utosini, unapojifanya nawaza mambo mengi ya ofisini
Pitia pitia night kali mitaa ya kinondoni, kina dada powa nusu uchi fegi mdomoni
Nakama unagari watajazana madirishani weee, hadi ukose hewa wote wanataka hisani
Kwenye madala dala kuibiwa ni kawaida, vaa cheni shingoni saa mkononi utoe faida
Wacha dirisha wazi kisha ukatize manzese,ili uwape mateja mtaji waende chimbo wakatese
Rudi mwananyamala ooh mateja kibao, katiza saa moja moja uone roba za mbao
Utaona kama mtoa roho yupo karibu yako, ni heri utoe chochote ili uokoe nafsi yako
Bongo eeeh Bongo Dar es salaam utalia lia liaaa Bongo Dar es salaam
Kaachonjo eeh ndani ya Dar es salam, utalia lia liaa ndani ya Dar es salaam
Bongo ya sasa si ya mwaka 47, mpaka bibi vizee sasa wanafanya ukahaba
Sijui niseme nini ili muweze kunielewa, na sijui nifanye nini nisaidia wanao onewa
Hakuna heshima nivurugu mechi kwenye jamii, hakuna utii wala mafunzo ya unabii
Nawezi wamifukoni wanachomwa moto kinyama, wengine hawajaiba wanapewa kesi kwa uhasama
Nani atakaye jua na sharia ipo mikononi, watu wa bongo mbona hamna utu moyoni
Vijana wamejibana wapate mtaji wa biashara, mnawaita machinga ingawa si wote kutoka mtwara
Mbaya kuliko yote mnapo vunja vibanda vyao, wengine walikuwa wezi je warudie zama zao?
Ni mshike mshike some times vita na mapolisi, wao na sisi rungu na pingu kama ibilisi
Huku kwetu uswahilini ni mambo ya kila siku, na nikama kuibiwa cheni kwenye ngoma ya mchiriku
Wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi, wanatamani wangezaliwa Brunei wamwage radhi
Masista duu wa bongo wanazidi kupanda chati. Huwezi kujua yupi wa kigogo yupi wa masaki
Mabrother majina yao ya asili hawayataki. Bitozi nyangema anataka aitwe Tupac
Ni burudani tosha hivyo ni vijimambo tu, wabongo tuna title kubwa lakini hatuna kitu
Unajua mustakabali wa ma supa staa wa bongo, lazima ufuzu chuo kikuu cha mbwembwe za uongo
City center ofisi ni mtu alipo simama, hata muhuri wa ikulu unapata haina gharama
Ngoma inakuwa nzito mnapokutana matapeli, akili kumkichwa ukilemaa umeachwa feli
Aliye uziwa cheni katoa hela bandia, aliye pokea hela nae kauza cheni ya bandia
Tulio zoea jiji tunasema ngoma droo, na unaseti mambo mengine yaende kwenye mtandao
Bongo eeeh Bongo Dar es salaam utalia lia liaaa Bongo Dar es salaam
Kaachonjo eeh ndani ya Dar es salam, utalia lia liaa ndani ya Dar es salaam
Katikati ya jiji hata ufikiri deal haziji, ukitaka ku win bongo cheza deal na wale magwiji
Naona vijana wa bongo wanapenda safari kafiri, hata mkoba hawana tengua kitendawili
Safari bado ningumu jama msiende kwa nguvu ya ndumu pumbavu ujinga sumu acha mwenyezi awa hukumu
Changa uchange uende kiwanja unachotaka, funga mkanda unavyotaka
Maskani kimara watu kilasiku mamtoni, Jonas kiwia wasalimie washngton
Ukiweza pita taxes mpe hi chie sam na mkumbushe uzushi wa bongo dar es salaam
Sinza ya leo kila baada ya nyumba baa, na zote zina, jaa hapo ndipo utakapo shangaa
Na kwenye night club ni lundo la kaka powa, huwezi ukaamini jinsi walivyojipodoa
Upinzani jadi bongo haupo simba na yanga, matonya na makamba na city na wamachinga
Nakali kuliko zote upinzani konda na denti, wanaposhikana mashati tu dent anapoketi
Hakuna mnyonge wala anaye kubali kushindwa, ngoma ngondoigwa na wote wanataka ubingwa
Na watu wana magari hadi ya milioni 200, kwa mbongo wa kawaida baiskeli kitenda wili
Wasio amini ni wale wenzangu na mimi, walio na imani aliyeko juu mgoje chini
Mtangoja milele na mtakufa bila kelele, kama walivyofanya wafuasi wa kibwetere