kaida wa ngara
Member
- Jul 14, 2020
- 72
- 67
Membe ange nyuma ya lisu jiwe xanne axubuhi ngerudizake chato mapemaaaaa
Sasa nakuona VEMA sanaaaaa Rafiki💯✅✅Afro sinema
Ungechelewa ningekuita rafiki, na hapa kuna shamrashamra za mbobezi.Sasa nakuona VEMA sanaaaaa Rafiki💯✅✅
Afadhali na yeye amepata nafasi ya kupokea kibegi hicho, huenda itamsaidia kuondoa msononeko wa akili. Lowasa alipata kubeba kibegi hicho kutokea CHADEMA na kuahidi mafuriko ambayo hayakutokea lakini sasa hivi hana msononeko tena. Baada ya uchaguzi, nadhani hatakuwa na msononeko wala kelele tena.Leo tarehe 17 Julai 2020, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu na Mwanachama wa ACT Wazalendo Ndugu Bernard Membe atazungumza na waandishi wa habari.
Ukumbi: Ofisi ya ACT Wazalendo Magomeni, Dar es salaam.
Muda: Saa 8.00 Mchana.
Waandishi wote mnakaribishwa.
Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.
17 Julai 2020.
=========
UPDATES
========
Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Mstaafu Tanzania Bernard Membe mchana huu amechukua fomu ya kugombea Urais kupitia chama cha ACT WAZALENDO ikiwa ni siku moja tu baada ya kupokewa rasmi kwenye Chama hicho.
Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.
Siasa:
Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.
Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.
Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyakuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo. Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.
Mafanikio:
Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.
Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.
Zaidi, soma:
CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama
News Alert: - Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka
Uchaguzi 2020 - Bernard Kamilius Membe: Nitagombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo
Wasifu wa Bernard Kamilius Membe
Mbona chadema mnamhofia sana Membe?Leo atakuwa anatangaza raimi kugombea uraisi.
Lissu akirudi,kibao kitageuka, na kuna hatari ya kugawana kura.
Ccm Mwisho Wenu Umekaribia...
Nchi Yetu Sote...
Na Mwaka Huu Mtaelewa kwa nini Kaka Man Aliimba Kama Noma na Iwe Noma.
Eeenh mkuu 'Alpha 13'.Okay tujibizane kwa hoja.
Sheria zina reference point ama grounds. Sheria zote zimetungwa baada ya kuchambua jema na baya "Morals".
Morals karibu zote tulizonazo zilikuepo kabla hata ya kuzaliwa (pia kabla ya wananchi wote waliopo hai leo).
Pia tunaweza vutana kwa hoja milele nani mwanzilishi wa Morals kati ya Mungu au mwanadamu tusimalize leo.
Naomba unisahihishe mwalimu, nimekosea wapi?Eeenh mkuu 'Alpha 13'.
Wewe ungekuwa mwanafunzi wangu unapata yai hapo hapo!
Unatoka kwenye mada unapiga zako kusikohusika kabisa na mada.
Usimfanye mwalimu akuone wewe hufundishiki.Naomba unisahihishe mwalimu, nimekosea wapi?
Siasa tuSijui kwanini huyu jamaa simuamini kabisa.
Some lilikua wananchi vs sheria. Mwenzangu alitegemea niwatetee wananchi, nilipochangua upande wa sheria akajanikosoa "wananchi ndio watunga sheria kupitia wawakilishi". Nikamjibu sheria zinatungwa kutoka kwenye morals "elimu ya mema na mabaya" ambayo ilikuepo kabla ya wananchi wote tuliopo sasa.Usimfanye mwalimu akuone wewe hufundishiki.
Huwezi kusoma majibizano yalipoanzia ukajua umetoka nje ya somo? Sasa unataka ulishwe kabisa?
Mtatunga sana hizi hadithi zisizo na miguu wala vichwa.Kwa upande mwingine: TL (simpigii chapuo) mwisho wa mwezi anakuja. Atadakwa fasta kwa kisingizio cha kesi za kuungwa ungwa. Usiku huo wa kuja TL "Elites" hawatalala na atadakwa hapo hapo uwanjani.
Maskini kaamua kujikana TL.Hayupo upande wao,hashiriki meza yao,hana urafiki nao na shilingi yao kaikataa. Usiku huo "wa kudakwa kwa TL,kwa kuwa ni mwisho wa mwezi "jasusi mbobezi" na "Kijana wa Mwandiga" wao watakuwa "ushuani" Masaki au Oysterbay wamelala na wake zao,wana amani tele moyoni huku wakisubiri kutimiza mpango wao oktoba 2020 na wapewe chao.
Basi ngoja niseme sipo kwenye 'mood' wa kuku'engage' kwa sasa.Some lilikua wananchi vs sheria. Mwenzangu alitegemea niwatetee wananchi, nilipochangua upande wa sheria akajanikosoa "wananchi ndio watunga sheria kupitia wawakilishi". Nikamjibu sheria zinatungwa kutoka kwenye morals "elimu ya mema na mabaya" ambayo ilikuepo kabla ya wananchi wote tuliopo sasa.
Ili kupunguza mvutano nikaenda hatua moja mbele kuonyesha chimbuko la elimu hii ya mema na mabaya mizizi yake ipo kwa Mungu.
Point yangu ni hii; sheria ndio muongozo, viongozi inawapasa wazisimamie pia wawe mfano kwa kuzitii ili wananchi wote tuzifuate.