Uchaguzi 2020 Bernard Membe achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,875
Leo tarehe 17 Julai 2020, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu na Mwanachama wa ACT Wazalendo Ndugu Bernard Membe atazungumza na waandishi wa habari.

Ukumbi: Ofisi ya ACT Wazalendo Magomeni, Dar es salaam.

Muda: Saa 8.00 Mchana.

Waandishi wote mnakaribishwa.

Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.

17 Julai 2020.

=========

UPDATES

========

Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Mstaafu Tanzania Bernard Membe mchana huu amechukua fomu ya kugombea Urais kupitia chama cha ACT WAZALENDO ikiwa ni siku moja tu baada ya kupokewa rasmi kwenye Chama hicho.

Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Siasa:
Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.

Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.

Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyakuwa anashikilia wadhifa huo - Dr Asha Rose Migiro - kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo. Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.

Mafanikio:
Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.

Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.

Zaidi, soma:

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

News Alert: - Bernard Membe apokelewa rasmi ACT–Wazalendo. Atoa ahadi kemkem endapo watashika madaraka

Uchaguzi 2020 - Bernard Kamilius Membe: Nitagombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Wasifu wa Bernard Kamilius Membe

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
 
Leo tarehe 17 Julai 2020, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu na Mwanachama wa ACT Wazalendo Ndugu Bernard Membe atazungumza na waandishi wa habari.

Ukumbi: Ofisi ya ACT Wazalendo Magomeni, Dar es salaam.

Muda: Saa 8.00 Mchana.

Waandishi wote mnakaribishwa.

Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.

17 Julai 2020.
Kama nilivyosema jana, anataka urais kisa cha kujiunga na ACT, pia nilisema anatamani vyama vyote viungane na kumchagua yeye kuwa mgombea urais, watu kama hawa unawaona ndani nje jinsi walivyo wehu na walafi wa madaraka. 😂😂😂
 
Ndipo mlipoifikisha nchi.. Lakini sidhani kama mna tafakuri jadidi kwenye matendo yenu hayo
Siasa zetu (pia dunia nzima) zilipofikia si pazuri.

Miongozo mara kadhaa imekua ikitolewa kulingana na haiba ya kiongozi mathalani ya sheria kuwalinda wahanga bado ugandamizaji umeshamili.
 
Kama nilivyosema jana, anataka urais kisa cha kujiunga na ACT, pia nilisema anatamani vyama vyote viungane na kumchagua yeye kuwa mgombea urais, watu kama hawa unawaona ndani nje jinsi walivyo wehu na walafi wa madaraka. 😂😂😂


Hata Magufuli anawaita akina Tundu Lissu ni walafi wa madaraka.
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom