Beno Malisa amuomba Rais Samia msamaha

Beno Malisa amuomba Rais Samia msamaha

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Beno Malisa, amemuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema ametambua makosa yake na bado ana nia ya kulitumikia taifa katika nafasi yoyote atakayopangiwa.

Malisa ameyasema hayo leo mkoani Tabora wakati wa makabidhiano ya ofisi kwa Mkuu mpya wa Mkoa huo, Angelina Mabula, akieleza kuwa bado ni kijana na mzalendo mwenye dhamira ya kulitumikia taifa.

Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kumuombea Rais Samia ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kuliongoza taifa.

Soma Pia : Beno Malisa atenguliwa Ukuu wa Mkoa wa Tabora, Angeline Mabula achukua nafasi yake


the gentleman has demonstrated a very high level of leadership maturity in politics by acknowledging where he went wrong.

well done Beno Malisa :KasugaYeah:
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Beno Malisa, amemuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema ametambua makosa yake na bado ana nia ya kulitumikia taifa katika nafasi yoyote atakayopangiwa.

Malisa ameyasema hayo leo mkoani Tabora wakati wa makabidhiano ya ofisi kwa Mkuu mpya wa Mkoa huo, Angelina Mabula, akieleza kuwa bado ni kijana na mzalendo mwenye dhamira ya kulitumikia taifa.

Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kumuombea Rais Samia ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kuliongoza taifa.

Soma Pia : Beno Malisa atenguliwa Ukuu wa Mkoa wa Tabora, Angeline Mabula achukua nafasi yake


Vipi kwenda kujiajiri? Si huwa wanahimiza vijana kujiajiri? 😂😂😂
 
Hivi vyeo uchwara kama RC na DC ndii vimezalisha uchawa kama huu.

Kwenye ila rasimu ya katiba mpya vilipendekezwa kufutiliwa mbali na kiwepo cheo kimoja tu ambacho kitakua kinapatikana kwa merit na watu wataomba nafasi na wawe ni wa eneo husika maana ndio wanajua matatizo ya hapo.

I
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Beno Malisa, amemuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema ametambua makosa yake na bado ana nia ya kulitumikia taifa katika nafasi yoyote atakayopangiwa.

Malisa ameyasema hayo leo mkoani Tabora wakati wa makabidhiano ya ofisi kwa Mkuu mpya wa Mkoa huo, Angelina Mabula, akieleza kuwa bado ni kijana na mzalendo mwenye dhamira ya kulitumikia taifa.

Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kumuombea Rais Samia ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kuliongoza taifa.

Soma Pia : Beno Malisa atenguliwa Ukuu wa Mkoa wa Tabora, Angeline Mabula achukua nafasi yake

Huyu anajua kosa alilolifanya
 
Aliteleza nini?

Aliwakosea Watanzania au alimkosea Rais, au aliwakosea Watanzania na Rais?

Kama alimkosea Rais tu, kwa nini asingemfuata Rais akamuomba radhi yeye in private?

Kama aliwakosea Watanzania pia, kwa nini hakuwaonba radhi Watanzania na kusema alikosea nini?

Kwa nini Watanzania wanasikia mtu anaomba radhi nusunusu, kwa mafumbofumbo, bila kuelewa kisa kamili?
Taifa linaenda enda tu bila dira 😎
 
Mlio karibu nae mwambieni anakoelekea atajikuta sarawali imetundikwa ukutani huku kipande cha nyama ngumu kimemuingia kinamtilia maji ya moto tumboni.

Malisa siyo wachaga hao sasa mchaga wa wapi huyu analia analia hivi badala atafute gun aende zinakokusanywa hela abebe?
Unajifanya unapinga, na hapa unapigia chapuo.
😂😂😂
 
:Mi kwa mtazamo wangu, na maoni yangu, nadhani inabidi niweke sawa kwamba kwa maneno machache sana niseme mimi kama mm naweza kuwa na mtazamo ambao Nitapenda kusema kuwa kwa maoni yangu naona ni vema kueleza kuwa inabidi sasa niweke sawa maelezo yangu kuwa hili suala ni ambalo kwa maoni yangu naona kuwa maneno ambayo naweza kueleza kwa ufundi sana na kutokana na mawazo yangu. Sasa nimalizie kwa kusema kuwa naona mawazo yangu ambayo yanaeleza kuwa mtazamo ambao mimi binafsi ningetamani kusema kuwa inabidi maelezo haya ambayo nayatoa ni kwamba, kwa maneno machache nieleze kuwa naweka wazi ya kwamba maoni yangu na mawazo yangu naeleza kuwa mtazamo huu ni kueleza kuwa sina la maana ndugu zangu.😁
 
Back
Top Bottom